Na Sophia Mwaipyana,Mbeya
SAMU MKONO
Miaka ya nyuma mikoa
mingi ilikuwa na timu zilizo kuwa zina shiriki ligi kuu katika mkoa wa kigoma
uliyo barikiwa kuwa na mastaa wengi wa muziki uliwakilishwa na timu ya
Mbanga Fc.
Ambayo ilikuwa ikiweka kambi
katikati ya mji wa Kigoma paleeee ujiji na walikuwa wakitumia uwanja wao wa
nyumbani Lake Tanganyika ilikuwa timu iliyo sheheni vijana hodari sana miaka
hiyo.
Samu Mkono ni kati ya
wachezaji waliyo itumikia timu hiyo huku akipitia timu nyingi
kutokana na umahiri wake katika soka .
JELAMBA ilikutana na Samu
Adamu maarufu kama samu mkono jina alilo pewa na golikipa wa Tukuyu
Stars kipindi kile ilipokuwa ikitikisa katika soka Emmanuel
Mwasile.
“Nilianza soka toka nikiwa
darasa la tano katika shule ya msingi Ikuti iliyopo mkoani Mbeya na baada
ya hapo nikaenda shule ya sekondari Mbalizi na nikachanguliwa kushiriki
katika mashindano ya umisenta yaliyo fanyika Arusha na tukawa washindi
watatu kanda ya nyanda za juu kusini”
“Nakumbuka wachezaji
tuliyoenda nao nipamoja na Fred Mbuna yeye akitokea Iringa na alikuwa
msaada mkubwa sana katika timu yetu ya nyanda za juu kusini kwani nakumbuka
alifunga magoli mengi”
“Lakini wakati nipo kidato
cha kwanza nilikuwa naichezea timu ya Mbalizi Rangers kwani mkuu wa shule
yetu alikuwa ndiyo meneja wa timu hiyo ,hivyo alinichukua na kunisajiri huko”
“Mwaka 1998 hadi 1999 nikachezea Tazara mwaka 2000-2003 niliichezea Tukuyu Stars mwaka huo huo
nilienda Mbanga Fc mwaka 2004 nikaenda Zanzibar hadi mwaka 2006 nikatua
Tanzania Prisons ambapo nikacheza hapa mpaka 2010”
“Nikiwa Tanzania Prison mwaka
2008 niliitwa katika timu ya Taifa lakini bahati mbaya nilivyo fika kambini
Shinyanga ndiko kocha Maximo alikokuwa ameweka kambi niliumia kifundo cha
mguu hivyo nikarudi bila kucheza hata mechi moja”
“Niliumia sana kuona
nimeshindwa kwenda kuitetea Nchi yangu ila nilikubariana na hali
nikarudi nilipo pona nikaendelea kucheza katika timu yangu”
Kwanini Tanzania
Prisons imepoteza ubora kama zamani
“Daah unajuwa kipindi
chanyuma wachezaji wengi tulikuwa na uwezo vipaji ila tulijisahau kuandaa
kizazi ambacho kilitakiwa kitupokee sisi pale tutakapo choka nazani hapo ndipo
tulipo kosea ndiyo maana sahizi tunashindwa kurudi katika ile hali ya zamani”
Ushirikina katika soka
“Ushirikina upo
nakumbuka kunasiku tulikuwa tunaenda kucheza Kahama tulisafiri na
waganga watatu katika basi tulivyo fika njiani mganga akasema tushuke kila mtu
akachume majani ya mti ndiyo tuendele na safari tulifanya hivyo kasha
tukaendelea na safari”
“Tulivyo fika kahama mimi
niliumwa kwahiyo sikwenda uwanjani na chumba nilicho kuwa nimelala kilikuwa
karibu na Yule mganga akaja kaniambia hii mechi ni ngumu kwahiyo naenda
uwanjani ila inabidi uweunaingia chumbani kwangu uangaliage vitu vyangu”
“Kule chumbani alikuwa
ametega vitu vyake na alikuwa amewasha mishumaa hivyo iliisije kunguza vitu
kanambia niwe naangalia nikafanya kama alivyo niagiza
nilienda kama mara mbili nikakuta kilakitu kiko sawa ile naenda mara ya tatu
nikakuta ile mitego yake imelipuka kumbe kule mpira ulikuwa umeisha na
tumefungwa goli 3 ile wakati natafakari akawa amerudi akasema nilikuwa nimesha
ona kilicho tokea huku”
“Baada ya hapo tulikuwa
tunaenda kucheza Morogoro kwahiyo wale waganga wote waliachwa
kule iliwarudi kwani walishindwa kazi natulivyo fika Morogoro
tulitoka sale ya goli 1-1”
Mbanga Fc ilikuwa ni timu ya
aina gani
“Ilikuwa timu nzuri kwasababu
aliyekuwa anaimiliki alikuwa anatoa huduma vizuri kwa wachezaji hadi viongozi
na kambi tulikuwa tukiweka pale pale ujiji na uwanja wetu wa
nyumbani ulikuwa ni Like Tanganyika”
Tukio gani baya kwako
katika maisha ya soka
