Mwanariadha nyota
duniani, Usain Bolt amekubali kumsamehe mwandishi wa habari aliyemgonga na wote
wakaanguka.
Mwandishi huyo alimgonga
Bolt na kumwangusha wakati akishangilia mara tu baada ya kushinda mita 200
katika mashindano ya IAAF kwenye Uwanja wa Bird Nest jijini Beijing, China.
Bolt alikuwa
anashangilia, mwandishi huyo alikuwa akimchukua kwa nyuma yake, ghafla akashindwa
kukithibiti chombo cha Sagway alichokuwa amepanda, kikamchota Bolt, wote
wakaanguka.
Lakini mwandishi huyo
alitoa mkufu na kumpa Bolt akionyesha kumuomba msamaha kwa kilichotokea wakati
yeye akichukua picha za TV.
Bolt naye kiroho safi
kabisa akakubali zawadi hiyo na kumueleza alishamsamehe.
Chapisha Maoni