Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Kipa iliyewai kuchezea klabu za Tanzania Prisons,
Moro United, Yanga SC, St.George ya Ethiopia,
African Lyon, Bandari FC na  Gor Mahia FC za
Kenya, Simba SC na timu ya Taifa ya Tanzania,
Taifa Stars, Ivo Mapunda amelaani vikali tabia
ya Jums Nyosso kuwadhalilisha wachezaji
wenzake kwa kuwashika sehemu za makalio.
“Binafsi nachukua nafasi hii kuwaomba
wachezaji wenzangu, wanaocheza na waliowahi
kucheza soka, wadau wote pamoja na
mashabiki wa ndani na nje ya nchi KULAANI
kwa nguvu zote tabia na vitendo vya aibu na
udhalilishaji anavyofanya mchezaji mwenzetu
Nyosso” ameandika Ivo katika akaunti yake ya
facebook mchana huu.
“Hii ni aibu, siyo yake pekee bali ni yetu sote
wachezaji hasa wa medani ya kimataifa.
Tunaonekana ‘hopeless’ pia na hata kukosa
nafasi ya kwenda nje ya kucheza soka kutokana
na tabia dhalimu. Tunaomba adhabu yake
itakayotolewa iwe fundisho kwa wengine wenye
tabia kama hii. Wanajifunza nini watoto au
vijana wanaochipukia katika soka kwa huu
udhalilishaji ukizingatia Nyosso ni mchezaji
mkubwa?”



Chapisha Maoni