Ukiikumbuka Maji Maji ambayo ilikuwa
inatikisa hapa nchini Miaka ya 1980 hadi 1990 uwezi kumweka kando John Kabisama
ambaye alikuwa ni miongoni mwa viungo washambuliaji bora kuwai tokea katika
timu Hiyo na Tanzania kwa ujumla.
Kabisama,mzaliwa wa Mbambabei
Wilayani Nyasa alianza kusakata kabumbu katika Shule ya msingi Maji Maji zamani
hikifahamika kama ‘Haideli’Songea Mjini.Amezungumza na Gazeti hili na kueleza
mengi kuhusu Soka:
“Nilianza Kucheza soka la ushindani
nikiwa na RTC ya Arusha mwaka 1977 ambayo ilikuwa ikishiriki ligi daraja ya
kwanza na nikiwa na timu hiyo nilipata bahati ya kuitwa kwenye timu ya taifa
kutokana na umahili wangu wa uwanjani kwa mara ya kwanza na ya mwisho.
“Lakini mwaka 1978 nilijiunga na
Kill Tex ya Arusha timu ambayo nilidumu nayo kwa misimu miwili ambapo baadae
mwaka 1983 nikatimukia AICC pia ya arusha,timu ambayo niliichezea kwa mafanikio
makubwa.
‘Mwaka 1885 Maji Maji ya Songea
wakanichuka Toka AICC[timu ya ukumbi wa mikutano Arusha] kutokana na kiwango
changu kuwa kikubwa sana nikiwa kama kiungo mshambuliaji ambapo kwa iliyewai
kuniona nikicheza anavifahamu vitu vyangu, Maji Maji niliichezea kwa kwa
mafanikio makubwa sana ambapo nikiwa na timu hiyo tulifanikiwa kuiwakilisha
nchi katika mashindano ya kimataifa mara mbili mfululizo,mwaka 1885,1986.
“Na mwaka 1989 baada ya kuona kuwa
soka nimeshalitendea haki na kucheza kwa muda mrefu nikaamua kugeukia shughuli
za kawaida,anasema Kabisama kisha anaendelea:
Ajira kikwazo timu kubwa.
“Wakati nipo RTC ya Arusha
Yanga na Pan Afrika walinichukua lakini tulishindana kuhusu ajira wao
walitaka nicheze mpira peke yake ingawa uwezo wa kunipa ajira walikuwa nao.
“Na kipindi kile kwa kuwa hapakuwa
na ajira ya moja kwa moja katika timu tulikuwa tunategemea ajira ambayo timu
inakutafutia hivyo mimi sikuwa tayari kujiunga na timu ambayo haikuwa tayari
kunipa ajira nikaamua kurudi RTC ya Arusha.
Kutokea kwa kona za Maji Maji.
“ Mwaka 1987 Maji Maji tulienda
nchini Zimbabwe kupambana na Power Diynamo katika Roundi ya kwanza ya Club
Bingwa Afrika,nakumbuka mechi ile ilikuwa ngumu sana kwetu kwani tulifungwa bao
5-1 na bao letu lilifungwa na Abdullah Chuma.
“Mechi ya marudiano tulitakiwa
kwenda Jijini mwanza ili kupambana na wapizani wetu,tulijiandaa vizuri ili
kulipiza kisasi cha bao 5,lakini kilichitokea tulipata ajari mbaya sana wakati
wa safari nyuma kidogo kabla ya kufika Madaba Toka Songea mjini,eneo ambalo
lina kona nyingi sana ambapo kutokana na ajari ile eneo hilo hadi leo linaitwa
kona za Maji Maji.
“chanzo cha ajari ile ni kwamba bosi
wa basi ambalo tulitakiwa kwenda nalo mwanza alikorofishana na Dereva wake
akaamua kuendesha mwenyewe,na kwa kuwa yeye alikuwa mgeni wa Bara Bara ya
Songea hakuzifahamu zile kona hivyo baada ya kuzipita kona kadhaa alifikiria
zemeisha ,kufumba na kufumbua tukajikuta tupo nje ya Bara Bara.
“Katika ajari ile wote Tulipona ila
mimi nilikatika karibia nusu ya ulimi pamoja na maeneo ya miguu nilijisikia
maumivu makali sana,lakini mtu ambaye aliumia sana nakumbuka ni Mweshimiwa Joel
Bendera mkuu wa mkoa wa morogoro ambaye alikuwa mwalimu wetu lakini mungu
alimsaidia baada ya wiki mbili akapata nafuu.
