Na Alex Mapunda,Iringa
MUSA OMARI ANASHIKIRIA MKANDA WA TAIFA
BONDIA
maarufu toka songea musa Omari [ Chetepete] Jumapili hii ataonyeshana umwamba
na Twaha Kiduku katika pambano la utangulizi la Roundi 6 kilo 64 ambapo litapigwa katika
ukumbi wa Friends Conner Jijini Dar es salam.
Siku
hiyo ambayo inasubiliwa kwa hamu na wapenzi wa ngumi hapa nchini,pambano kali
litakuwa kati ya Cosmas Cheka ambaye Atapepetana na Ramadhani Shauri huku
mapambano mengine ya utangulizi ni kati ya Juma fundi atavaana na Goodluck
Mrema,Kudra Tamimu atakumbana na Teacher Alon,Kyc Amal uso kwa uso na Bakari
Dunda kisha Chidi Mchina atadundana na Said Torres.
Akizungumza
na Sports JELAMBA VIWANJANI Bondia musa Omari toka Songea alisema maandalizi
kuelekea katika pambano hilo yanaendelea vizuri na akawataka wapenzi na wadau
wa ngumi hapa nchini kujitokeza kwa wingi siku ya jumapili ili kwenda
kumshuudia akionyesha uwezo wake wa ngumi hapa nchini.
“Mimi
siongei sana na simwogopi bondia yoyote hapa nchini ndio maana hata Miyeyusho
ananiogopa, kikubwa ni uwanjani nakumbuka pambano langu la mwisho ambapo nilimpiga
bondia toka Malawi alikuja kwa kelele sana lakini kama sio mwamuzi angefia
ulingoni watu waje kwa wingi katika pambano hilo”alisema musa omari kwa
kujiamini.
|
musa omari |
Hawali
Musa omari alitakiwa kukipiga na Kosmas cheka pambano ambalo lilipagwa kufanyika
Songea lakini limesogezwa hadi mwenzi wa pili baada ya Kosmas kupangiwa pambano
lingine.
Asante kwa kutembelea Hope FM Iringa, Asante kwaku-share habari hii, Kama una Maoni, Ushauri, Story ya ku-share na sisi na au Unahitaji msaada...!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Chapisha Maoni