Uongozi
wa klabu ya Yanga umesema utapinga maamuzi ya kamati ya Sheria na Hadhi
ya Wachezaji kuhusiana na maamuzi yake ya kumtangaza mchezaji wake,
Emmanuel Okwi kuwa huru.
Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ya Yanga, Sam Mapande
amesema kuwa hawajaridhishwa na maamuzi hayo ambayo yanakinzana na
shitaka zima la mchezaji huyo.
Mapande amesema
kuwa kamati ya TFF imeamua sakata la Okwi kinyume na malalamiko yao
kwani hakukuwa na lalamiko la mchezaji huyo wa Uganda kuhusiana na
malipo ya fedha zake za usajili.
Alisema kuwa cha
kushangaza, kamati hiyo ya TFF iliamua kusikiliza kesi ambayo haikuwa
mbele yao na kutoa maamuzi ambayo hata wao wameshangazwa nayo.
“Kwanza
kesi yenyewe ilikuwa haijamalizika, walituambia tuwasilishe vielelezo
kuhusiana na kitendo cha mchezaji huyo kufanya mazungumzo na klabu ya
Misri, lakini cha kushangaza maamuzi yametolewa, hili limetushangaza
sana,” alisema Mapande.
Alisema kuwa mazingira
yalikuwa yameandaliwa kuibeba Simba na Okwi kwani hata malalamiko yao
kwa Simba hayakusikilizwa. “Malalamiko yetu yalikuwa wazi kabisa, yapo
kimaandishi, hatukuwai kulalamikiwa, suala la fedha za usajili la Okwi
limetoka wapi, kama lilikuwepo, mbona hatujajulishwa kimaandishi kama
utaratibu ulivyo,” alisema.
Alisema kuwa Kamati
hiyo kumruhusu mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Zacharia Hans Pope ambaye
pia ni mwenyekiti wakamati ya usajili ya Simba kuwemo katika kikao
hicho kinyume na taratibu za Fifa kupitia kifungu namba 19 kinachoeleza
mgongano wa kimaslah
Chapisha Maoni