“Tukashindwa kwenda mwanza wenzetu
wakapata ushindi wa mezani licha ya sisi tulipata ajari,maamzi yale mimi
binafsi yaliniuma sana kwa kuwa nilikuwa na hasira sana na wale jamaa toka
Zimbabwe.
Hawezi kusahau
“mwaka 1979 tulicheza mechi ya
kirafiki kati ya RTC na Yanga katika mechi ile nilipigwa kichwa cha makusudi
hadi kuzimia na mchezaji wa Yanga Hamad Omari akitokea nyuma yangu na baada ya
tukio hilo yanga wakamtoa nje na kumwingiza mchezaji mwingine.
“Tatizo ni kwamba tulipishana maneno
ya kimpira na mimi milikuwa mwiba mkali kwa timu yake na yeye pia na hadi
mwisho wa mchezo tulifungwa bao 1-0,kwa tukio lile siwezi kumsahau kwa kuwa
ilikuwa makusudi.
Ushirikina Michezoni.
“Mwaka 1985 kulikuwa na pambano kali
kati ya maji maji na Pan Afrika pambano ambalo ilitakiwa lichezwe siku ya
Jumamosi lakini pan walichelewa kufika uwanjani kwa sababu ambazo hazikuwekwa
wazi na pambano likahailishwa adi siku ya Jumatatu.
“Kipindi hicho Maji Maji alikuwa
imemuleta mzee wa kamati ya ufundi Toka Kigoma ambaye alikuwa anahakikisha
kamati ya ufundi nje ya uwanja inakwenda sawa.
“Yule Mzee tulimpa jina la Mzee
Mziba jina la mchezaji maarufu kutokea kigoma,kwa kweli mimi nilikuwa siamini
imani hizo lakini yule mzee nilimweshimu sana,nakumbuka alituambia kuwa kwa
kuwa mechi yenu na Pan itachezwa siku ya Jumatatu mtashinda bao 3-0,na hata
kama mkipata nafasi nyingine ya kufunga bao haitawezekana.
“kwa kipindi kile Pan Afrika
likikuwa Tishio Mimi sikuafiki kama tungeweza kupata ushindi mkubwa kiasi kile
lakini sisi tulikuja kuamini mara baada ya kumalizika ule mpambano ambapo
tulishinda bao 3-0 kama alivyotuambia yule mzee.
“Mzee Mziba alikuwa akieshimika sana
na Maji Maji alikuwa akisafiri na Timu kila ilikoenda kucheza na kila ambacho
alikisema ndicho ambacho kilikuwa kinatokea kwa hali ile yule Mzee alipata
umaarufu mkubwa sana.
“Hakuishia hapo Maji Maji ilisafiri
kwenda dar kukiputa na wekundu wa Msimbazi Simba mwaka 1985 mchezo wa ligi kuu
ambapo tuliweka kambi yetu katika chuo cha usafirishaji cha Mabibo Dar,baada ya
Chakula cha jioni Mzee Mziba alitutembelea katika kambi yetu na akatukuta tupo
katika hali ya uzuni sana akatuuliza kwanini mpo katika hali hiyo?.
“Tukamwambia tunaofu juu ya mchezo
wa kesho,Mzee Mziba alicheka sana na kwa maneno ya Dharau hakatuambia mchezo wa
kesho ni raisi na msiwe na wasi wasi tutashinda mechi ngumu tayari
tumeshacheza,tukaenda kulala.
“Uwezi kuamini Siku ya mechi
tulicheza mchezo mzuri Sana kama alivyosema yule mzee Simba walikuwa wakitafuta
mpira kwa tochi na hadi dakika 90 za mchezo ulipomalizika Tuliivurumisha Simba
bao 2-1,mabao ya Maji Maji yaliwekwa kimiani na Selestine Sikinde pamoja na
madaraka Suleman kisha lile ya kufutia machozi la Simba nakumbuka lilifungwa na
Zamoyoni Mogela.
“Lakini Mzee Mziba aliendelea
kuimalisha ufundi nje ya uwanja ambapo tulikuwa tumebakisha mechi 8 ili ligi
imalizike na mechi nyingi zilibaki kanda ya ziwa,Mzee wetu akatuambia msiwe na
wasi wasi ila kati ya mechi 8 zilizobakia mtafungwa mechi moja tu ila sijui
mechi gani.
“kweli baada ya maneno yale mechi
ambayo ilifuata tulipambana na CDA ya Dodomo mechi ambayo tulifungwa bao 1-0,na
kuanzia hapo hatukufungwa tena mechi nyingine hadi tukamaliza ligi,hapo
nikakumbuka maneno ya yule mzee na kuamini uwezo wake.
