Na Alex Mapunda
……………………………………………………………………………………..
Mbwana Makata.
MBWANA makata ni miongoni mwa mlinda
mlango bora ambaye alifanikiwa kutikisa soka la Tanzania miaka ya 1985-92 hapa
nchini akiwa na club ya Tukuyu stars na Yanga ya jijini Dar es salam.
Makata ambaye ni mtoto wa kwanza
katika familia yenye watoto 7,alizaliwa katika kijiji cha makolora mkoani
Tanga,wiki hii amekutana na MWANDISHI WETU na kifanya maojiano maalum, kuhusu
maisha yake ya soka.
“Nilianza kucheza mpira tangu
nilipokuwa shule ya msingi Makolola,Mkoania Tanga,na nilipata nafasi ya kushirika
mashindano mbali mbali licha ya umri wangu kuwa mdogo,lakini nilianza kucheza
soka la ushindani mwaka 1981 nikiwa na Reli ya Iringa hapo ndipo kipaji changu
kilipoanza kuvuma kwa kuwa nilidumu nao kwa kipindi cha miaka 3 na 1984
uongozi wa timu ya waziri mkuu ya dodoma wakanisajili na nilicheza katika
kikosi chao nikiwa kama golikipa namba 1,na tukafanikisha kuifikisha mbali timu
hiyo.
“Kutokana na uwezo wangu wa kujituma
na kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu pindi niwapo langoni,mwaka 86,nikanyemelewa
na Tukuyu Stars ya Mbeya,timu ambayo niliichezea kwa mafanikio makubwa sana kwa
kuwa kupitia tukuyu stars uwezo wangu wa kucheza soka ulijulikana hadi nje ya
mipaka ya Tanzania kutokana na tukuyu stars ilipata nafasi ya kushirki michuano
ya kimataifa yeye akiwa kama golikipa namba 1,mara baada ya timu hiyo
kufanikiwa kulitikisa soka la Tanzania kwa kutwa ubingwa mwaka 1986.
“Hata hivyo nafasi yangu ya kubaki
tukuyu stars ilififia kwa kasi sana kutokana na timu ya soka ya Yang Africans
toka jijini Dar es salam kunisaka kwa udi na uvumba licha ya kwamba timu hiyo
ilikuwa na magolikipa mahili sana hapa nchini ikilinganishwa na timu zingine na
mnamo mwaka 1988 nikajiunga rasmi na Yanga.
“Nikiwa Yanga nilipata upizani
mkubwa sana toka kwa Joseph Fungu na Juma Pondamali ambao kwa hakika walikuwa
na uwezo mkubwa sana wa kulinda lango lakini nilicheza kwa kujiamini huku
nikifanya mazoezi mara kwa mara na mwisho wa siku tukawa tunapokezana Kucheza
katika mechi mbali mbali za ndani na Kimataifa.
Kuondoka Yanga
“Kipindi kile club zilikuwa
hazitulipi mshahara tulikuwa tunapata posho,ila zilikuwa zinamtafutia ajira
mchezaji,mimi nilitafutiwa ajira City council,kakini kuna lidandasi lilitokea
mwaka 1992,hali ambayo ilipelekea kupunguza wafanyakazi na moja ya watu ambao
walikumbwa na zahama hiyo ni Sisi wachezaji ambao tulikuwa tunafanya kazi
katika eneo lile kiukweli baada ya tukio lile maisha yangu ya soka yalikuwa
magumu sana ndani ya yanga.
“Na hasa hukizingatia tukio lile
lilikuwa limetokea muda mfupi mara baada ya kurejea toka kwenye maumivu mazito
ya enka,ambayo yalinifanya nisipate nafasi ya kucheza mara kwa mara, nilikuwa
nikitegemea posho ambayo ilikuwa haikidhi maitaji yangu,na kipindi kile
tulikuwa tunapata posho kubwa katika mechi za Simba na Yanga ambapo tulikuwa
tunachukua elfu 19 adi 20,lakini kwa mechi za kawaida tulikuwa tunachukua elfu
3 au 4.
“Sikufanya ajizi kwa usalam wa
maisha yangu mwaka 1992 nikajiunga na Rtc Kagera timu ambayo ilinihaidi kunipa
ajira ya kudumu,hata hivyo mambo yalienda kombo mnamo mwaka 1993 nikaamua
kutundika Daruga na ukawa mwisho wa maisha yangu ya kucheza soka.
Baada ya kutundika daruga
“Mwaka 1993-1998,niambua kuachana
kabisa na mambo yanayohusu soka nikaamua kujikita katika biashara ili kujijenga
kiuchumi,nilikuwa nikisafirisha bidhaa kama vile vipodozi,viatu, sukari na vitu
vingine vingi katika maeneo mbali mbali,na nilifanikiwa kuiingizia kipato
kikubwa na nikawa naishishi vizuri na familia yangu,lakini mwaka 1998 baadhi ya
viongozi na wadau mahili wa soka wakanishauri kujiunga na mafunzo ya ukocha
kutokana na mchango mkubwa ambao niliutoa kwa taifa pindi nilipokuwa mchezaji.
“Nililidhia kwa moyo mmoja na
nilifanikiwa kupata mafunzo ya ukocha ambapo timu yangu ya kwanza kufundisha
ilikuwa ni Mji Mwapwa ya Dodoma ambayo niliipandisha hadi ligi kuu bara na
nikadumu nayo kwa misimu 3 na mwaka 2000 nikajiunga na timu ya Idd Azan
mweshimiwa mbunge ambayo nilidumu nayo kwa kipindi cha miaka 4,na timu hiyo
ikauzwa na ikafahamika kwa jina la Pan Afrika,na mwaka 2004 nikaamu kuondoka
kwa kuwa timu hiyo ilikuwa imeshapata kocha mwingine.
“Safari yangu ya ukocha ilizidi kuwa
ndefu na mwaka 2004 nilipata nafasi ya ukatibu mkuu wa kamati ya ufundi
ndani ya chama cha soka cha kinodoni,ambapo nikiwa hapo nilifundisha timu ya
Copa coca cola ya kinondoni chini ya umri wa miaka 17,na nikafanikiwa kuchukua
ubingwa wa michuano hiyo.
“Kikosi changu cha chini ya umri wa
miaka 17 cha kinondoni kimetoa wachezaji wengi sana wenye uwezo wa kusakata
kabumbu hapa nchini kwa sasa akiwemo chiritoph Edwald[simba] na Tino Agostino
[prisons] ambao wanafavya vyema kwa sasa katika soka la Tanzania,
“Lakini pia mwaka 2008,nilipata
nafasi ya kuwa kucha wa mkoa wa kisoka wa Kinondoni katika michuano ya Taifa
Cup,ambapo sisi kidondoni tulifanya vizuri sana katika michuano ile na tulikuja
kutolewa na wezetu wa Ilala timu ambayo ilikuwa na wachezaji wengi wa ligi kuu
akiwemo Musa Hasani Mgosi na Mohamed kijuso,chini ya kocha mwezangu Jamhuri
kiweru na wakatawazwa mabingwa.
“Sikuishia hapo baada ya michuano ya
Taifa cup kumalizika nilijiunga na wanakishamapanda Toto Afrika ya Mwanza
ambayo niliifundisha kwa mafanikio makubwa ikilinganishwa na mwenendo wa timu
hiyo kwa misimu mingine lakini mimi niliifikisha nafasi ya Tano ya ligi kuu ya
vodacom Tanzania,lakini nikiwa bado niko Mwanza nilipata nafasi ya kuifundisha
timu ya mkoa wa mwanza mwaka 2009,tukafanikiwa kushika nafasi ya Tatu,na hapo
nikaondoka Mwanza nikajiunga Tanzania prisons ya Mbeya.
“Prisons nilifundisha kwa kipindi
cha msimu mmoja na baadae nikaachana nao na nikapata nafasi ya kuchukua kombe
la Taifa cup nikiwa na timu ya mkoa wa Mbeya,Mbeya Irozi mwaka 2011 hapo ndipo
Nikachukua jukumu la kuonpdoka mbeya na kujiunga na Jkt Oljoro toka mjini
Arusha,timu ambayo naifundisha hadi hivi sasa na nimemaliza nayo ikiwa katika
nafsi zuri, ligi kuu Vodacom Tanzania bara
katika msimu wa ligi uliomalizika
hivi karibuni kwa Timu ya Yanga kunyakua ubingwa wa ligi hiyo.
Ushirikina michezoni
“Kwa kipindi kile nacheza suala la
ushirikina lilikuwa likichukua nafasi kubwa kwa vilabu vikuwa na timu zingine
kuliko sasa,ingawa imani hizo hazina msaada wowote katika soka kwa kuwa mpira
ni mazoezi,kipaji,kumsikiliza mwalimu, mbinu pamoja na pesa.
“Nakumbuka mwaka 1988 nikiwa na
Yanga siku chache kabla ya mchezo wetu wa mwisho na Costal Union ya Tanga
walikuja waganga wapatao 10,Toka mikoa Tofauti kwa ajiri ya kutufanyia dawa ili
kupata ushindi katika mechi yetu na wachezaji wote tulilazimishwa kushiriki
tukio lile kuanzia saa 3 usiku hadi saa 8 usiku lakini licha ya kutumia dawa
zile Tulikung’utwa bao 1-0,na Wagosi wa kaya wakatangazwa kuwa mabingwa wa
Tanzania kwa mara ya kwanza na sisi tukamabulia nafasi ya pili.
“Kikosi cha yanga ambacho kilikosa
ubingwa mara baada ya kutumia Kikombe toka kwa wataalam wa miti shamba ni kama
ifuatavyo Golini nilikuwepo mimi mwenyewe,2 Lawrenc MwaluSako,3 Fred Felix,4
Godwin Aswile,5 Said mwamba6,6 Issa Athuman,7 Abuu Bakari,8 Athuman China,9
Abeid Mziba,10 Edga Fungo na 11 ni Celestin Sikinde ambao walipelekwa puta na
Costal Union mwaka 1988.
Hatasahau
Siwezi kusahu nilipoumia Enka nikiwa
na Yanga mwaka 1989,kati yetu na Reli Moro,ambapo nilitolewa nje dakika ya 20
ya mchezo mara baada ya kuumizwa vibaya na Dankan Butinini,na nafasi yangu ikachuliwa
na mlinda mlando mwezangu Sahau Kambi ambaye naye aliumia kabla ya mchezo
kumalizika na nafsi ikachuliwa na Joseph Fungo ambaye aliimili adi Dakiki 90 ya
mchezo.
“Hiyo katika mchezo ule Yanga
walitumia magolikipa watatu kutokana na sisi kuumia,tukio lile liliniweka nje
ya uwanja kwa kipindi kirefu hadi likatishia uwezo wangu wa kucheza mpira ndani
ya Yanga lakini baadae nikapona Vizuri na kulejea uwanjani.
Kumbukumbu
“Naikumbuka sana mechi yangu ya
kwanza ya kimataifa nikiwa na Tukuyu Stars katika kombe la Afrika mashariki na
kati dhidi Sports Club Vila ya Uganda [nakivugo stadium],mwaka 1987,mechi
ambayo tulitundikwa bao 4-2 kwa kweli ilikuwa mechi ngumu sasa kwetu na mimi
Nilikuwa mechi yangu ya kwanza kuchieza nje ya Tanzania.
“kutokana na ugeni wa mashindano
Tukatolewa katika hatua ya makundi na kurudi nyumbani kwa kuwa katika
mashindano hayo tulifanikiwa kushinda mechi moja pekee zidii ya timu toka
Somalia.
Tofauti TFF-FAT.
“Kwa sasa Tff imejitaidi kututoa
Toka kwenye soka la ubabaishaji na kutuleta kwenye soka la kisasa kwa kuwa
Shirikisho hilo lina kamati mbali mali za kutatua migogoro michezoni Tofauti na
FAT ambayo maamuzi yalikuwa yakichuliwa na watu wachache.
“Kipindi kile wachezaji walikuwa
wanajituma sana ndio maama tulikuwa tunafanya vizuri lakini kwa sasa uongozi
unajitaidi ila Tatizo wachezaji kutokujitoa kwa moyo.
“Na pia ili kukuza na kulifikisha
mbali Soka letu TTF inatakiwa itumie nguvu katka kuhakikisha vilabu vyetu
vianaachana na kumilikiwa na wanachama na badala yake ziendeshwe kwa mfumo wa
Kampuni.
Wachezaji wa kigeni
“Wana umuhimu mkubwa sana kwa kuwa
wanaleta changamoto kwa wachezaji wa ndani,lakini timu zetu zijitaidi kusajili
wachezaji wenye uwezo sio kupoteza pesa kuokota wachezaji wasio na tija ambao
tunaweza kuwapata hapa hapa nchini.
“Nawakubari sana Kipre
Tchetche na Aruna Niyozima,kwa uwezo wao wa kisoka wanajitaidi sana kucheza
kama watanzania wanavyotaka kwa viwango vya wachezaji wa nje.
Wachezaji Anaowakubari
“wachezaji wengi ni wazuri lakini
wafuatao ni zaidi nikiwatenga katika makundi 4,kwa upande wa mlinda mlando
Juma K Juma[Simba] anafunika,beki Kelvin Yondani[Yanga],kiungo Amri
Kiemba [Simba]ni mchezaji wa hali ya juu sasa kwa sasa hapa nchini akifuatiwa
na Abuubakari[Sure Boy] wa Azam FC lakini poul Nonga[Jkt Oljoro]anacheza
vizuri sana katika safu ya ushambuliaji.
Dawa ya Soka la Tanzania
“Ili timu zetu zifanye vizuri ndani
na nje ya Tanzania lazima pawepo na udhamini wa kueleweka kwa kuwa pesa ni
Tatizo kwa timu zetu, walao timu ya kwanza adi ya 9 ziwe na udhamini wa kudumu.
“Pia lazima wachezaji wakae kammbini
muda mrefu na makocha wapewe muda wa kutoisha wa kukaa na wachezaji ili kujenga
timu kwa muda mrefu.
Maisha baada ya soka
“Sasa ivi nimeoa na nina watoto
watatu,japokuwa soka halikunifaidisha kiuchumi zaidi ya kupata sifa na
kufahamiana na watu wengi lakini kazi yangu ya ukocha inanisaidia kuendesha
maisha yangu na naishi vizuri.
“Kwa sasa sijishughulishi na kazi
yeyote zaidi ya ukocha kwa kuwa Kazi hiyo ni ngumu na ukijiusisha na mambo
mengi sni ngumu sana kufanya Vizuri,anaeleza Mbwana Makata ambaye alikuwa
anasumbuliwa vilivyo na Abeid Mzimba wakati alipokuwa mchezaji katika nafasi
yake ya ugolikipa.
Chapisha Maoni