Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Na Sophia Mwaipyana,Mbeya
Timu ya Mbaspo Fc imefanikiwa kutwa ubigwa wa ligi ya wilaya ya Mbeya Mjini baada ya kuwafunga timu ya African Boy magoli 3-0  katika uwanja wa magereza mkoani hapa.

Timu ya Mbaspo Sc ilionyesha ushindi wa mapema kwani ilianza kwa kasi na kuutawala mpira kila wakati  huku wapinzani wao wakijaribu  kujibu mapingo  bila mafanikio.

Christophar Boniphac ndiye aliwainua mashabiki wa timu yake baada ya kupanguwa ngome ya wapinzani wao  dakika ya 41 na kuiandikia goli lakwanza timu hiyo.

Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu ya Mbaspo Sc ilikuwa ikiongoza kwa goli moja wakati wapinzani wao walikuwa   hawajaambulia kitu.

Kipindi chapili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiriko ya wachezaji ,lakini timu ya African Boys ilienderea kubanwa koo kwani walishindwa kupanguwa ngome ya wapinzani wao .

Goli la pili lilifugwa na Eria Jimmy baada ya kumalizia pasi iliyo pigwa na Christophar kisha ikagonga mwamba na kurudi uwanjani ambapo ilimaliziwa n Erie kwa shuti kalili lililoenda kujaa wavumi moja kwa moja wakati goli la tatu lilifugwana  Musa john,dakika ya 50 na 86.



Magoli hayo yaliifanya timu ya Mbaspo Sc kufikisha  pointi 37 wakati nafasi ya pili kishikwa na timu ya ilemi Fc  ikiwa na pointi 36 ambazo zote zita wakilisha wilaya ya Mbeya mjini.


Chapisha Maoni