Na Alex Mapunda, Iringa
Keneth wane.
Keneth wane ni miongoni mwa washambuliaji
bora walioibuka kwa kasi kubwa na kufifia kama mshumaa uliowekwa kwenye
upepo mkali,alitingisha soka la hapa nchini na jina lake kung’ara vilivyo akiwa
na maji maji ya Songea miaka ya 1994-1997.
Wane ambaye ni mzaliwa wa
kijiji cha chaburuma Songea vijijini Kipaji chake kilianza kung’aa toka
akiwa shule ya msingi chaburuma na baadae akajiunga na red kids timu ambayo
alichezea kwa mafanikio makubwa akiwa katika umri mdogo ambapo kupitia tmu hiyo
alipata nafsi ya kuchukuliwa na chaburuma Rangers timu ambayo ilikuwa
ikishiriki ligi daraja la nne mwaka 1989,timu ambayo hakudumu na baadae
akatimukia posta timu aliyochezea adi mwaka 1993.
Kujituma kwake na kucheza kwa
ushirikiano na wezake huku akisifika kwa kuokoa timu katika mazingira
magumu mara kwa mara,iliwavutia Maji maji ambao mwaka 1994 wakamsajili rasmi
kama mchezaji wa kutumainiwa ambapo mwaka 1997 aliachana na soka na kuendelea
na shughuli zake za kwawaida.
Ubinafsi wa kocha,kupunjwa posho zao
ulimfanya achukie mpira.
“niliamua kuachana na Maji maji kwa
sababu kuu mbili kwanza kocha Suleman Gwaja alikuwa amekamatwa na baadhi ya
wachezaji wakongwe na akaanza kutuchukia wachezaji wengine bila kuweka wazi
sababu za kutuchukia, mimi baada ya kuona sipangwi kwa muda mrefu nikaamua kumwaga
manyanga.
“Kuna kipindi zaidi ya wachoezaji 8
wa kikosi cha kwanza walikuwa majerui lakini kocha kwa mapenzi yake akaondoka
na kikosi dhaifu kwenda mbeya na kanda ya ziwa akiwa na wachezaji pungufu hali
ambayo ilinikatisha sana tamaa baada ya kutuacha songea wakati hatukuwa na
matatizo.
“Vile vile wakati tuko maji maji
tulikuwa tunategemea zaidi posho za uwanjani wakati wa mechi kubwa za Simba na
Yanga na mara nyingi tulikuwa tunapewa elfu 20 adi 30 pesa ambayo ilikuwa kubwa
sana kwa kipindi kile na ilikuwa ikitusaidia sana,lakini kilichonifanya
nikasirike kuna mechi tulicheza na Simba baada ya mchezo huo tulipewa elfu 8
kila mtu huku viongozi wakijilimbikizia pesa nyingi ambazo hawakustahili kwa
kweli kutonana na tukio lile mimi niliamua kuachana na maji maji na kuanza
kuchukia mpira kwa kuwa nilijitaidi kuoji kwa uongozi sikupata majibu
mazuri.
Mkataba Maji Maji ulinizuia kwenda
Simba na Yanga.
“mwaka 1995 Simba na yanga
waliniitaji lakini tayari nilikuwa na mkataba na Maji Maji hali ambayo iliweka
uzibe wa mimi kujiunga na timu hizo na nikabaki na Wanalizombe kwa kuwa timu
hizo zilishindwa kuvunja mkataba wangu.
Tulienda kwa Mganga, tukachezea
kichapo cha bao 5-1
“Tukio hili hadi naingia kaburini
siwezi kusahau,nakumbuka mwaka 1995 tulienda mwanza kucheza na Pamba ya mwanza
viongozi wa Maji Maji wakatupeleka kwa mganga wa toto Afrika ili kutufanyia
dawa kwa kuwa toto na pamba walikuwa wapinzani wakubwa.
“Siku hiyo tulichanjiwa dawa na kila
mmoja aliogeswa dawa Ndoo mbili na siku hiyo tulipelekwa wachezaji 7,lakini
mimi sikufurahishwa na kitendo cha kuchanjwa dawa nikamua kumdanganya mganga
ili asinichanje nilichokifanya nikamwita pembeni na kumwambia kuwa wakati nipo
mdogo nilipatwa na ugonjwa wa ajabu na wazazi wangu wakanipeleka nchini msumbiji
ili kunifanyia dawa ambapo mganga wa msumbiji alinichanjia dawa na akaniambia
mtu yeyote arusiwi kunichanjia dawa hadi kitoke kibari toka kwake baada
ya kumweleza hayo mganga akaduwaa! Sana.
“Lakini baadae akaniambia kuwa hata
nichanja ila atanipa ilizi ambayo nitaweka kwenye ugoko nikakubariana naye,pia
baada ya kuoga dawa mganga alituagiza tukatafute kuku na kumchinja saa saba
usiku na damu yake kuchanganywa na maji pia kuoga kitu ambacho tulikitekeleza.
“kilichotokea kila nikikumbuka
Napata machungu Maji Maji tulilambwa bao 5-1 wote siku ile tulitoka uwanjani
vichwa chini si viongozi wala wachezaji hakuna ambaye alikuwa anaitaji kuongea
na mwezaji na hatukupoteza muda tukaingia kwenye Gari na kurudi Songea.
Nawadai Maji Maji elfu 15 ya usajili
naomba wanilipe.
