Na Alex Mapunda
Rashid
Idd chama.
“kabla ya
kwenda kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika
mwaka 1980 nchini Nigeria tulienda kuweka kambi ya mwenzi mmoja nchini
mexico na tulicheza mechi za kirafiki
hili kujiweka fiti kukumbana na wapinzani wetu nchini Nigeria.
Nakumbuka kuna mchezo tulienda kucheza katika mji wa starehe ambao upo inje kidogo
ya mji mkuu wa mexico,mchezo hule ilikuwa balaa mwamuzi wa mchezo ule aliwatoa
wachezaji wetu watatu kwa kadi nyekundu na tayari wapinzani wetu walikuwa mbele
kwa bao 2-1,lakini Peter Tino alifanya
kazi zuri na akasawazisha lile bao, ubao ukasomeka 2-2.
Baada ya mchezo
ule tulianza kucheza rafu mbaya sana kwa wapinzani wetu kwa kuwa sheria za soka
zinasema mwamuzi aruhusiwi kutoa kadi nyekundu zaidi ya ya tatu uwanjani isipokuwa anaruhusiwa
kuvunja mechi,sisi kwa upande wetu tulikuwa tayari mchezo uvunjike lakini sio kufungwa,tuliendelea kuwapiga buti
hadi mwisho wa mchezo wachezaji wa
mexico walitupa heshima na walishukuru mungu mpira kuisha bila kuvunjika mtu”.
Sio mwingine ni Rashidi idd Chama kwa wapenda
mpira watamkumbuka milele kutokana na
uwezo wake mkubwa wa kusakata kandanda
ambao alikuwa nao hasa miaka ya 1976
hadi miaka ya 1990 akiwa na klabu mbali mbali pamoja na timu ya taifa .
Chama
mzaliwa wa Tabora eneo la ng’ambo, alianza
kusakata kandanda akiwa katika shule ya msingi miembeni kisha Sekondari
ya kinondoni zote za Jijini Dar es salam nyota yake ilianza kung’ara
toka mwaka 1971 wakati alipukuwa akitumikia kikosi
cha watoto katika timu ya yanga kwa
kipindi cha miaka 5 ambapo mwaka 1976 alisajiliwa rasmi kuchezea timu
ya wakubwa ya Dar es salam yang Africa,kutokana na umahili wake
mkubwa wa
kucheza namba zote katika safu ya ulinzi alipata nafsi hiyo akiwa na
umri ya
miaka 17 ambapo bado ailikuwa hajaitimu elimu ya shule ya msingi[darasa
la 6].
Mwaka 1977 Chama alichaguliwa kuchezea timu ya taifa
ya vijana mara baada ya jopo la makocha wa timu ya taifa kubaini uwezo wake
na mwaka mmoja baadae akachaguliwa kutumikia timu ya wakubwa ‘Taifa Stars’
ambapo kwa mara ya kwanza walienda
kushiriki michuano ya challenge mjini
Nairobi.
Na katika michuano hiyo timu ya taifa ya Tanzania
ilitolewaa na timu ya Taifa ya Malawi
katika mchezo wa nusu fainali kwa stahili ambayo haijatokea
tena katika soka,mchezo kati ya Tanzania na Malawi
ulichezwa siku tatu,siku ya kwanza timu
zote zilitoka sare ya bila kufungana
zikapigwa penalti 5 kwa kila upande
ambapo timu zote zilipata ushindi katika penalti hizo mchezo ukahailishwa
adi siku ya pili kwa kuwa sheria za kipindi kile zilikuwa
haziruhusu mapigo ya ziada ya penalti baada ya penalty tano kupigwa.
Timu zote mbili zikalazimika kuingia uwanjani siku ya
pili ili kujaribu tena bahati zao lakini kwa mara nyingine mchezo ulimalizika
kwa sare ya penalti 5-5 hali ambayo ilipelekea mchezo huo kusogezwa hadi siku
ya Tatu huku hali ya kukamiana kwa timu hizo ikaongezeka mara dufu,lakini siku
ya tatu jahazi la Tanzania lilienda mlama mara baada ya mchezaji wa Tanzania kasimu manara, kukosa
penalty baada ya timu hizo kutoshana nguvu kwa mara nyingine ndani ya
dakika 90 ambapo Malawi walipata nafsi ya kuingia fainali huku Killi Stars wakakumbana na ndugu zao toka
visiwani Zanzibar katika kinyang’anjiro
cha kumtafuta mshindi wa tatu na wakafainikiwa kuichabanga bao 2-0
zikisukumizwa wavuni na Peter Tino.
