LUNDENGA |
Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni
waendeshaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga, ametangaza kujiuzulu
nafasi yake ya mwenyekiti katika kamati ya kuandaa shindano hilo na badala yake
ameacha nafasi hiyo kwa wadau wengine.
Lundenga alitangaza uamuzi huo jana na kudai kuwa
amefikia uamuzi huo baada ya kuitumikia nafasi hiyo kwa miaka mingi lakini
ataendelea kutoa ushirikiano katika kamati mpya ya shindano hilo.
Uongozi mpya uliotangazwa jana unasomeka hivi:
Juma Pinto (mwenyekiti), Lucas Rutta (makamu mwenyekiti), Doris Mollel (katibu
mkuu), Jokate Mwegelo (msemaji wa kamati), pamoja na wajumbe 8 ambao ni Hoyce
Temu, Mohammed Bawazir, Gladyz Shayo, Magdalena Munisi, Shah Ramadhani, Hamm
Hashim, Khalfani Saleh na Ojambi Masaburi.
Hivi
karibuni Barala la Sanaa la Taifa (Basata) liliifungia Miss Tanzania
kwa miaka miwili, hata ilitumikiaa dhabu hiyo kwa miezi nane kabla ya
kufunguliwa.
BY SALEH
Chapisha Maoni