Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Wendesha baisikeli wapiga vita kisukari


Hakuna mwanariadha anae kubali udhaifu haswa wakiwa wamehusishwa katika michezo migumu duniani.
Lakini timu moja ya wataalamu wa kupeleka baiskeli wamegeuza ugonjwa huo sugu kuwa njia dhabiti ya kuwafanya wafanikiwe.
Mkurugenzi mkuu ambae pia ni Mwanzilishi wa timu ya Novo Nordisk Phil Southerland,alipatikana na ugonjwa wa kisukari aina ya kwanza wakati alipokuwa miezi saba .
Madaktari waliwaambia wazazi wake kuwa kuna uwezo mkubwa wa mtoto wao kuwa kipofu ama apoteze maisha yake katika umri wa miaka 25.
Vile vile ,Phil alipewa tahadhari ya kutojihusisha na michezo lakini katika umri mdogo aliokuwa nao alipenda sana kuendesha baiskeli na hivyo basi kuchangia pakubwa katika maisha yake.
Phil mwenye miaka 32 anasema kuwa ”niligundua kuwa mazoezi yalinisaidia sana kudhibiti ugonjwa wa kisukari” . Wakati alianza kushinda mashindano , aliweza kumhamasisha rafiki yake aliyekuwa na ugonjwa wa kisukari kujiunga na riadha hiyo ya kupeleka baiskeli ili aweze kudhibitI viwango vya damu mwilini mwake.
Phil amejitolea kusaidia wengi walio na hali hiyo,alijaribu sana kupata mtu mwenye ugonjwa huo ili aweze kushindana nae.
“wakati watu wamepatikana na dalili za ugonjwa wa kisukari ,madaktari husema kuwa „kazi yako imekwisha” ama “huwezi fanya jambo lolote ukiwa na ugonjwa wa kisukari.”
Kwa kawaida huwa hawana nia mbaya wakisema hivyo,ni kwa vile wanataka wagonjwa kuishi kwa uangalifu mkubwa,na kwa miaka mingi wengi wameamini na kukata tamaa maishani.
Phil anasema kwamba anataka kila daktari kujua kuwa watu wenye ugonjwa wa kisukari aina ya kwanza,wanaweza kufanya jambo lolote wakisimamiwa vyema.
Ugonjwa wa kisukari aina ya 'Type 1' hutokea pale mwili unaposhindwa kutoa insulini ambayo ni homoni inayosaidia mwili kutumia sukari iliyo ndani ya damu kuupa mwili nguvu inayohitajika kwa binadamu kuishi.
'Bila insulini'
Mgonjwa wa kisukari hulazimika kujimipa kiwango cha insulini mwilini
Kiwango cha sukari huongezeka kwenye damu na kuufanya mwili kudhoofika kwa kukosa nguvu. Badala yake mwili hujaribu kupata nguvu kutoka kwa protini na mafuta yaliyo mwilini, hali ambayo husababisha mwili kupoteza uzani na matatizo mengineyo.
Inakisiwa asilimia kumi (10%) ya watu wazimu wanaugua ugonjwa huu wa kisukari aina ya type 1. Maradhi haya hutibiwa kwa kujidunga sindano yenye insulini, kula chakula bora na kufanya mazoezi kila mara.
Hata hivyo, waendeshaji baiskeli wa kulipwa wanaotumia muda wao mwingi mashindanoni kama vile mashindano ya Tour of Britain, hupata ugumu kudhibiti ugonjwa huu.
Bwana Southerland anaelezea ya kwamba timu yake hukagua kiwago cha sukari mwilini ya uendeshaji baiskeli wote kila baada ya dakika 15 kabla ya kuanza mashindano. Aliongeza ya kwamba huwa wanakagua chakula wanachokila lakini baada ya mashindano kuanza, ni wajibu wa washindani kujitunza.
Waendeshaji baiskeli huweza kujua kiwango cha sukari katika miili yao kwa kutumia kifaa kidogo cha kielektroniki wanachobeba mifukoni kilicho na uwezo wa kupima kiwango wa sukari mwilini.
Kulingana na bwana Phil, kila mwendesha baiskeli hutumia njia tofauti kudhibiti maradhi haya lakini akasisitiza kwamba wote hubeba sindano za insulini zinazoweza kutumiwa kujidunga mwilini ili kupunguza kiwango cha sukari mwilini, hivyo basi mwili unapata nguvu.
 
“Baadhi yao hula chakula kila mara bila kujidunga sindano yenye insulini ilhali wengine hujidunga sindano mara tatu (3) au nne (4) wakati wa mashindano,’’ Phil alifafanua.
'Mipango mikubwa'
Baadhi ya wagonjwa wa Kisukari hujidunga sindano ya Insulini mwiliniaidha mara tatu au nne kwa siku
Kuishi kama mwanariadha mwenye kisukari ni ngumu.
Kwa miaka mingi, kampuni ya kutengeneza dawa ya Novo Nordisk iliyo uholanzi imekuwa ikihusika katika utengenezaji wa aina tofauti za insulini .
Juhudi za kampuni hii zimehusisha pia kuwaelimisha na kuwatia moyo watu wenye ugonjwa huu wa kisukari.

BY BBC


Chapisha Maoni