Manchester
United al maarufu mashetani wekundu jana ilikwea hadi nafasi ya tatu ya
msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kuwaadhibu wapinzani wao
Southampton kwa jumla ya magoli 2 - 1 katika mechi iliyopigwa kwenye
uwanja wa St. Marys
Kinara wa Manchester United hapo jana alikuwa
ni Robin Van Persie ambaye ndiye aliyefunga magoli yote mawili kwa
upande manchester United.Kwa matokeo hayo sasa Manchester inapanda hadi nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi hiyo na kuwashusha Southampton hadi nafasi ya tano.
Msimamo ulivyo kwa sasa Chelsea wapo nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi hiyo, Manchester City ya Pili na Manchester United wapo nafasi ya tatu.
Chapisha Maoni