Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


 Webb Howard

Manchester United waliwika mechi yao ya kufuzu kwa hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Club Bruges na kufanikiwa kurejea dimba hilo kuu la klabu Ulaya, baada ya kukaa mwaka mmoja kwenye baridi.
Wayne Rooney alifunga mabao matatu na kuwapa ushindi wa 4-0 dhidi ya klabu hiyo ya Ubelgiji mechi ya marudiano Jumatano na kukamilisha ushindi wa jumla wa 7-1 kwa mabingwa hao mara tatu wa Ulaya.
"Ninadhani tulikuwa tumejipanga vyema. Tulicheza kiasi kwa urahisi kuliko awali,” meneja wa United Louis van Gaal aliambia BT Sport. "Unaweza kuunda mianya na tulifunga na kwa hivyo hilo ni jambo njema pia.”
Van Gaal alifurahia kwamba Rooney alifikisha kikomo ukame wake wa mabao uliodumu mechi 10.
"Kila bao humuongezea Imani mchezaji, hata Wayne. Ninamfurahia sana,” Mholanzi huyo alisema.
“Ana mtazamo bora zaidi. Wachezaji kama hao wa kiwango kama hicho lazima mwishowe watajikwamua.”
United wamefunga mabao mawili pekee mechi zao za kwanza tatu Ligi ya Premia msimu huu lakini kutofungwa na Bruges Jumatano ilikuwa mara yao ya nne kutofungwa katika mechi nne.
Watasafiri Swansea City Jumapili, timu iliyowalaza mara mbili ligini msimu uliopita.
“Ulikuwa usiku mwema kwa Manchester United lakini sasa tunaangazia Swansea City," Van Gaal alisema.
"Msimu uliopita tulipoteza alama sita kwa na kwa hivyo tunaweza kuboresha.”


Chapisha Maoni