Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Yanga wametua mjini
Morogoro, mwenyeji wao naye
amewakaribisha kwa kuwa
yuko tayari kwa kazi ya
kesho Jumatano.
Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar,
Mecky Maxime ambaye wengine
huchanganya na kumuita
Mexime, amesema wako tayari
kwa mechi hiyo ya Jumatano
na Yanga wasitegemee
mteremko.
Yanga wamekuwa na rekodi
mbaya na Morogoro, kwa
misimu miwili sasa wamekuwa
wakipoteza mechi zao kwenye
Uwanja wa Jamhuri dhidi ya
Mtibwa Sugar.
Maxime amesema wao wako
tayari, pia wanataka
kuendeleza ushindi kama
ilivyo kwa Yanga.
Yanga na Mtibwa zote
zimeshinda mechi nne za
mwanzo za Ligi Kuu Bara na
kila moja ina pointi 12.
“Kama ilivyo kwa mechi
nyingine, tumejiandaa
vilivyo. Waache waje tu
wataona,” alisema Maxime
ambaye kikosi chake tokea
kuanza kwa msimu kimekuwa
kikizigonga timu
inazokutana nazo.



Chapisha Maoni