Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Ramires celebrates his stunning third goal by putting the ball under his shirt as he congratulated by Cesar Azpilicueta
Ramires (right) struck his effort with such power that he had both feet off the ground at one point
Ramires's goal flew in at an incredible speed of nearly 60 miles per hour - leaving Kasper Schmeichel in the Leicester goal no chance
Terry (right) flicks home from close range after a scramble in the Leicester box following a Chelsea corner
Didier Drogba (centre) was the star of the show for Chelsea - and he was leading his team-mates in celebrations at full time

Chelsea walitoka nyuma na kuilaza Leicester City 3-1 Jumatano na sasa wanahitaji ushindi mmoja pekee kutwaa taji la Ligi ya Premia kwa mara yao ya kwanza katika miaka mitano.
Chelsea walielezwa kuwa "wasiofurahisha” na mashabiki wa Arsenal wakati wa sare ya 0-0 debi ya London Jumapili na hawakuridhisha kwenye mechi hiyo dhidi ya Leicester waliokuwa wakisaka ushindi wa tano mtawalia ligini katika juhudi za kujiimarishia nafasi ya kunusurika ligi kuu.
Marc Albrighton aliweka Leicester mbele kipindi cha kwanza kikielekea kumalizika lakini Didier Drogba akasawazisha muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza kabla ya mabao ya dakika za mwisho kutoka kwa John Terry na Ramires kuhakikisha Chelsea watatwaa taji iwapo watashinda dhidi ya Crystal Palace Jumapili.
Chelsea wana alama 80 kutoka kwa mechi 34 huku mabingwa wa msimu uliopita Manchester City wakiwa nambari mbili na alama 67. Arsenal wamo nambari tatu wakiwa pia ana alama 67 lakini wana mechi moja hawajacheza.
Leicester walisalia nambari 17 na alama 31 kutoka wka mechi 34, alama moja mbele ya Sunderland walio nambari 18 lakini vijana hao wa Nigel Pearson wamecheza mechi moja zaidi.
“Ninafikiri labda tunaogopa kushinda ligi,” Drogba aliambia Sky Sports. "Kushinda mechi mbili na tunatawazwa mabingwa lakini hii ilikuwa ngumu. Tunatambua Leicester.
"Kipindi cha pili tulirejea na tulitaka kuhakikisha mechi dhidi ya Crystal Palace ndiyo itatupatia taji la ligi.
“Huwa hatutambulizi vya kutosha. Tunaongoza ligi, tuna alama nyingi zaidi na watu wanasema hatuvutii.”
Leicester walikaza kamba mapema kwenye mechi lakini wakalazimika kufanya mabadiliko mawili ya haraka kutokana na jeraha, Matty James akaingia nafasi ya kiungo wa kati Andy King naye Ritchie De Laet nafasi ya difenda Robert Huth.
Mdundo wa wenyeji hata hivyo haukuathirika sana na mkabaji wa kushoto Paul Konchesky alimlazimisha Petr Cech kufanya kazi ya ziada kuokoa katika mlingoti wake wa karibu kabla ya Chelsea kuondoa mpira eneo la hatari baada ya mtafaruku eneo la hatari.
Leicester walichukua uongozi baada ya Jamie Vardy kutuma krosi eneo la hatari na Albrighton akatumia vyema kuteleza kwa Cesar Azpilicueta na kumbwaga Cech.
Lakini huku Leicester wakiwa bado wanaimba "Tunasalia juu”, Chelsea walisawazisha Droga alipofunga krosi ya Branislav Ivanovic dakika ya 48 na kusawazisha.
Chelsea walidhibitiwa vyema na Leicester lakini wageni hao walinyakua bao la uongozi dakika ya 79 Gary Cahill alipopiga kwa kichwa kona ya Cesc Fabregas na kuielekeza kwenye goli na Terry aliyekuwa karibu akambwaga kipa Kasper Schmeichel.
Ikiwa bao la Chelsea lilikuwa la kibahati tu, la tatu halikuwa kwani kiungo wa kati wa Brazil Ramires alituma wavuni kombora la guu la kushoto kutoka nje tu ya eneo la hatari na kupeleka klabu hiyo ya London karibu na taji.


Chapisha Maoni