AUGUSTINE LUHOLE.
MIONGONI mwa
wachezaji wazuri katika safu ya ulizi ambao walipata kuwaika hapa nchini miaka ya
1980 hadi 96 ni pamoja na Augustine
Lihole ambaye alicheza kwa kiwango cha hali ya juu akiwa na Tumbaku ya
morogoro,mseto ya morogoro pamoja na Lipuli ya Iringa Timu ambayo aliichezea
kwa mafanikio makubwa katika historia yake ya kusakata kandanda.
Luhole mzaliwa
wa mkoani mara Wilaya ya Talime, alianza kuburuza gozi la ng’ombe toka akiwa
shule za msingi ikiwemo Shule ya kawe dar,shule ya uhuru Arusha[jakalanda]
pamoja na shule ya mchikichini Morogoro
lakini kiwango chake kilikuwa zaidi akiwa na umri wa miaka 16 katika sekondari
ya Forest hill na alicheza katika michuano ya Umiseta kanda ya mashariki kipindi
hicho timu za mtaani zilianza kumgombania kama mpira wa kona.
Lakini katika
maojiano maalumu na Gazeti la championi anafafanua yafuatayo kuhusu maisha yake
ya mpira:-
“nilianza
kucheza mpira kwa kiwango kikubwa nikiwa na Timu ya Tumbaku ya Moro tarehe 26
mwenzi wa nne 1976, timu ambayo nilijiunga nayo lengo kubwa likiwa ni kupata
kazi suala ambalo nilifanikwa na nilikuwa nilikuwa nikilipwa elfu moja na mia nane,ambapo kipindi kile
kupata kazi ilikuwa ngumu sana,timu hiyo niliichezea kwa kiwango kikubwa sana ambapo mwa 1986/88 nikajiunga na timu ya
mseto ya morogoro baada ya kutokea lidandasi katika timu ya tumbaku na baadhi
ya wachezaji wakaachishwa kazi nikiwemo mimi.
“sikudumu na
Timu hiyo nikajiunga na lipuli ya Iringa 1988 mwenzi wa 12 baada ya kiongozi wa
lipuli Laurence kunifuata morogoro ili kunisajiri pamoja na mwenzangu Venansi
moshi na kipindi hicho lipuli ilikuwa ikitafuta wachezaji wenye sifa ili kuipandisha timu hiyo ligi kuu.
“nakumbuka
tulipigana sana ili kuhakikisha Lipuli inapanda Daraja na baadae timu ikacheza
vizuri hadi ikapanda daraja na ikacheza ligi kuu,nakikumbuka Kikosi bora cha
lipuli ambacho kilikuwa tishio cha mwaka
1990/92 baadhi ya wakali ambao walikuwepo ni pamoja na Kipa Ivo ng’itu,Kongo
Mruge,Gula Mathias,cristopher Kienes,Ezekiel Mpande[marehemu]pamoja na Heri ngunja
[marehemu]
“wengine ni
Chachage Bokaza,Ikupirika nkoba,Shabani musa,Julias ngawambala,mchele
mchele,Felix Jogoo chama,Agostino Luhole,Mohamed keto pamoja na Athumani
Kilambo,makocha wa timu hiyo alikuwepo pasco Bela pamoja na Phiri kocha Toka Zambia.
Baada ya
kuitumikia Lipuli kwa moyo mmoja baadae alichaguliwa na timu kwenda Zanzibar ili
kusomea mafunzo ya ukocha baada ya kufaulu akarudi kuja kuifundisha lipuli
ambapo kufikia mwaka 1996 aliondoka Iringa na kuelekea pwani ili kumtibu mtoto wake
alikuwa mgonjwa,akiwa huko alifundisha timu ya kisalawe sports club na akaifikisha
hadi ligi daraja la pili na kufikia 2003 akarudi mara ambako alifundisha timu
ya Msoma JK football klabu timu ambayo
ilikuwa ikishiriki ligi ya mabingwa ambapo mwaka 2008 akachuliwa na polisi mara
ambapo walitolewa kanda na timu toka kigoma na baadae akajiunga na timu ya
Polisi Tarime Timu ambayo anafundisha hadi hivi sasa.
