Na Sophia Mwaipyana ,Mbeya
Maisha ni safari ndefu ambayo binadamu tunasafiri huku hatujui safari hiyo inaishia wapi
ikiwa imeambatana na mipango mengi
ambayo kila binadamu anatamani ifanikiwe ilikuweza kumwaongezea nguvu ya
safari yake lakini kunawakati tunakutana na vikwazo vingi ambavyo
vinaweza kufanya ukakata tama lakini tunaambiwa kukata tamaa nisawa na
kujiroga mwenyewe.
Bahati
Mwaipopo alikuwa na mipango mingi aliyo
tamani kutimiza kupitia soka lakini alikutana na vikwazo vingi hali
iliyo pelekea lengo lake la kupata kazi kupitia soka kugonga mwamba.
championi
ilifanikiwa kufanya naee mahojiano kuhusu maisha yake ya soka ambapo
aliatufahamisha kuwa alianza kucheza soka toka akiwa darasa la tano
katika shule ya msingi Mbalizi hadi
mwaka 1987 akiwa shule ya sekondari Kipoke aliiwakirisha nyanda za juu kusini katika
mashindano ya Umisenta taifa yaliyo fanyika mkoani Shinyanga .
Timu yake
ya kwanza kuichezea ni timu ya Young
Stars ya Mbalizi mwaka 1989 -1991 na
mwaka 1993 aliichezea timu ya Benki kuu na mwaka 1994 -1996 aliichezea timu ya Ujenzi
Rukwa na mwaka 1997 aliichezea Tukuyu Stars
hadi mwaka 1998 alihamia katika timu ya 44kj iliyokuwa mbalizi ni timu
ya jeshi.
Kwanini
Tukuyu Stars hukudumu
“Kipindi
kile mpira ulikuwa haulipi kama sasa kwahiyo lengo langu kubwa nilikuwa nataka
nipate timu ya jeshi ili nipate kazi na ndiyo maana nikaenda katika timu ya
jeshi lakini bahati mbaya zaidi sikuweza kutimiza ndoto yangu ya kuingia
jeshini kupitia kipaji changu”
Mechi ngumu
kwako
“Ni ile
mechi ya mwaka 1995 Ujenzi na Yanga
mwaka huo Yanga ilikuwa inaitwa Yanga Kampara kwasababu walikuwa
wametoka kuchukua ubingwa Uganda na mechi hiyo tulifungwa goli nne na
mechi ilikuwa ngumu sana kwetu kutokana
na timu hiyo kusheheni wachezaji wazuri”
Tukio gani
ambalo huwa halisahau
“nimatukio
kama mawili hivi huwa siyasahau katika maisha yangu lakwanza ni ile ajari ya basi mwaka 1992 nikiwa naichezea Benki
kuu tulikuwa tunaenda Tabora kucheza
na Polisi Tabora”
“Tulipofika
kijiji kimoja kinaitwa Kasulu dereva alikuwa katika mwendo kasi gafla akaona mtu
mbele sasa ile anataka kumkwepa gari
likahama njia ila namshukuru mungu wachezaji tulipata majeraha tuu hakuna aliye
poteza kiungo wala maisha”
“chakushangaza
hata tulipofika Tabora waligoma kutusogezea mechi kwahiyo tulicheza hivyo hivyo
na tukatoka sale ya goli moja’
‘Pia mwaka
1996 nikiwa ujenzi nakumbuka tulienda
kucheza mechi na timu ya Waziri mkuu Dodoma tulikaa siku nne tukiwa tumeishiwa
pesa yakula hadi pesa ya kuweka mafuta katika gari ili kurudi Rukwa’
“Kwahiyo
wachezaji tukawa hatuna chakula wale wenye uwezo tulikuwa ukimchukua mchezaji mmoja unaenda naye kula
chakula cha mchana jioni tena unaenda
kula na chezaji mwingine”
“Alitokea
msamaria mmoja ambaye ni mkazi wa Sumbawanga akatupa pesa ya kujaza mafuta
ambayo yatatufikisha Mbeya kwahiyo
tulipofika Mbeya mimi nikaisafirisha timu na nikaenda kurudishiwa pesa tulipo
fika Sumbawanga”
Kwanini
ujenzi ilipoteza mwelekeo
“Unajua mkuu
wa mkoa kipindi kile timu inafanya vizuri mkuu wa mkoa alikuwa Chrisanti
Mzindakaya kwahiyo alikuwa anaipa sapoti sana timu pamoja na Padri Msakira
kwani ilikuwa hadi kambi tunaweka
misheni wakati mwingine chini ya usimamizi wa padri”
“kwahiyo
shida ilikuja pale Mzindakaya alipo hamishwa na kuja mkuu wa mkoa mwingine
