Miaka 35 iliopita nikiwa na
umri mdogo sana. Wakati huo nikisoma nursery kwenye shule ya Tanganyika... Nakumbuka
mchezo wangu rasmi wa kwanza kushuhudia wa timu ya taifa ya Tanzania ambayo
ilikuwa ikicheza na nchi ya Nigeria (Green Eagle's).
Nimeita
kumbukumbu nusunusu sababu ya umri mdogo niliokuwa nao wakati huo. Lakini ktk
nusu ninazozikumbuka. Nilipanda basi la timu ya taifa ambalo kama sikosei
kipindi hicho FAT (sasa tff) walikuwa wanalimiliki.
Nakumbuka
timu iliondokea hoteli ya Africana na sisi tulikuwa kule kwa wiki 4 na mzee ambaye
alinipigia pande kupanda basi la
mashujaa wale ambao kwangu sitawasahau kamwe.
Ninazo
kumbukumbu pia bendi ya DDC Mlimani Park ilitumbuiza kabla na wakati wa
mapumziko katika mechi ile murua kabisa. Ingawa kwa siku zile sikujua kama wale
ndio sikinde ngoma ya ukae!
Nusunusu
yangu inanikumbusha kikosi kilichoanza game ile.
1-Juma
Pondamali
2-Leopard
Tasso Mukebezi
3-Hasan
Zito Kiaratu
4-Jellah
Mtagwa(C)
5-Ishaka
Hassan Chukwu
6-Salim
Amiri
7-Omari
Hussein
8-Mohammed
Rishard Adolph
9-Peter
Tino
10-Mohammed
Salum
11-Thuweni
Ally
Kocha
Mkuu alikuwa Joel Nkaya Bendera,
kwangu
hii timu ambayo ilitoka kucheza fainali za mashindano ya Mataifa huru ya Afrika
(Afcon) ilikuwa timu bora ya taifa kuwahi kuiona ingawa nilikuwa mdogo!
Timu
hii ilimkosa nahodha wake mkuu Leodgar Chillah Tenga ambaye alikuwa ameumia kwenye
mchezo wa kombe maarufu siku hzo likiitwa Jengo Cup ambapo timu yake ya pan
African ilicheza na yanga.
Bahati
mbaya hiyo ndiyo ilikuwa game ya mwisho rasmi kwa tenga ambaye aljeruhiwa vibaya
sana goti na baba yangu mkubwa Kitwana Manara ‘Popat’.
Ifahamike
hyo ilikuwa mechiya marudiano dhidi ya africa Magharibi hao ambapo kwenye game
ya kwanza kule Surulele Stadium Nigeria tulitoka suluhu bin suluhu.
Bahati
mbaya kwetu wakatufunga mbili mtungi huku ikitajwa kukosekana kwa tenga
kuliififisha defence line ya Stars. Siku hiyo alitumika defender
chipukizi(wakati huo) Chukwu ambaye ndiye aliyeziba pengo la captain Tenga
Iwapo
kama tungefanikiwa kuwatoa wala pilipili wale. Stars ilikuwa ikutane na Algeria
ambao ndio waliofuzu kucheza Kombe la Dunia la Spain 1982,
Mungu
jalia bahati haikuwa yetu. Lakini tulikuwa karibu kabisa na World Cup kuliko
kipindi chochote cha uhai wa taifa hili!
Katika
miaka yake yote ya uhai wa mataifa yetu mawili. Nchi hizi zmekutana mara tatu
tu. Ukiacha game hizo za kufuzu kwa Kombe la Dunia. Stars na mwewe hawa!
washawahi kukutana pia kwenye mechi ya ufunguzi wa Kombe la Mataifa huru ya
Africa (Afcon) pale Lagos na Stars tukalala 3-1.
Miaka
ya mwishoni mwa miaka ya 1990 tulicheza nao lakini ilikuwa kwenye mechi ya
kufuzu kwa michezo ya Olimpiki ambayo wachezaji wanaoruhisiwa kucheza ni wale
walio chini ya miaka 23.
Mechi
hizi pia wapo hao walitutoa na nakumbuka walikuja na nyota wao Tijan Babangida
ambaye ni ndugu wa winga mahiri wa zamani wa ajax Amsterdam.
Nimeandika
waraka huu mrefu kdogo ili itukumbushe shughuli tuliyo nayo mbeleni. Kwanza
kihistoria baina yetu, pili kiuhalisia kuhusu uwezo wa kabumbu wa wapinzani
wetu hawa ambao wamejaaliwa mamia ya wanasoka wanaocheza soka huko Ulaya.
Najua
kwenye mpira lolote linawezekana.lakini tuendelee na maandalizi yetu huku
tukiomba kwa Mungu pia, na hasa kheri tunaweza kuishangaza Afrika kwa kuwafunga
manguli hawa wa kandanda si Afrika tu bali ulimwenguni kote.
Mungu
ibariki Stars
Mungu
ibariki Tanzania
Amiin
Haji
S.Manara
Chapisha Maoni