Chelsea walijipata nyuma kutokana na bao la Marc Albrighton kabla ya mapumziko baada ya kipindi cha kwanza kisichovutia ambapo hawakucheza vyema.
Kocha huyo Mreno alikiri kwamba aliwasomea wachezaji wake muda wa mapumziko kabla ya mabao ya kipindi cha pili kutoka kwa Didier Drogba, John Terry na Ramires kuwapa ushindi na kuwaacha wakihitaji kulaza Crystal Palace pekee Jumapili ndipo washinde taji lao la kwanza tangu 2010.
"Nikiwaambia kwenye televisheni kile nilichosema kutakuwa na 'pe pe pe’. Pe pe pe nyingi,” alisema akizungumza na BBC.
Nahodha Terry alikiri kwamba "walikeleleshwa muda wa mapumziko” lakini hakufafanua hasa ni nini Mourinho alisema kilichowafanya waamke kipindi cha pili.
Mabadiliko katika uchezaji wa kipindi cha pili yalionyeshwa vyema na Drogba, aliyeonekana kulemewa kipindi cha kwanza lakini baada ya mapumziko alifufua kumbukumbu za ukali wake kama mshambuliaji.
Chelsea walibomoa vijana wa Leicester ambao walikuwa wameshinda mechi zao nne zilizotangulia wakijizatiti kusalia ligi kuu.
Huku mjadala kabla ya mechi ukiangazia sana iwapo uchezaji wa Chelsea “si wa kuvutia”, walijitetea vya kutosha na kucheza vyema na kupata bao kali la tatu kupitia kiungo wa kati Ramires.
"Mechi ya leo ilinivutia mimi," Mourinho akaongeza. "Kuwa nyuma muda wa mapumziko si jambo lisilovutia – ni kuwa na presha.
“Jinsi tulivyocheza kipindi cha pili, labda ndio uchezaji bora wa timu hii katika kipindi cha mwezi mmoja, uchezaji mzuri sana.
“Aprili kila mtu alitarajia tudondoshe alama dhidi ya Arsenal na Manchester United, lakini Aprili ndio mwezi ambao tulibomoa wapinzani wetu.
“Tulishinda kila mechi isipokuwa hiyo ya Arsenal na kwa hivyo nina furaha. Sasa tunahitaji alama tatu zaidi pekee.”
Alionya mashabiki hata hivyo dhidi ya kucherehekea mapema, kabla ya mechi hiyo dhidi ya Palace.
"Stamford Bridge iko tayari kusherehekea lakini ninaweza kuwaomba jambo moja nalo ni kwamba wasisherehekee,” akasema.
“Tunataka kushinda Jumapili lakini itakuwa mechi ngumu. Stamford Bridge lazima iwe tayari
Chapisha Maoni