Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



sajili ambazo zilikwama dakika za mwisho na
kuhusishwa na figisufigisu kibao kutoka pande
fulani fulani, karibu kutazama hapa chini…
FABIO COENTRAO
Mwaka 2013 beki huyu wa kushoto alihusishwa
kuhamia Old Trafford. Timu za Real Madrid na
Man U zilishakamilisha kila kitu ila kosa
walilolifanya ni kuchelewa kukusanya nyaraka
za usajili kwa wakati. Kipindi hiki Man U
walikuwa na mabeki wa kushoto, Patrice Evra
na Alexander Buttner, kitu hiki ndicho kilikuwa
kinawapa kiburi kuchelewesha nyaraka hizi hadi
dirisha kufungwa. Pia United walipewa kiburi na
beki Leighton Baines wa Everton kwani kipindi
hiki walikuwa wanaamini watanasa saini yake.
JOAO MOUTINHO
Kiungo wa kimataifa kutoka Ureno alitarajiwa
kusaini Tottenham mwaka 2012 wakati timu hii
ipo chini ya Meneja Andre Villas Boas. Wakati
Spurs ikidhani imempata mrithi wa Luca Modric,
madudu ya dakika za mwisho yalikwamisha
uhamisho huu na kupelekea Moutinho kwenda
Monaco. Inasemekana Spurs walikamilisha
taarifa saa 3 usiku ila majadiliano yalikwenda
hadi saa 7 usiku na hatimaye tarehe 1
September kufika bila maafikiano kufika baina
ya timu zote. Kulikuwa na majadiliano ya
pande 3, vilabu viwili na ule upande wa mmiliki
wa mchezaji. Mwisho wa siku usajili huu
ulikwama dakika za mwisho.
ANDER HERRERA
Japokuwa kwa sasa ni mchezaji wa Manchester
United, ila alipaswa kuhamia kwenye timu hii
mapema sana mwaka 2013 lakini Atletco Club
Bilbao ilipishana na Man U dakika za mwisho
na hatimaye uhamisho huu kukwama mwaka
2013. Inaelezwa timu hizi zilishindwana kwenye
maafikiano ya bei licha ya wanasheria wa vilabu
hivi kukutana mara kwa mara. Baada ya dili hili
kukwama kipindi cha kiangazi hatimaye
mwaka 2014 Man U ilimnasa mchezaji huyu na
kwa sasa ameingia kwenye vitabu vya wachezaji
waliosajiliwa na Man U.
YEVHEN KONOPLYANKA
Winga huyu kutoka Ukraine alihusishwa na
kuhamia Anfield mwaka 2014 na tayari baadhi
ya makaratasi yalisha sainiwa na vilabu hivi
viwili vya Liverpool na Dnipro. Mmiliki wa
Dnipro tayari alishatangaza muda wowote winga
huyu atakwenda Liverpool. CEO wa Liverpool Ian
Ayre tayari alitarajiwa kwenda Ukraine
kukamilisha kila kitu kabla dirisha halijafungwa
ila cha kushangaza uhamisho huu ulikwama
dakika za mwisho hadi dirisha linafungwa.
Liverpool walikwama kumpeleka mchezaji huyu
Merseyside kutokana na uzembe mwishoni
kabisa.
DAVID DE GEA
Huu ni mfano mzuri kwa kipindi hiki kwani
ilifikia hatua ya mlinda mlango huyu kutaka
kuuza kila kitu pale Uingereza kwa kuamini
kuwa anakwenda kwao Hispania ila dakika ya
mwisho kabisa mambo yalikwenda kombo. Kuna
mambo mengi yalitokea juu ya uhamisho huu ila
suala la ada ya uhamisho lilichelewesha usajili
huu na makubaliano ya dakika za mwisho
yalifanya muda kutokuwa rafiki na hatimaye
usajili huu kuwa ndoto. Kila timu imeonekana
kutoa lawama kwa mwenzake na ukweli unabaki
kuwa dakika za mwisho mambo ndio
yaliharibika kabisa.



Chapisha Maoni