Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Na Alex Mapunda,Iringa

FAINALI ya michuano ya kiwanda cha chai wilayani Mfindi, Unliver Tea Cup ambayo ilipangwa kufanyika wikendi hii  imepigwa kalenda hadi itakapo tangazwa tenda baadhi ya sababu ni maandalizi ya mtanange  wa fainali bado hayajakamirika ikiwemo zawadi kwa washindi bado haifahamiki itakuwaje.


Katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu Timu  ya Rugoda Fastoli iliibuka kidedea baada ya kuifumua bila huruma  Kilima Estate kwa jumla ya bao 6-1 mchezo ambao ulikuwa wa upande mmoja.

Timu ambazo zitaonyesha umwamba katika mchezo wa Finali ni engeeny Fc dhidi ya Rugoda Fastoli Fainali ambayo inatarajia kuwa na upinzani wa hali ya juu kuokana na uwezo mkubwa wa timu hizo ambapo katika mchezo ambao walikutana  hatua za mwanzo timu hizo zilitoshana nguvu ya bila kufungana.

Michuano hiyo iliyoanza kutimua vumbi Tkribani wiki tatu zilizopita imeibua vipaji vingi vya soka kwa kuwa vijana wengi walipata nafsi ya kuonyesha uwezo wao na kama itafanyika mara kwa mara, mkoa wa Iringa utajitoshereza na hazina kubwa ya wachezaji waliopo hapa ambao bado hawajapewa nafsi ya kucheza.



Chapisha Maoni