Na Alex
Mapunda
WANACHAMA wa tawi la Simba mkoani Iringa wanatarajia kukutana januari mwakani ili kujadili
mwenendo wa timu yao ambayo imeanza kwa kuchechea katika ligi kuu ya Vodacom
msimu huu.
Katibu wa
tawi la wekundu wa msimbazi [simba] tawi la Iringa, bwana John alisema lengo
kubwa la kikao hicho ni kujadili masuala yote kuhusu timu ya simba ikiwemo
mwenendo wa simba katika ligi kuu ya Vodacom toka msimu uliopita ambapo timu
hiyo haijafanya vizuri.
“kwanza nimefurahishwa
na ushindi tulioupata katika pambano la nani Mtani Jembe,timu yetu ilicheza kwa
kiwango cha hali ya juu na wachezaji wengi walionekana kucheza vizuri kuanzia kwa
mlinda mlango hadi washambuliaji “
“lakini kikubwa
ili kujenga timu ya simba viongozi,mashabiki pamoja na wachezaji lazima kila kundi lifanye kazi yake
ipasavyo kwa maendeleo ya Simba,sisi wanachama tunaumia sana pindi timu yetu inapofanya
vibaya wakati uwezo wa kuijenga tunao,na tumiamua kukutana ili kujadili kuhusu timu
yetu na vitu gani vifanyike kwa manufaa ya simba” alisema katibu wa tawi la
Simba mkoa wa Iringa.
Timu ya Simba msimu uliopita ilimaliza ligi kwa kushika
nafsi ya nne suala ambalo lililalamikiwa sana na wadau pamoja na mashabiki wa timu
hiyo lakini pia msimu huu katika mechi saba ambazo simba imecheza imeshinda mechi
moja huku ikitoka sare mara 6 na inashika nafasi ya 7 katika msimamo wa ligi kuu
ya Vodacom ambayo imesimama kwa muda.
Chapisha Maoni