Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.






Jackson Mayanja wa Kagera Sugar ambaye mechi ijayo kikosi chake kitakuwa wageni wa Ndanda mjini Mtwara, Jumamosi alisema anajua ugumu uliopo kwenye mechi hiyo, lakini hayuko tayari kuona Ndanda wanaipoteza.
 
Wakati kocha Tom Olaba wa Ruvu Shooting akieleza: “Nimebakiza mechi na Prisons na Polisi Morogoro, ni michezo migumu, lakini niwaambie mashabiki, nafasi ya kushuka daraja kwa kikosi changu wasahau.
Kocha wa Polisi Moro, John Tamba akieleza kuwa nafasi pekee aliyonayo ni kushinda mechi zake mbili zilizosalia na si vinginevyo.
Naye Mbwana Makata wa Prisons alisema anachokifikiria ni kujinasua katika jahazi la kushuka daraja na kusisitiza kuwa anahitaji pointi tatu kwenye mchezo wao ujao na Mbeya City.
“Mbeya City na sisi ni kama ilivyo Simba na Yanga, hivyo najua mchezo utakuwa mgumu, lakini tuko fiti tunachokiangalia ni kutoshuka daraja.
Kocha wa Ndanda, Meja Mstaafu Abdul Mingange pia alieleza kufikiria pointi sita katika mechi zake mbili na kusisitiza kuwa bado ana nafasi ya kutoshuka daraja kama akishinda zote.



Chapisha Maoni