“ Niule mwaka nilipokuwa
nachezea Tukuyu Stars nilikuwa nimekaa mda sana bila kucheza kwasababu
nilikuwa nimeumia mguu lakini siku hiyo nikaingia uwanjani ilikucheza na
Afc baada ya kuairishiwa mechi mara ya kwanza kwasababu golikipa wao
alifia uwanjani kwahiyo walipo kuja mara yapili nikapangwa kucheza”
“Ile nimecheza kidogo
nikaurukia mpira narudi chini nikavunjika mguu tena ilikuwa karibu na pale
alipo angukia Yule golikipa wao aliye kufa kwahiyo niliwaza sana
kuwa yawezekana na mimi ningeenda kama mwenzangu”
Kwanini hukudumu Tukuyu Stars
“Nitimu ambayo niliipenda na
nilifanya vizuri sana kutokana na mwalimu wangu West Gwiva nilikuwa
nampenda sana kwani nilikuwa namwelewa sana”
“Ilashida ilikuja pale
uwongozi wao ulinibania mimi kwenda kucheza Simba yani ilikuwa hivi
viongozi wa simba waliongea na viongozi wangu kuwa wananiitaji lakini
viongozi waliwaambia kuwa eti mimi bado mdogo na nimewaomba waendelee kunilea
kimchezo hadi miaka miwili ipite”
“Kumbe wao hata
hawakunihusisha katika hilo swala sasa siku moja nikiwa mapumziko dar
–es-salaam nilikuwa uwanja wa taifa naangalia mpira nikakutana na kiongozi wa
samba”
“Akaniita kaniambia wewe dogo
vipi Simba wanakuhitaji wewe unasema bado mdogo hujui huku kama utalipwa vizuri
nilibaki namshangaa kwani zile habari kwangu zilikuwa ngeni “
“Kwahiyo ndiyo akanieleza
kuwa tuliongea na viongozi wako kuwa tukusajiri huku wakasema eti umesema
undelee kuwa pale hadi miaka miwili ili waendele kukulea kwani bado mdogo
toka hapa sikutaka tena kurudi Tukuyu nikaenda zangu Mbanga Fc kigoma kwani
walikuwa wananiitaji”
Ilikuwaje siku ya kwanza
kucheza na timu kubwa
“Msema kweli mpenzi wa mungu
kiukweli mwalimu wangu aliniandaa sana kisaikolojia na kweli mechi yangu
ya kwanza kucheza na timu kubwa ilikuwa ni Simba na Tukuyu Stars mwalimu
alijuwa kama nitacheza katika kikosi chakwanza hivyo alitumia mda mwingi
kunijenga “
“Najioni ilopo fika mwalimu
aliniita nakuniambia mechi ya kesho nimechi ya kawaida sana kwahiyo
ichukulie kama mechi nyingine lakini nahisi bila mwalimu wangu West Gwiva
ningelala na hofu kubwa ila kwa ajili alivyo nijenga wala sikuogopa na
nilicheza kwa kujiamini sana”
Kwanini uliachana na
mikikimiki ya soka ukiwa bado unanguvu
“Nikweli kilicho
fanya niachane na soka mapema ni mguu kwani hadi leo unanisumbua kwahiyo toka
nivyo umiaga mguu ukawa kikwazo kikubwa kwangu kwani kila mara ulikuwa
unanisumbua nikaona bora nipumzike”
Mafanikio uliyo yapata
kupitia soka
“Heshima kazi mdogo
wangu leo hii mimi niko kazini kutokana na mpira kwahiyo mafanikio
niliyonayo kwasasa chanzo chake ni mpira ,pia kutembea sehemu mbalimbali na
kufahamika”
Ilikuwaje hadi ukaitwa Samu
mkono
“Nakumbuka hili jina
lilizaliwa nikiwa nachezea Tukuyu Stars kunagolikipa mmoja alikuwa
anaitwa Emmanuel Mwasile aliniita hivyo kutokana na nilivyo kuwa
namlinda akiwa golini kwahiyo alikuwa ananiambia jamaa unanilinda kama mkono
vile kwani mkono tunatumia kufanyia kujikingia nakila kitu”
“Kwahiyo toka hapa nikawa
naitwa Samu Mkono ukija hata hapa kazini ukisema Samu Adamu utaambiwa
hatumfahamu ila ukisema Samu Mkono hata mtoto anakuleta nyumbani”
Ushauri wako
“Wachezaji wajitahidi kufuata
maelekezo ya mwalimu iliwaweze kuwa wachezaji wazuri wacheze mpira wa
kimataifa kama Sammata”
Maisha yako ya sasa
“Kwasasa mimi ni askari
magereza na ninaendelea na shughuli zangu ndogondogo “
“ Ninamke na
watoto watatu nawapenda sana kwani mke wangu mama Norin
alikuwa akinipa sapoti sana kipindi nilipokuwa nacheza mpira ingawaje enzi hizo
ndiyo tulikuwa bado tuko katika uchumba lakini yeye alikuwa ndiye mshauri wangu
wakwanza na kunifariji pale ninapokuwa katika matatizo”
MWISHO
Chapisha Maoni