“Baada ya msimu Kumalizika nakumbuka
yule Mzee alituaga na akatuaambia ameitwa uarabuni kwaajiri ya kwenda kutoa
tiba,ambapo toka alipoondoka yule mzee hakutokea tena mwingine kama yule,na
mimi imani ya kuamini mpira nje ya uwanja ikatoweka.
FC Leopald walitulinganisha na timu
ya shule.
“Mwaka 1986 katika michuano ya Club
Bingwa Afrika tulipambana na Fc Leopald ya Kenya ambapo wezetu wakenya
walitudharau sana adi walidiliki kukifananisha kikosi chetu na timu ya shule na
kuhaidi watatufunga zaidi ya bao 6,
“Nakumbua katika mchezo huo
nilicheza vizuri sana na baada ya mechi niliandikwa sana na vyombo vya habari
vya Kenya kutokana na shughuli ambayo niliwaonyesha siku ile ingawa wakenya
walitufunga bao 1-0, na ilikuwa kinyume na matarajio yao.
“Na mchezo wa marudiano mchezo
ambao ulichezwa Mjini Arusha FC leopald walitubamiza tena bao 1-0 na
wakafanikiwa kusonga mbele.
Waamuzi
“Ni wavivu sana kubadilika,zamani
waamuzi walikuwa wanafanya vizuri licha ya techinologia kuwa chini,lakini siku
izi wanaweza kujifunza toka nje kupitia Tv pamoja na mitandao.
Mchezaji anayemhusudu
“Mcheaji ambaye namkubari sana kwa
hawa wanaocheza sasa hivi hapa Tanzania na anaitendea haki nafsi ya kiungo
ambayo nilikuwa nacheza ni mchezaji tegemeo wa Azam Fc Abul Bakari [Sure Boy]
,Mora amjali zaidi.
Timu ya Maji maji.
“Timu imepoteza mwelekeo kwa
asilimia kubwa kutokana na kuyumba kiuchumi pamoja na kukuwa na viongozi wenye
mtanzamo chanya tofauti na kipindi kile sisi tunacheza pia wanachama
waepukane na dhana potofu ya kuutegema mkoa kwa ajiri ya kuendisha Timu.
“Nakumbuka mwaka 2010 Maji Maji
ilipata mdhaamini lakini aliingia mitini kwa sababu ya matumizi hasi ya pesa
zake ndani ya timu,hebu tujaribu kuwa wabunifu na kutafuta mbinu za kuinasua
timu na sio kufuja kidogo kinachopatikana.
“Mimi nikiwa kama mjumbe wa Maji
Maji baada ya uchaguzi wa hivi Karibuni ningependa kuona Timu yetu inasonga
mbele na uongozi mpya ulioko madarakani usirudie makosa yaliyofanyika huko
nyuma.
Makocha wa kigeni
“Wanafaa kuleta changamoto kwa
makocha wazawa lakini ifikie wakati pia makocha wazawa wawezeshwe kama wa nje
pindi wanapopewa nafasi, kama Nigeri walivyoweza kufanya kazi vizuri na Kocha
wao Stivin Keshi nasi tuige mfano huo.
Ushauri Binafsi
“Soka la Tanzania linakufa kwa
sababu ya kuitanzama Simba na Yanga lazima Tubadilike,Tff na wadhamini
wazichukulie timu hizo ni timu za kawaida.
“watu wenye machungu na mpira
wajaribu kuzipa udhamini na timu zingine Sio Yanga na Simba Peke yake hatuwezi
kusonga mbele.
Baada ya kustaafu
“Kuanzia mwaka 1989 -1994 nikuwa
nafanya kazi katika shirika la usagishaji la taifa[national milling],kuanzia
hapo nilikuwanafanya shughuli zangu za kawaida ambapo mwaka 2006 nikapata
nafasi ya kuajiliwa na kampuni ya kuuza vifaa vya vipodozi pamoja na vyakula
[Wadswortny Distributor],na pia ni Mjumbe wa Timu ya Maji Maji pamoja na kocha
wa kambalage Veterani.
“Pia nina mke na watoto 6, Mpira
umenisaidia Sana kujuana na watu ambayo ni Slaa kubwa katika maisha hata kupata
kazi National Milling ni kupitia mpira ingwa soka linalipa sasa ivi kuliko enzi
zetu,anaitimisha John Kabisama mwenye umri wa miaka 58 hadi mwaka 2013,
ambaye ni shabiki wa kutupwa kabisa wa Barcelona na Maji Maji ya
Songea,ambapo katika maisha yake hawezi kumsahau Beki wa Yanga
Elisha John kutokana na alimsumbufu wake uwanjani.
mwisho
Chapisha Maoni