Tulinusurika kufa mikumi
“nakumbuka
nikiwa Lipuli tulitoka kucheza mpira Dar,tulipofika mikumi eneo la Iyozi Dereva
alipaki gari vibaya, mwenyewe akaenda kununua mkaa baada ya muda mfupi kuna
gari kubwa lilitokea gafla mbele yetu ilikatugonga na kutuburuza kwa umbali wa
mita 25 na mimi nilikuwa nimekaa mbele ya gari hilo nashukuru mungu Tulitoka
Salama.
Waamuzi wanaua mpira wetu
“wakati nipo
lipuli Tulienda kucheza na yanga jijini Dar katika mchezo ambao ulikuwa mgumu
sana katika mechi hiyo mwamuzi alitoa maamzi ya ajabu sana,nakumbuka mpira
ulikuwa umetoka nje baadae ukanaswa na mchezaji wa yanga na akamimina crosi na
kutufunga bao mwamuzi akaita kati,wakati hata watoto wadogo waliona kuwa mpira
ulitoka nje ya uwanja,katika mechi hiyo yanga waibuka na ushindi wa bao 1-0.
“pia wakati
tulipopigania lipuli kupanda daraja Tulienda Tabora kucheza na milambo na
kipindi hicho milambo ilikuwa timu tishio kwa kuwa ilikuwa ikibebwa sana na
mkuu wa mkoa wa kipindi hicho mzee gama alisimama kidete ili kuhakikicha timu
hiyo inapanda daraja,tulianza kwa kuwafunga bao moja baadae mwamuzi akatoa penalti
ya uongo na milambo wakasawazisha ambapo
kwa msimu huo milambao na lipuli zote zikapanda daraja.
Ushirikina
“nakumbuka
nikiwa na Tumbaku ya moro tulicheza na pan Africa sisi tulikuwa na mzee wetu wa
kamati ya ufundi,siku ya mechi aliingia chumbani ili kuhakikisha anaweka vizuri dawa kwa ajili ya mechi kitu
ambacho kilitokea ni kwamba tulichezea kichapo cha bao 4-0.
“wakati wa
kubadilisha nguo yule mzee akatoka chumbani na kutuambia kuwa wakati wa mpira
umefika twendeni uwanjani tukamwambi tumecheza alishangaa sana kumbe
kilichotokea mzee wa kamati ya ufundi wa pan Afrika alimpiga dawa ya usingizi
ili kufanikisha malengo yao ya kutufunga.
Zamani&sasa
“wachezaji
wavivu pia wanapenda starehe mpira sio maigizo kama tunataka kufanya vizuri na
timu ya taifa.
Anaempenda
“Elius maguri
mchezaji wa simba ambaye amesajiliwa na simba ni mchezaji mwenye kipaji na
atafika mbali.
Stasahau.
“tulienda
shinyanga kucheza na RTC shinyanga nikiwa na Lipuli ya Iringa tukiwa kule mashabiki
walifanyia fujo baadae tukahaidi kulipa kisasi kwetu pia, hata mashabiki wetu
baada ya kupata taarifa walikasirika sana,kweli walipofika mashabiki wa iringa
wakaripa kisasi kwa huwafanyia fujo ambapo RTC Shinganga walisindikizwa na helkopta ya polisi hadi
Ilula nje kidogo ya mji wa Iringa.
Ushauri kwa stars&Lipuli
“Timu ya
Taifa ijegwe kwa muda mrefu na pawepo na shule za michezo za kueleweka ili
kuwakuza wachezaji wetu tofauti na ilivyo hivi sasa haieleki wachezaji wanatoka
wapi.
“timu ya
lipuli ni timu ya wanairinga wote kila mmoja akumbuke kuwa
mchango wake ni muhimu kwa Lipuli,pia nawaomba viongozi wa lipuli
kuandaa mechi ya maveterani waliocheza timu hiyo kwa lengo la kuwakutanisha
wachezaji wazamani wa lipuli na wachezaji wa sasa pia kutoa hamasa kwa wadau
kuchangia timu hiyo.
Baada ya kustaafu soka.
“umri wangu
ni miaka 55 nina mke na watoto 5,sasa ivi ni kocha pia nafanya biashara ndogo
ndogo ili kujikimu kumaisha”,anahitimisha luhole.
Chapisha Maoni