Michuano ya Taifa ya mpira wa miguu
kwa wanawake ya Proin Women Taifa Cup inaanza rasmi Desemba 28 mwaka huu kwa
mechi ya ufunguzi kati ya timu za mikoa ya Mara na Mwanza itakayochezwa Uwanja
wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Kombaini za mpira wa miguu za mikoa
yote ya Tanzania Bara zitashiriki mashindano hayo yatakayochezwa kwa raundi
mbili mwanzoni, na baadaye hatua ya robo fainali hadi fainali.
Mashindano hayo yanayodhaminiwa na
kampuni ya Proin Promotions Limited, kuanzia hatua ya robo fainali, mechi zote
zitafanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja Biashara wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania, Peter Simon Shankunkuli aliishukuru kampuni ya Proin
ambao ni watengenezaji, wazalishaji na wasambazaji wa filamu za kitanzania kwa
kuwezesha mashindano hayo kufanyika kwa mara ya kwanza.
Proin Promotions imekua wakivumbua
vipaji mbalimbali vya uigizaji na sasa imeamua kujikita katika mpira wa miguu
ili kuweza kuvumbua vipaji kwa wachezaji wa kike.
Shankunkuli alisema nafasi bado zipo
kwa wadhamini watakaoguswa na mashindano hayo, kwa kuwasiliana na TFF au Proin
Promotions Limited kwa maelezo zaidi
Chapisha Maoni