“Maji Maji walinisajili kwa Elfu
30,lakini adi leo nawadai elfu 15 pesa ambayo viongozi hawakunipa kwa sababu
wanazozijua wao,nawarahumu kwa ukatili huo,kwa kuwa hata wakati tulipokuwa
tukisafiri kwenga kucheza nje ya mkoa wa Ruvuma tulikuwa tukipewa pesa kidogo
ya kula kama ni ziara ya siku 8 mnaweza mkapewa pesa ya siku 4 au tano ikiisha
basi.
“Namkumbuka rafiki yangu Dastan
Mkuni alikuwa akila wali maharage badala ya nyama ili kubana matumizi kwa kuwa
ugali maarage ulikuwa unauzwa bei raisi, hali hiyo iiwafanya wachezaji wengi wa
Maji Maji kucheza chini ya kiwango na timu kufanya vibaya,yote hayo ni uchu wa
viongozi wa kudhurumu timu.
Nawachukia wachizaji wa hapa
nchini kwa uvivu wao.
“Nimeacha Kwenda kuangalia mpira
uwanja wa taifa kwa kuwa wachezaji ambao wezangu wanawasifia wanacheza vizuri
naona wananichefua sana hawafanyi vile vitu vinavyotakwa katika mpira wachezaji
wengi wanafanya mazoezi wakati wakiwa na kocha pekee,sio kwamba nawaonea ndio
ukweli lazima wabadilike,na ukweli wenyewe soka letu tunaenda kulizika huku
tukiona.
Tukio kali.
“Tukio hilo kila nikikumbuka
linaniacha hoi,wakati nipo Maji maji kuna kipindi tulizuiwa katika moja
ya gesti mjini Shinyanga mara baada ya mchezo wetu dhidi ya shinyanga Shooting
ambapo timu yetu ya Maji Maji ilikosa pesa ya kuripia gesti baada ya
viongonzi kushauriana waliafikiana kiongozi mmoja habaki pale gesti hadi pesa
itakapolipwa na tukaondoka kuelekea Moshi kwa ajili ya mchezo mwingine na
kilichotokea Yule kiongozi akatumia ujanja na kukimbia pale gesti tukakutana
wote moshi.
“lakini haikuishia hapo tukiwa
Kilimanjaro tukazuiwa tena katika gesi nyingine ambapo timu ililazimika kumwika
poni kiongozi mwingine na kama ilivyokuwa shinyanga nae alifanikiwa
kutoroka na kurudi Songea ambapo hadi leo hii Maji Maji hawajalipa zile
pesa.
Soka La sasa na zamani.
“siku hizi wacheaji wengi wanapenda
starehe kuliko kufanya mazoezi ya mpira na wanasubiri adi kocha aseme
Fanyeni mazoezi tofauti na enzi zetu sisi ambapo kabla ya mazoezi ya
kocha tulikuwa na mazoezi binafsi ambayo yalitufanya tuimalike zaidi ili kukuza
soka letu lazima wachezaji wajitambue wanatakiwa kufanya kitu gani.
Goli bora alilowai funga.
“tulicheza na shinynga shooting
mwaka sikumbuki mchezo ule ulikuwa mgumu sana kwa Upande wetu Maji Maji kwa
kuwa wezetu walitangulia kutikisa wavu wetu dakika za mwanzo ,lakini kucheza
kwetu kwa juhudi na maarifa hasa kipindi cha pili ilipelekea timu yetu kufanya
mashambulizi ya mara kwa mara langoni kwa wapinzani wetu hali ambalo
ilipelekea kupatikana kona dakika za mwisho na mimi bila ajizi
nikakunjua mguu na kupiga mpira ambao ulienda kwa kasi kubwa na kujaa wavuni
pasipo kugusa mtu yeyote huku mlinda mlango wa shinyanga akiwa ana la kufanya.
Atoa somo kwa Malizi.
“namweshimu sana kiongozi mpya wa
shirikisho la soka hapa nchini kwa sasa Jamal Emelani Malizi kwa ukomavu wake
katika kuongoza mpira,lakini ili aendelee kurinda heshima yake namshauri
kuimalisha na kujenga shule za mpira kwa wingi nchi zima ili kupata sura mpya
zenge uwezo sahhi wa kucheza mpira na kuachana mfumo wenye haibu wa sasa wa
kupeana nafasi za kucheza mpira kwa kujuana mimi naamni kama hilo
litatekelezwa soka letu litapanda chati.
Ushauri kwa Wanalizombe.
“Viongozi wa Maji Maji lazima
watambue kuwa mpira wa miguu kwa sasa unaitaji pesa na ushauri toka kwa
wachezaji wa zamani wakilitambua hilo Timu itafanya vizuri kinyume na hapo maji
maji itachelewa sana kurudi ligi kuu.
Baada ya kustaafu soka.
“Nina mke na mtoto mmoja,pia nashukuru
mungu naishi vizuri na familia yangu ingwa soka halikunifanyia chochote lakini
kwa sasaa naenelea na shughuli zangu za kawaida,anahitimisha wane ambaye
anamkumbuka sana mwalimu wake Rashid Kato ambaye alimweka katika ramani ya
soka,anaomba wadau wa soka na wapenda michezo kwa ujumla wamtafute kupitia simu
namba 0712628063.
mwisho
Chapisha Maoni