Na Alex Mapunda,Iringa
TATIZO la uhaba wa viwanja limejidhiirisha wazi
mkoani Iringa baada ya hivi karibuni mechi kati ya lugalo FC pamoja na Jako FC kusimamishwa ili kupisha timu
inayohaminika ina uhuru wa kutumia uwanja huo kutumia.
Mechi hiyo ambayo ilifanyika
katika shule ya msingi Umoja ilivunjika mwazoni mwa kipindi cha pili ili
kupisha timu nyingine ambapo hadi muda huo Lugalo ilikuwa mbele kwa bao 2-0
dhidi ya jako Fc.
Baada ya kumalizika mchezo
huo kocha wa Jako Fc Joshua michelle
alisikitika sana kuhusu kitendo hicho na kuitaka manispaa kutenga maeneo zaidi
ya viwanja ili kukunza na kundeleza michezo mkoani Iringa.
“nimeskitika sana tumekuja na
mashabiki wetu,lakini tunaondoka bila mpira kumalizika,Sijui kwa nini,Tanzania
tuna maeneo ya kutosha lakini tunashindwa kuwa na viwanja vya kutosha vya michezo.
Pia moja ya shabiki ambaye
aliudhuria kwenye mtanange huo Chris Tomas alisema kuwa mpira wa Tanzania tutachelewa kuufikisha kule
ambapo wezetu wapo kwa kuwa bado kutatua vitu vidogo vidogo tunatushindwa.
Mara nyingiImezoeleka mpira wa miguu m unaweza kuvunjika ukitokea
ugomvi baada ya timu husika kukwaruzana,timu kugomea mchezo au mwamuzi
kuvurunda katika mchezo husika na si kwa sababu ya kupisha timu nyingine
icheze.
Chapisha Maoni