MBEYA CITY COUNCIL FOOTBALL CLUB
TAARIFA KWA UMMA
Bodi ya klabu ya Mbeya City ilikutana leo tarehe
29.09.2015 kwa dharula kulijadili suala ambalo
hivi sasa linaendelea kujadiliwa katika Umma wa
wanamichezo nchini likimuhusisha mchezaji wa
timu yetu Juma Said maarufu kama “Nyoso”
baada ya mchezo kati ya timu yetu na Azam Fc
uliochezwa tarehe 27.9.2015 katika uwanja wa
chamanzi.
Katika kikao hicho kilichomalizika hivi
punde,yafuatayo yameamuliwa:
1. Kwa kuwa katibu Mkuu wa Klabu jana aliiagiza
idara ya Mawasiliano na Mahusiano ya Klabu
kulifanyia utafiti suala hili,Bodi imeiongezea idara
hiyo wajumbe wawili ili kuunda kikosi kazi
kitakachofanya kazi kwa adidu za rejea zifuatazo:
(a) Kupitia rejea za mchezo husika na kuangalia
Mazingira na Asili ya suala zima lililojitokeza.
(b) Kupata Maelezo ya awali ya mchezaji wetu
juu ya suala lenyewe.
(c) Kufanya uchambuzi wa kisayansi wa mzizi wa
suala analohusishwa mchezaji kwa kushirikisha
watalaam wa Ushauri Nasihi na Saikolojia kisha
kuishauri Bodi.
2. Kazi hii iwe imekamilika ndani ya masaa 86
kuanzia jana saa saba mchana ilipoanza.
Klabu inaomba umma wa wanamichezo kuwa na
subira.
Wasalaam,
E.E.Kimbe
KATIBU MKUU
MCC FC
Asante kwa kutembelea Hope FM Iringa, Asante kwaku-share habari hii, Kama una Maoni, Ushauri, Story ya ku-share na sisi na au Unahitaji msaada...!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni