Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.






 NA ALEX MAPUNDA.
Description: https://mail.google.com/mail/u/0/images/cleardot.gif






Maji maji FC.
            
Miongoni mwa Timu ambazo zilitokea kuwa tishio hapa nchini miaka ya 1980 hadi 2000 ukiachana na Simba na yanga kwa wapenda soka lazima ataikumbuka Maji Maji ya Songea Maarufu kwa Jina la Wanalizombe.
Maji Maji ambayo Ilizaliwa rasmi mwaka 1977 kwa muunganiko wa timu mbali mbali mjini Songea chini ya Mwasisi wa timu hiyo Dk Roulence Gama ilianza kupata umaarufu mkubwa mwaka 1980 mwaka ambao timu hiyo ilipata nafasi ya kushiriki kwa mara ya kwanza ligi Daraja la kwanza hapa nchini.
Jelamba viwanja imefanya Mazunguzo Maalum na aliyewai kuwa Meneja wa Maji Maji Aly Mbalika Kuanzia mwaka 1997 pia Meneja wa Sasa Godfrey Ambros Mvula ambao Baba zao walikuwa watu muhimu sana ndani ya Maji Maji Miaka ya 1980, Kwanza mzee Mbalika anaanza kueleza histori ya timu hiyo kuanzia mwaka 1980 hadi 2001;-
“Mzee Gama baada ya kuwasili Mkoani Ruvuma alianzisha azimio la Mlale akiwa kama mkuu wa mkoa likiwa na maana ya kilimo Pamoja na michezo lakini kwa upande wa michezo hakuenda mbali sana hasa alilenga zaidi mchezo wa mpira wa miguu akaazisha timu ya Maji Maji na kujenga uwanja Wa Maji Maji uwanja ambapo vyumba vyote vya uwanja huo aliwapangisha wachezaji wa Maji Maji Na kuwanunulia fenicha.
“Timu hiyo kwa mara ya kwanza ilikuwa chini ya kocha Mahili king Kibadeni ambaye aliiongoza timu hiyo na ikaanza kupata umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wa kipesa ambao timu hiyo ulikuwa nao na kuweza  wa kusajili wachezaji toka kila kona hapa nchini na nje kutokana na mwenendo mzuri wa timu hiyo maji maji ilipata nafasi kuchukua ubingwa wa muungano mara mbili mfululizo mwaka 1885 hadi 1886.
“Lakini mara baada ya Gama kuhamishwa miaka ya 1990 timu ilianza kuteteleka ilikuwa chini ya mkuu wa mkoa mwingine mh Banduka ambaye licha ya kufuata misingi ya Gama kuna kipindi lilitoka Tamko kuhusu timu hiyo kujiendisha yenyewe ombi ambalo lilishindwa kukubarika moja kwa moja  lakini mkoa wakatoa kibari cha timu kujiendesha yenyewe na wakasaidia kuipa uwezo wa kufanya  Biashara kama kuuza mbolea pamoja na bia ili kupata pesa ya kuweza kuikwamua timu na mwaka 1995 Banduka akahamishwa na akaja Mama Anna Makina.
“Makinda aliikuta maji maji ikiwa imeteteleka ambapo viongozi wa Timu wakamfuata na kumueleza kuhusu Azimio la Mlale ambalo mzee Gama alilianzisha ambapo Mama Makinda akufumbia Macho akalipokea kwa mikono miwili na kuanza kulifanyia kazi na akatangaza kufanya kila kitu kuhusu Maji Maji.
“Kweli Maji Maji ikasajili wachezaji wazuri na kila mchezaji kutimuziwa maitaji yake yote Ikiwa ni Pamoja na kuwafungulia akaunti  benki na kumwajili kocha ambaye alimlipa Laki 500,000 kwa mwenzi na akaamlisha kuwa kwa kila mechi ambayo Maji Maji watacheza mapato ya uwanjani asilimia 70 zitaenda kwa wachezaji wakishinda ,sare asilimia 60 na wakifungwa asilimia 25 ili kuwapa faraja wachezaji na kutambua kazi yao wawapo uwanjani.
“Uwezo wa Maji Maji ulipanda gafla ambapo 1996 ikachua nafsi ya 4,mwaka1997 nafasi ya 3 na mwaka 1998 Maji maji ikachukua ubingwa wa muungano kwa mara ya  tatu chini ya wachezaji Bora kabisa hapa nchini.ambapo mwaka huo wachezaji ambao walikuwa Tishio kwa timu hiyo baadhi yao ni hao wafuatao;-
Shaib Kambanga,David Mjanja,Omari Kapilima,Godfrey Kikumbizi,Jemes Mwagama,Stevin Mapunda,John Alex,Kelvin Haule pamoja na Doyi Moke,
“Wengine ni Dello Ntumba,Omari Hussein,WIlle Martin,Said Msham,Samson Poul, Hamis ngwena pamoja na Amri Said   kikosi ambacho kilikuwa bora hapa nchini kuwai tokea kwa timu ya maji Maji ambacho ndicho kikawa kikosi cha mwisho cha ushindi.
“Miaka ya 2000 Makinda akaondoka na akaja mweshimiwa Said Said Kalembo kama mkuu wa mkoa mpya ambaye akaondoa moja kwa moja Mpango wa kuisaidia timu hiyo kwa asili mia 100 ambapo akatangaza rasmi kuwa mkoa umefikia kikomo kuendelea  kuisaidia Maji Maji na timu hiyo  itaendeshwa na wanachama kama katiba ya timu inavyosema.
“Tamko lile lilizoofisha sana Maji Maji na wakajaribu kwenda kubembeleza lakini majibu hayakubadilika pia wakajalibu kufikisha Taarifu kwa mweshimiwa Gama ambaye kwa kipindi hicho alikuwa mweshimiwa mbunge,lakini gama ilisema kuwa kama mkoa umekataa kusaidia timu mimi sina la kufanya na uwezo wa kusaidia timu kwa sasa sina ila ninachokiomba mkateue watu maalum ili kwenda kubembeleza tena kwa mkuu wa mkoa na akikataa mimi naamini Maji Maji haitakuwepo lazima Itashuka Daraja.
“Maji Maji ilijalibu kuwatuma wazee kwenda kwa mkuu wa mkoa kubembeleza kwa Mara nyingine napo Majibu hayakutofautiana na yale ya mwanzo na timu ikawa katika hali Mbaya na Mwaka 2000 timu ya maji maji ilishuka Daraja lakini Maji Maji wakawa wajanja wakaipeleka Tff  Mahakamani kwa kukiuka sheria.
“kitu ambacho Kilitokea  Maji Maji walishika nafsi ya tatu toka mwisho na toka miaka ya nyuma timu mbili ndizo ambazo zilikuwa zinashuka Daraja lakini kwa msimu ule katikati ya ligi TFF wakatangaza kuwa kuanzia mwaka huo timu tatu ndizo  zingeshuka daraja badala ya mbili na mwishoni mwa ligi Maji Maji wakashika nafasi hiyo ya Tatu hapo ndipo wakaenda maakamani  na kuwashitaki TFF kuwa walikosea badala yake wangetangaza toka mwanzoni mwa ligi na sio katikati ya ligi Wanalizombe wakashindi kesi hiyo lakini kutokana na kwamba maji maji ilikuwa katika hali Mbaya Sana ikashuka Daraja Rasmi Mwaka 2001.anahitimisha mzee Ali Mbalika ambaye alikuwa meneja wa timu ya Maji Maji kwa kipindi hicho.
Lakini kuanzia Mwaka 2003 katibu mkuu wa Sasa wa cha mpira wa miguu manispaa ya Songea  Bwana God Mvula akateuliwa Rasmi kuwa Meneja wa Timu ya Maji Maji nafsi ambayo anaishikilia hadi hivi sasa, na hapo anaendelea kusimulia Histori ya Maji Maji kipindi Cha Utawala wake.
“Mwaka 2002 Maji Maji ikapanda daraja lakini kutotana na timu kuendeshwa kwa mfumo wa kutembeza Bakuri  hali ilikuwa ngumu sana kuendesha timu ambapo mwaka 2005 timu ikashuka tena hali iliyopelekea kwa timu hiyo kuwa katika mazingira magumu sana,ambapo baada ya kushuka daraja timu ilipata wasamalia wema ambao walikuwa ni wanaruvuma waishio Dar,wakafanya usajili wa nguvu na timu ikaweka kambi ya kudumu Dar lakini mechi zake ilikuwa inachezea kama kawaida Songea na wakafanikisha kuipandisha timu.
“Lakini Baadae wanacha wa Maji Maji wakagawanyika na wengi wao wakadai timu irudi Songea hali ambayo ilisababisha ugomvi mkubwa sana na wale wafadhili wakaachia timu na kumbuka mwaka 2007 timu ilishuka daraja tena ambapo mechi ya mwisho tulicheza na Kahama United tukafungwa bao 3-2 kwa kipindi hicho maji maji ilicheza kwa Takribani mechi Tatu ikiwa na wachezaji saba pekee mara baada ya kutokea mpasuko kati ya wanachama.
“Mwaka 2008 timu ikapanda tena daraja mara baada ya kupigana kwa kutumia nguvu kubwa sana na ikafanya vizuri kwa misimu ya hawali ambapo mwaka 2010 timu ilipata uzamini toka Caspian ambapo ikapata vifaa vya michezo na pesa za matumizi ndani ya timu, lakini zikiwa zimesalia mechi Tano ligi kumalizika ulitokea Ugomvi mkubwa sana kati ya wanachama na uongozi wa timu mimi nikiwa kama meneja wa timu wanachama walidai kuwa timu ilikuwa inafanya vibaya na ili kuinusuru wakaichukua na kuiweka mikononi mwao na Sisi Kama viongozi Tukaamua kujiuzulu na wanachama wakateua uongozi wao.
“uongozi wa wanachama ambao uliendesha timu hiyo mwenyikiti alikuwa Bwana Haule makamu Hamis Ponela Huku meneja wa timu akiwa ni Stivin Mapunda [Garrincha] ambapo wajumbe alikuwepo Mathias Nyoni,Mponda Hamidu,Mr Sayuni pamoja na Said Mangwe.
“uongozi huo ambao ulifadhiliwa na bwana Super feo,Ottawa pamoja na Mdaula kwa kutoa kiasi kikubwa cha pesa ili kuinusuru Maji Maji hata hivyo Maji Maji haikuwa na bahati 2011 ikashuka Daraja.
“Baada ya timu kusuka Daraja na kupoteza kabisa mwelekeo Mimi na Henly Kabela tukaamua kuchukua timu na kuanza kufanya usajili kwa juhudi zetu na tukaunda uongozi wa mpito kupitia kwa chama cha soka Manispaa ya Songea [Sufa]ambapo Mwenyekiti alikuwepo Hamis Gayo,Mkamu Benjamin Mwakasonda, katibu Henily Kabera,Katibu mwenezi Hossam Hassan Ulaya huku Mimi mwenyewe God Mvula nikaendelea kubakia katika nafasi ya umeneja,na mwenyekiti wa sasa wa timu Mwana Millanzi alikuwa Mjumbe wa Timu.
“Na tukaanza harakati za kuinasua timu kupanda daraja ambapo hadi hivi sasa bado tunapambana ili kuhakikisha timu inasonga mbele kwa kuwa timu imefanya usajili wa kweli baada ya uongozi wa mpito Kumaliza Muda wake, Anasimulia Mvula Kisha anaendelea.
Hali ya Maji Maji kwa hivi Sasa.
“Bado ina hali ngumu kwa kuwa timu ipo katika kipindi cha usajili na tunahitaji pesa za usajili ili kukamilisha usajili na kuiendesha Timu Bajeti ya maji maji kwa mwaka ni Tanzania millioni 109 pesa ambayo bado haipo mfukoni na inategemea kupata toka kwa wanachama.
“Na sisi kama uongozi tumesha anza kuchukua hatua mbali mbali ili ili kuhakikisha tunainusuru timu ikiwemo kusani Mkataba na Kampuni ya Nssejere Sports Toka mchini marekani kwa ajili ya kutengeneza vifaa vya michezo vyenye nembo ya timu ya Maji Maji ambavyo Tayari baadhi ya vifaa vimeshaingia hapa nchini na vitauzwa kwa wadau wa michezo na wanachama wa timu ya maji maji.
Inakoelekea Maji Maji
“Hivi karibuni sisi Maji Maji kwa kushirikiana na Kampuni ya Mwandi ikiwakutanisha wadau wa soka mkoani Ruvuma chini ya mkuu wa Mkoa Mh Saidi Thabiti Mwambungu walifanya mkutano na kufikia mwafaka kuwa timu hiyo sasa imaenda kuvunja recodi hapa nchini kwa kuwa timu ya kwanza kuendishwa kwa mfumo ya kumiriki hisa mchakato ambao umeshapamba moto.
“Na Akieleza katika Mkutano huo ambao ilifanyika hivi karibuni Mjini Songea  mwakilishi wa Mwandi bwana Abel Ngilangwa aliziweka wanzi faida ya Timu Kuendeshwa kwa mfumo wa kampuni ikiwa ni Pamoja na Timu kuwa na uwezo wa kumiriki Mali zake pasipo kuingiliwa na mtu yeyote ambapo mtu yeyote ili awe na uwezo wa kuwa msemaji katika timu lazima awekeze hisa kwa kuwa mfumo wa kampuni wanachama watabaki kama Rafiki wa timu.
“Mkutano ambao ulifikia mwafaka na mchakato wa Maji Maji kusajiriwa Kuwa Kampuni umeshaanza mara moja huku Bado wakiwa wanaendelea kushirikiana na Tanzania mwandi ili kukamilisha zoezi hilo na hisa za Maji Maji zitaanza kuuzwa mara Moja pindi watakapo kamilisha usajiri.
“Wadau wa Maji Maji watarajie Ujio Mpya wa Timu Yao ambao utakuwa wa kisommi zaidi na hapatakuwa tena na ubabishaji ndani ya timu.
Mvula aliwai kusakatata Kabumbu.
“sikufanikiwa kuchezea timu kubwa ila nilikuwa katika kiwango kizuli pindi nilipowa nachezea Bogota Fc na Power Rangers Timu ambazo nilichezea hadi ligi Daraja la tatu ambaapo baadae nikateuliwa kuwa Meneja wa Timu ya Maji Maji.
Tukio Analolikumbuka
“Nikiwa Meneja mwaka 2010 ulizuka ugomvi mkubwa sana kati ya Maji Maji na Yanga Muda Mfupi Kabla ya Mechi mara baada ya yanga kuvuja mlangu wa ofisi ya Club Ya maji Maji na kutokea katika chumba ambacho Maji maji walikitumia kwa ajili ya kubadilishia nguo ili kuingia uwanjani wakidai kuwa Milango ya kuingilia ndani ya uwanja wa Maji Maji kuliwekwa dawa ili wao wafungwe.
“ulitokea ogomvi Mkubwa sana kiasi kwama wanachama wa Maji Maji walitishia Kuwapiga Yanga kwa Kitendo kile lakini kwa bahati zuri wanachama walitulia na mchezo ukaendelea.
“Lakini licha ya Yanga kuvunja milango ya Maji Maji katika mchezo ule walichezea kichapo cha bao 1-0 ambalo liliwekwa kimiani na Tomas Moris mchezaji ambaye wao walimtema.
Wimbo wa Mchaka Mchaka ukipigwa Ni ishara ya Ushindi Kwa Maji Maji.
“Baba yangu alikuwa mkurugezi wa Matimila Bendi pia ilikuwa karibu sana na Mzee mwagama  kipindi hicho nipo shule ya msingi  kulikuwa na wimbo ambao ilitungwa na Amza Clala chini ya bendi yake ambao ulifahamika kwa jina la mchaka Mchaka.
“Sasa Maajabu ya wimbo ule ulikuwa ukipigwa lazima lazima Maji Maji Ipate ushindi pia ilichochea Morali kubwa kwa timu ya Maji Maji na ikapelekea kupata umaarufu mkubwa.
Maisha nje ya Timu Ya Maji Maji.
“Sasa ivi licha ya kuwa Meneja wa Timu Ya Maji Maji pia nina vyeo vifuatavyo;kwanza ni katimu mkuu wa chama cha mpira wa miguu Manispaa ya Songea,pia ni Mwenyekiti wa chama wachezaji [Suptanza],vile vile ni Mmoja wa wakurugezi kwaenye kituo cha michezo cha Good hope Sports na katibu mkuu wa Songea Veterani.
GOD MVULA
“Mimi nina umri wa Miaka 39 nina mke na watoto,shughuli zangu ninazozifanya nje ya soka namiriki duka la vifaa vya michezo pamoja na used sipea pia nanunua vyuma chakavu na mwisho namiriki duka la vyakula,amaitimisha Mvula ambaye pia nishabiki wa kutupwa kabisa wa Maji maji FC pamoja na Mshertani wekundu [Mchester United].
 
LUOGA MCHEZAJI WA ZAMANI WA MAJI MAJI
MWISHO


Chapisha Maoni