Tottenham
wanafanya mipango ya kuwapata kiungo Morgan Schneiderlin,25 pamoja na
mshambuliaji Jay Rodriguez, 25,wote toka klabu ya Southampton na beki wa
Raul Albiol, 29,wa Napol ya Itali ili kuimarisha kikosi chao.
Kocha wa Sunderland Gus Poyet bado anamuhitaji mshambuliaji Fabio Borini, 23, aliekosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Liverpool.
Bosi wa Newcastle Alan Pardew anataka kumsajili kwa mkopo kipa Mark Schwarzer, kutoka chelsea ambae ni chaguo la tatu kwa kocha Jose mourinho.
Harry Redknapp kocha wa QPR ana imani atamsajili kwa mkopo mshambuliaji Robbie Keane, 34, nyota wa zamani wa Tottenham anayechezea timu ya LA Galaxy ya Marekani.
BY BBC
Chapisha Maoni