ambaye alikuwa hapendi michezo kwahiyo shida ilianzia hapo timu ikayumba
mishahara ikawa hakuna tena wachezaji tukaweka mgomo na wakatuambia asiye taka
aondoke mimi na wenzangu kama watatu
tuliondoka”
Ushirikina
katika soka
“Ushirikina
upo sana sema kuna utofauti kila timu
ina utaratibu wake timu nyingine
wanafanya viongozi na nyingine hadi wachezaji mnashirikishwa ,mfano kuna
wakati wachezaji tulikuwa tunaamshwa usiku tunaenda kuchezeshwa mpira makaburini”
‘Nakumbuka kunasiku tulikua tunacheza Iringa katika uwanja wa Samora sikuhiyo mimi nilikuwa
ndiyo kapteni kwahiyo kabla ya mechi wakati wenzetu wanavaa mimi na golikipa
tulitolewa na kupelekwa mto Lwaha ‘
“Tulipo fika
kule nilipewa njiwa nimnyonge njiwa huyo alikuwa amefungwa sanda nyeusi nikamnyonga
alafu nikaambiwa nimtupie katika mto huku nikinuwiza baada ya hapo tukaondoka
kwenda uwanjani”
“Lakini
chaajabu tulipo fika uwanjani mechi
ilikuwa ngumu sana na tulifungwa goli
3-1 kwahiyo ushirikina katika soka upo sana
ila hauna faida yoyote zaidi ya kupoteza mwelekeo wa timu kwasababu mkiamini sana
hiyo imani ndiyo pale mtapoteza mechi nyingi sana”
Kwanini
ushindani kipindi hiki ni mdogo
“Timu zote iliifanye vizuri
lazima iwe na wadhamini kwahiyo tunaona
kwasasa wadhamini wamebaki tu katika timu za dar-es-saalm na ndiyo timu hizo
zinakuwa na ushindani mkubwa kwasababu wachezaji wanapata mahitaji yote kwa
wakati’
“Kwahiyo
hali hii inaziathili sana timu zetu za mikoani ukiangalia zamani timu nyingi
zilikuwa zinawadhamini wake ukiangalia
Mecco ilikuwa chini ya shirika la ujenzi yani timu nyingi zilikuwa na wadhamini
wao hasa mashirika binafsi”
“lakini sahizi
tunaona mabadiriko kwa huyu mdhamini ambaye ameanza kuja hadi mikoani kuwadhamini Mbeya City na Ndanda Fc kwahiyo
wadhamini wajitokeze ilituweze kuongeza ushindani katika ligi yetu ‘
“Zamani timu
nyingi zilikuwa zinachukuwa ubigwa kutokana na hilo lakini kwasasa tunabaki tu
simba Yanga unaona mfano safari hii
mabigwa ni Azam kwanini sababu wanamdhamini wao ambaye ameifanya timu ilete
mabadiriko katika ligi kuu”
Mafanikio
“Kama
nilivyo kwambia zamani mpira ukipata mafanikio makubwa nikupata ajira siyo
vinginevyo zaidi zaidi ni kutembea Nchi nzima na kufahamika”
Mchezaji gani unaempenda hapa Tanzania
“Ni Canavaro
Yule nimchezaji sababu kiwango chake
hakishuki na hana utani akiingia uwanjani hata kama nimechi ya kirafiki, pia ni
mchezaji ambaye anacheza nafasi niliyokuwa nacheza mimi”
Wachezaji
unao wakumbuka ulio cheza nao
“nikiwa
ujenzi ni Atupele Mapungiro na nikiwa 44kj ni sajigwa jamaa alikuwa mvumilivu
sana katika mazoezi na alikuwa na bidii”
Ushauri wako
“Mimi
ushauri wangu ni kwa mashabiki wa Mbeya
tuzipe sapoti timu zote ilizote
ziweze fanya vizuri sasa tukiegamia upande mmoja je siku hiyo timu tunayo itegemea isipo fanya vizuri
itakuwaje, tukumbuke Prisons ndiyo timu toka zamani ilikuwa inatuwakirisha
katika soka”
Familia
“nina
familia ya watoto sita ila kati yao namuona mwanangu Girbet ndiye atarithi kipaji changu kwani nyota
njema huonekana asubuhi “
Maisha ya
sasa
“Sahizi ni
mjasiriamari napia naichezea timu ya maveterani ya Mbalizi na ninaishi
huko katika mji mdogo wa Mbalizi,na
sitegemei kuacha kabisa kucheza soka kwasababu
napenda niupe mwili wangu mazoezi”
Mwisho.
Chapisha Maoni