Kelvin Haule ambaye aliwika akiwa na tukuyu stars,maji maji na taifa stars
Alipoishia jana……………..
HAULE ALIPOCHIPUKIA KISOKA |
“Kuna kipindi nilitekekezwa na Yanga hotelini mwaka 1987 wakati nipo na Yukuyu Stars kwa kipindi cha mwenzi mmoja bila kujua hatima yangu ni ipi huku wakinipa matumaini ya kunipa mkataba lakini tulishindana baadae kwa kuwa Yanga waligoma kuniamishia kikazi jijini Dar es salam na wakanitaka nicheze bila kazi kwa kuwa kipindi kile kila Timu ililazimika kumtafuta mchezaji kazi nje ya soka nikaamu kuachana nao na na kujiunga na Wanalizombe mjini Songea.
Songa nayo…………..
Tukio la kuvunjika mguu lilininyima usingizi
“Stasahau wakati nilipovunjika mguu mwaka mwaka 1987 katika uwanja wa CCM kirumba mwanza katika michuano ya Shimmuta,wakati ya mechi kati ya NMC-shirika la usagaji pamoja na BIT timu ambayo iliusisha makampuni ya biashara, katika mechi ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa kutokana na wachezaji wengi wa ligi kuu kusajiliwa na timu hizo.
“katika mechi hiyo kwa upande wetu NMC tulishinda goli 2-1 magoli ambayo nilifunga mimi mwenyewe,lakini Vegasitus Limbu alinichezea rafu mbaya sana na akanivunja mguu,niliumia sana lakini mungu akajaria nikaudumiwa vizuri na kurejea uwanjani.
KELVIN HAULE KULIA |
Mechi ninayoikumbuka
“Naikumbuka sana mechi ya clab Bingwa afrika raundi ya Tatu, kati ya Maji Maji na Fc Leopard ya Kenya ilikuwa ni mechi kali na ngumu sana kwa upande wetu ambapo mchezo wa kwanza ulifanyika jijini Arusha katika uwanja wa Amri Abeid,walituchalaza goli moja mtungi hali ambayo ilikatisha tama ya kusonga mbele.
“katika mechi ya marudiano nchini Kenya katika uwanja wa Moi Kasalani mechi ikianza kwa mashambulizi ya kila upande wakati wote wa mchezo na hadi mwamzi anapuliza kipenga cha mwisho FC Leopard 0,Maji Maji mtungi na tukatupwa nje kabasa ya mashindano.
Timu za Tanzania kufanya vibaya
“wachezeji wengi wanaochezea timu zetu za hapa nyumbani hawana uzoefu mkubwa wa kushindana tofauti na wachezaji wa timu za wezetu ambao wanacheza mechi nyingi kushinda hapa nyumbani hilo ni tatizo kubwa Tff lazima walifikili.
“vile vile hapa Tanzania wachezaji wanaibuka tu kutokana na kucheza mitaani na kucheza timu kubwa ambazo zinatuwakilisha katika mashindano ya kimataifa,kwa wenzetu wanakuzwa katika shule za michezo toka wakiwa wadogo,hali ambayo inapelekea timu zetu kufanya vibaya kimataifa.
Endelea kufuatilia kesho tarehe 17-04 atahitimisha historia ya maisha yake.
Chapisha Maoni