Timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania (Twiga Stars)
inaendelea na mazoezi kisiwani Zanzibar kujiandaa fainali za Michezo ya Afrika
(All Africa Games) zitakazofanyika mwezi ujao nchini Congo Brazzavile.
Mara baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya
Taifa ya Wanawake ya Kenya (Harambee Starlets) mwishoni mwa wiki iliypita,
kocha wa Twiga Kaijage ameendelea kufanyia marekebisho yalitojitokeza katika
mchezo huo kwa lengo la kuhakikisha vijana wanakua vizuri kabla ya kuanza kwa
fainali hizo.
Kikosi cha wachezaji 21 pamoja benchi la Ufundi na
kiongozi wa msafaa wanatarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa mwezi Agosti
kuelekea nchini Congo-Brazzavile tayari kwa kushiriki kwa fainali hizo za
Michezo ya Afrika zitakazoanza kutimua vumbi Septemba 3- 19, 2015.
Katika hatua nyingine Shirikiksho la Mpira wa Miguu
chini (TFF) limewaomba wadau, wadhamini, taasisi na mashirika mbalimbali
kujitokeza kuzidhamini timu za Taifa za vijana U15 na Twiga Stars.
Twiga Stars inayokwenda kushirki fainali za michezo ya
Afrika inahudumiwa na TFF pekee, hivyo ni nafasi nzuri kwa mashirika,
wafanyabiashara kujitokeza kuidhamini timu hiyo ya wanawake inayokwenda
kupeperusha bendera ya nchi kwenye michuano hiyo.
Aidha timu ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 pia
inahudimiwa na TFF pekee katika program ya kuandaa kikosi bora kitakachoshiriki
kwenye kuwania kufuzu kwa fainali za vijana Afrika mwaka 2017.
TFF peke yake haina uwezo wa kuziandaa timu hizo, hivyo inawaomba wadhamini kujitokeza kudhamini timu hizo katika progam za mapinduzi ya mpira wa miguu nchini.
Chapisha Maoni