Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Mbeya City imepata sare ya
bao 1-1 dhidi ya wenyeji
wake Toto African katika
mechi iliyopigwa kwenye
Uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza, leo.
Wageni Mbeya City ndiyo
walianza kupata bao katika
dakika ya 12 kupitia John
Kabanda aliyefunga kwa
mkwaju wa penalti. Bao hilo
likadumu hadi kipindi cha
kwanza kfilipoisha.
Kipindi cha pili
kilionekana ni cha Mbeya
City ambao walitawala
zaidi, lakini wakapoteza
nafasi nyingi za kufunga.
Toto waliibuka na kuanza
kusukuma mashambulizi mengi
zaidi kuanzia dakika ya 70
na kuonyesha kuwachanganya
wageni wao.
Edward Christopher
aliipatia Toto bao la
kusawazisha kwa shuti kali
la kushitukiza
lililomshinda kipa mkongwe
Juma Kaseja na kaundika bao
hilo.
Kaseja na Edo, wote
waliwahi kuwa wachezaji wa
Simba kabla ya kila mmoja
kuchujua njia yake.
Mbeya City ilicheza bila ya
nahodha wake ambaye
amefungiwa miaka miwili
baada ya kumdhalilisha
nahodha wa Azam FC, John
Bocco.

RATIBA

Jumamosi Oktoba 3
Mgambo Shooting v Coastal Union
Majimaji FC v Mwadui FC
Toto Africans v JKT Ruvu

Jumapili Oktoba 4
Stand United v Mbeya City
Kagera Sugar v Tanzania Prisons



Chapisha Maoni