Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Katibu Mkuu wa Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF),
Mwesigwa Selestine leo
amesaini mkataba wa mwaka
mmoja na mfuko wa huduma ya
afya (NHIF) kwa ajili ya
kutoa huduma kwa wachezaji
wa Ligi Kuu pamoja na
viongozi wa benchi la
ufundi.
Hafla ya kusaini mkataba
huo imefanyika katika
hoteli ya Protea Courtyard
iliyopo Upanga jijini Dar
es salaam ambapo katibu
mkuu wa TFF, Mwesigwa
Selestine na Mkurugenzi wa
Masoko na Utafiti wa NHIF
Rehani Athumani walisaini
kwa niaba ya pande hizo
mbili.
Akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa mkutano wa
uwekaji sahihi mkataba huo,
Mwesigwa amesema
anaishukuru NHIF kwa
kudhamini kutoa huduma ya
afya kwa wachezaji na
mabenchi ya ufundi kwa
vilabu vyote 16
vinavyoshiriki Ligi kuu ya
Vodacom.
Aidha, Mwesigwa ameziomba
klabu za Ligi Kuu Bara
kutoa ushirikiano na watoa
huduma ya afya kwa
wachezaji na viongozi
kutoka NHIF pindi
watakapokuwa wanafika
kwenye vilabu vyao kwa
ajili ya shughuli
mbalimbali.
Mkurugenzi wa Masoko na
Utafiti wa NHIF,  Rehani
Athumani akiongea kwa niaba
ya mfuko huo amesema wako
tayari kufanya kazi na
kutoa huduma ya afya kwa
ngazi zote ikiwemo kwa timu
za madaraja ya chini pia.
TFF na NHIF zimeingia
mkataba wa mwaka mmoja wa
udhamini wa huduma ya afya
kwa wachezaji kwa ligi kuu
na viongozi wa benchi la
ufundi, mkataba ambao
unaeza kuongezwa kila
unapomalizika.
TFF kwa kupitia bodi ya
ligi inavitaka klabu zote
za Ligi Kuu zitoe
ushirikiano kwa wafanyakazi
wa NHIF katika kurahisiha
shughuli za usajili ikiwa
ni pamoja na kutoa taarifa
na nyaraka sahihi zikiwemo
picha za wahusika katika
muda sahihi.



Chapisha Maoni