Mwaka 1979 chama aliwapa kisogo yanga na akatimukia
Pan Afrika timu ambayo aliitumikia adi
mwaka 1982 na akarudi tena Jangwani baada ya kuikosa timu hiyo kwa muda mrefu
ambapo alicheza yanga adi mwaka 1988 alipoamua kujiunga na Maji Maji ya Songea timu ambayo aliichezea
kwa misimu kadhaa ambapo mwaka 1990
aliitajika na klabu ya Pamba toka mkoani mwanza.
Safari yake ya mwanza iliambatana na mikosi kwa
kuwa kabla ya kucheza mechi yeyote ya
ligi timu ya pamba ilienda nchini Burundi kucheza michezo yz mjaribio kabla ya
ligi kuaza kitu ambacho kilimkumba
aliumia mguu pasipo kucheza mchezo wowote
na akafungwa pio pii na ndoto za kuchezea pamba zikagonga ukuta akaamua
kurudi Dar.
Baadae mwaka 1991 katibu ya kampuni ya ndovu bwana Twaa funguo alimchua toka dar ili
kuchezea timu ya kampuni hiyo timu ambayo
aliichezea adi mwaka 1996 hapo ndipo
aka kaa chini ya mti na kusema imetosha sasa,akaachana na soka,anaeleza Iddi
chama kwa umakini kasha anaendelea;-
Watu
walinifitini Ndovu.
“Wakati niliposajiliwa ndovu mwaka 1991 watu wengi
walinifanyia fitina kwa wivu wao ambao haukuwa wa msingi huku wakidai kuwa
uwezo wangu wa kusakata kandanda ulikuwa ukingoni lakini sikujali maneno
yao,kitu ambacho nilikifanya ni kuhakikisha natimiza yale yote ambayo
yalinipeleka ndovu na hatimaye walikuja kuikubari kazi yangu ya uwanjani.
Amecheza
mashindo yote ya vilabu na timu zote za
taifa Africa.
“Nimecheza klabu bingwa afrika,kombe la Shirikisho
kipindi kile kombe la washindi,michuano inayoandaliwa na nchi za ukanda wa
Afrika mashariki na ngazi ya vilabu na timu ya Taifa lakini kubwa zaidi
kushiriki michuano ya mataifa huru ya afrika michuano ambayo kwa Tanzania
ilikuwa ni mara ya kwanza na mwisho kwa kuwa adi dakika hii ile rekodi bado
haijavunjwa tena kwangu mimi najisikia faraja kubwa sana.
“Sisi wachezaji wa miaka ya 1970 sijisifii tulikuwa na
uwezo wa hali ya juu sana kuanzia
mazoezi na uwezo wa kusakata kandanda ambao mwenyezi mungu alitujalia na
kikubwa lila mchezaji alikuwa makini na wachezaji wengi wa kipindi kile
waliupenda mpira kwa dhati tofauti na wachezaji wa zama hizi.
kombe la mataifa ya afrika
1980,mwanaume ndani .
“mimi
niliuwa ni miongoni mwa wachezaji wachache ambao tulibahatika kwenda
kuwakirisha taifa letu nchini Nigeria
ingwa nilikuwa na umri mdogo sana
kuchezea timu ya Taifa kwa kuwa niliwanyang’anya namba watu ambao
nilikuwa nawaeshimu sana katika soka la hapa nchini,kiukweli nilifarikika sana.
“kutokana
na ushindani ambao ulikuwepo kwa wachezaji hadi dakika za mwisho wachezaji
ambao walikuwa na uhakika wa kwenda Nigeria walikuwa ni wawili pekee ambaye ni
Juma ponda mali pamoja Athumani mambosasa kwa kuwa walikosa upinzani kwa upande
wa magolikipa hapa nchini, walikuwa
wanatisha.
