BAADA ya kushinda Kura zilizopigwa
na Wanahabari toka Nchi 54 Wanachama wa UEFA,Messi ametawazwa kuwa mchezaji bora wa UEFA.
DONDOO MUHIMU KWA WACHEZAJI HAO TATU
BORA:
Cristiano Ronaldo (Portugal – Real
Madrid)
-Ndie Mfungaji Bora wa La Liga
Msimu uliopita kwa kupachika Mabao 48 na pia kufungana na Messi na Neymar
katika Ufungaji Bora wa UEFA CHAMPIONS LIGI.
-Alipachika Jumla ya Mabao 61
katika Mashindano yote akiwa na Real Madrid na hivyo kumpita Lejendari Alfredo
Di Stéfano na kushika Nafasi ya Pili ya Ufiungaji Bora katika Historia ya Real.
-Alipiga Bao 5 katika Mechi
moja hapo Aprili 5 Real ilipoibonda Granada Bao 9-1.
-Alimaliza Msimu kwa kupiga
Hetitriki 3 mfululizo dhidi ya Espanyol, Getafe na Armenia.
Lionel Messi (Argentina – Barcelona)
-Alivunja Rekodi ya Telmo Zarra
ya Bao 251 za La Liga na pia kuifungia Barcelona Mabao 58 katika Mashindano
yote na kuiwezesha kutwaa Trebo, yaani kutwaa Ubingwa wa La Liga, Copa del Rey
na UEFA CHAMPIONZ LIGI.
-Kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI
alifunga Bao 10 na kufungana na Ronaldo na Neymar kama Wafungaji Bora wa
2014/15.
-Amefungana na Ronaldo wakiwa
na Mabao 77 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na ana Mabao 80 katika Mashindano yote ya
Klabu ya UEFA yakiwemo Mawili aliyofunga kwenye UEFA Super Cup Jumatatu Usiku
dhidi ya Sevilla.
Luis Suárez (Uruguay – Barcelona)
-Alifunga Bao 2 katika Raundi
ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI walipoibwaga Manchester City.
-Ni mmoja wa Mastraika Watatu
wa Barcelona waliopiga Jumla ya Mabao 122 Msimu uliopita pamoja na Neymar na
Messi.
Chapisha Maoni