KIUNGO aliyewai kuwika na Yanga pamoja na timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boyz, Nurdin Bakari,Amejiunga na Lipuli ya Iringa timu inayoshiriki ligi Daraja la kwanza.
Akizungumzia suala hilo,
Katibu msaidizi wa Lipuli Ronjino Malambo amesema wamemsajili Bakari ili kuongeza
nguvu katika kikosi chao.
Malambo alisema baadhi ya wachezaji wengine wenye majina ambao wamesajiliwa na timu hiyo ni pamoja na Danny Mrwanda,Meshack Haberi,Yona Ndabila pamoja na Lulanga Mapunda.
Bakari ambaye aliigharimu Serengeti Boyz kwa tatizo na Umri pia Aliwahi kupigwa chini na Simba kutokana na kudaiwa kuwa na tatizo la moyo, lakini alipotua Yanga akaonyesha kiwango safi na hakuwahi kupata matatizo ya moyo uwanjani.
Chapisha Maoni