“baadhi
ya wachezaji ambao tulipata nafasi adimu
ya kwenda Nigeria kupeperusha bendela ya nchi yetu ni pamoja na
Juma pondamali,Athumani mambo sasa,Reopard Mkebezi, pamoja na Mohamed Kajore [marehemu]
“wengine
ni Redga Tenga,Jela mkagwa,Juma mkambi [marehemu],Omari husein,bila kumsahau
Husain Ngurungu,pia wakichagizwa na mimi
mwenyewe,Mohamed salumu,Piter Tino
pamoja na mtu mzima Ally,tuli kuwa
wengi hao ni baadhi ya ninaowakumbuka.
“Tukiwa
inchini Nigeri huku tukiwa na presha kubwa ya mashindano mchezo wa kwanza
tulipepetana na wenyeji Nigeria tulichezea kichapo cha bao 2-1,sawa na matokea
ya mchezo ambao ulifuata ambapo pia
waarabu toka Misri yalitufumua bao 2-1,ambapo tulijikongoja katika mchezo ya
mwisho dhidi ya Tembo wa afrika Ivory Coast kwa matokeo ya sare ya bila
kufungana.
Kikubwa
ambacho kilituponza kutolewa mapema
ilikuwa ni woga wa mashindano kwa kuwa ili kuwa mara yetu ya kwanza kushriki fainali za mataifa ya afrika, kwa
upande wa uwezo wa kusakata kandanda kwa asilimia kubwa tuliwazidi na kinachoniumiza mara baada ya kutolewa katika
michuano ile hadi leo hii hatujapata tena nafsi ya kushiriki mashindano makubwa
kama yale kila nikikumbuka roho inauma sana.
Imani za kishirikina
“siweze kukataa hayo mambo yapo sana watu kuvaa irizi
uwanjani pamoja na kuchinja mbuzi kwa
hizi timu zetu kubwa haya mambo yapo
sana,lakini mimi baba yangu alinipa wosia kwamba mara zote katika shughuli
zangu zote nimtangulize mwenyezi mungu
yeye ndiye mwenza wa yote,na katika mpira silaha pekee ni mazoezi
na kipaji cha kuzaliwa nacho vinginevyo
hata kama ni mtoto waganga mpira utakushinda.
Soka la sasa na zamani.
“vijana
wetu wa sasa hawajitambui starehe
zimezidi tofauti na enzi zetu tulikuwa
na nidhamu ya hali ya juu ndio maana tulikuwa na miili ya kucheza mpira,
kiukweli mpira na starehe ni vitu ambavyo havitangamani lanzima wachezaji wetu
wa sasa wabadilike.
Anaowapenda.
“
Agrey Moris,kelvin yondani,Aathumani Idd pamoja na mchezaji chipukizi wa
wekundu wa msimbazi Ramadhani Singano [MESSI] wanajitaidi kucheza vizuri,
Ushauri
kwa soka la Tanzania.
“Rais
washirikisho la mpira wa miguu hapa nchini awatambue na kueshimu
mchango wa wachezaji wa zamani ambao utakuwa msaada mkubwa kwa timu yetu
ya taifa ,kama atapuuzia wazo hilo bado vijana wetu watakosa madini toka kwa
wakongwe.
“sisi
wachezaji wa zamani hapa nchini kusema kweli hatutambuliki kama wachezaji
wezetu wanavyotambulika kwenye nchi nyingine,viongozi wa sasa wasiteue viongozi
wa soka kisiasa toka katika ngazi za wilaya lanzima kila mtu awe tayari kubadilisha
soka letu.
Baada ya kutundika daruga.
“umri
wangu ni miaka 56 hadi 2013,nafanya biashara ndogo ndogo pia nina duka la vifaa vya
michezo hapa mjini Arusha,nina mke na watoto
watatu mmoja wakiume ambaye
naamini atarithi mikoba yangu pia
yupo kwenye kituo cha michezo ambacho nafundisha hapa Arusha nikiwa kama kocha,
alikuwepo kwenye michuano ya copa cocacola anaitwa Ibrahim Chama anacheza
nafasi ya ushambuliaji.
Chapisha Maoni