HATIMATE kimeeleweka,Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeiagiza
Etoile du Sahel kulipa kitita cha dola 300,000 (Sh milioni 480) pamoja na fidia ya usumbufu [faini].
Fifa imeitaka klabu hiyo ya Sousse nchini Tunisia
kuhakikisha inalipa fedha hizo ndani ya mwezi mmoja pamoja na faini ya dola 28.
Hatua hiyo imekuja baada ya Simba kushinda kesi
iliyotokana na Simba kushitaki kwa Fifa baada ya Etoile kushindwa kulipa fedha
za malipo ya kumnunua Emmanuel Okwi.
Rage aliahidi Etoile wangelipa wakati akiwa
madarakani, kabla hajaondoka, lakini haikuwa hivyo.
Zigo likamuangukia yeye kwa kuwa ndiye aliidhinisha
Okwi kwenda Etoile hata kabla ya Waarabu hao kulipa, kabla ya kumgeuka.
Etoile walizidi kusumbua baada ya Okwi kurejea
Uganda na baadaye Yanga, hali iliyofanya Simba kukata tama.
Taarifa zinaeleza barua ya agizo hilo, tayari
imetua TFF ambayo imewasilisha kwa Rais wa Simba, Evans Aveva kwamba anatakiwa
kupokea mzigo pamoja na faini hiyo ndani ya mwezi mmoja.
Chapisha Maoni