Na Alex Mapunda,Iringa
TIMU
ya soka ya Kurugenzi ya mafinga Mkoani Iringa
imesajili wachezaji wapya watano ili kuimalisha kikosi hicho ikiwa ni
mandalizi ya ligi daraja la kwanza raundi ya pili ambayo inatarajia kutimua
vumbi hivi karibuni.
Moja
ya wachezaji ambao kurugenzi imewasajili ni pamoja na mchezaji Abdul Ngedeke
toka nchini Nigeria ambaye timu hiyo ilishindwa kumsajili roundi ya kwanza na
amekuja kuimalisha safu ya ushambuliaji wa timu hiyo ambayo roundi ya kwanza
ilionekana kuwa butu.
Wachezaji
wengine waliosajiliwa na timu hiyo ni pamoja na kipa Jafari Salum[Toka Kimondo],Miraji Miraji mchezaji
huru,Kiungo Omari Hamis pamoja na Akadene Yawa toka katika shule ya michezo ya
Silvester Mashi [mwanza]
Akifafanua
kuhusu maandalizi ya timu Hiyo Meneja wa
Kurugenzi Athumani Kahamia amesema kuwa lengo kubwa la Kurugenzi ni kupeperusha
vyema bendera ya wakazi wa mafinga na
Iringa kwa ujumla na kuhakikisha timu za ligi kuu kwa nyanda za juu kusini
zinazidi kuongezeka.
“mashabiki
na wadau waendelee kuiunga mkono kurugenzi,kutokana na maandalizi ambayo tunaedelea
kufanya mimi naamini raundi ya pili timu itafanya vizuri kuliko roundi ya
kwanza”alisema Kahamia.
Katika
kundi A ligi daraja la kwanza timu ya
kurugenzi inashika nafsi ya 7 na kufikisha pointi 13 baada ya kucheza mechi 11
ambapo timu hiyo inaitaji kushinda mechi za mzunguko wa pili ili kujihakikishia
nafsi ya kucheza ligi kuu ya Vodacom mwakani.
Chapisha Maoni