ALEX MAPUNDA MWANDISHI
Mbui Yondani.
Mbui Yondani ni miongoni mwa
washambuliaji wapiga mashuti hatari sana ambao waliwahi tokea hapa nchini na
kamwe hawezi kusahaurika kwa mshabiri na wadau wa soka hapa nchini hasa kwa
Timu ambayo zamani ilikuwa kiboko ya vigogo hapa nchini nazunguzia Reli
Morogoro .
Yondani ambaye ni mzaliwa wa mtaa wa
Kirumba Polisi Jijini Mwanza ambaye ni Baba yake mdogo wa Beki mahili wa
Yanga Kelvin Yondani, alianza kusakata kabumbu wakati akiwa mdogo katika shule
ya Msingi mwenge iliyopo Jijini Humo.
Katika Mazungumzo maalum na Gazeti
hili ameeleza kwa kina kuhusu historia yake ya soka;
“Licha ya kucheza mpira katika
timu ya Uwanja CCM Kirumba pamoja na Basuko,nilianza kucheza soka la ushindani
mwaka 1988 katika timu ya Coop United ambayo ni timu ya watoto wa mjini hapa
Mwanza timu ambayo wamepitia wanasoka wengi wa mkoani Mwanza.
“Mwaka 1989 nilijiunga na Reli ya
Morogoro timu ambayo ilikuwa tishio kwa vigogo hapa nchini nazungumzia Simba na
Yanga,wakati nipo Reli nilipata nafasi ya kuchezea timu ya Taifa kwa mara ya
kwanza mwaka 1992 kutokana na kiwango changu kuwa juu sana kwa kipindi
hicho,nakumbuka tulicheza kwenye michuano ya Challenge ambapo Tanzania
tuliwakilishwa na Kaka Kuona pamoja na Victoria,Hayo ni majina ya timu ya Taifa
Sisi tuliwakilishwa na timu mbili kwa kuwa tulikuwa waandaaji .
“Baada ya kupata nafasi ya kuitumikia
Timu ya Taifa mwaka 1993 nikasajiliwa na Simba ya Jijini Dar Es
Salam,Timu ambayo niliichezea kwa msimu mmoja lakini kutokana na
mizengwe,kocha alikuwa anawapanga wanchezaji kulingana na mapenzi yake hata
kama wewe ni mzuri,Na ni ukweli usiopingika kipindi kile nilikuwa
mchezaji wa kiwango cha juu sana,
“Baada ya kuona kwamba Simba naweza
nikaua kiwango changu mwaka 1994 nikatimukia Milambo ya Tabora,lakini
kutokana na maisha magumu ya huko Tabora,Timu yangu ya Zamani Reli ya Morogoro
wakaamua kunirudisha, hapo nilicheza kwa miaka miwili 1996 hadi 1998.
“Mwaka 1998 hapo nilifikia juu ya
kustaafu soka na kuangaika kuhusu
maisha yangu kwa kuwa kwa kipindi chote hicho sikuwa vizuri kiuchumi, nikaacha
kucheza Soka la ushindani nikachezea Mwanza Veterani Pamoja na Pamba ya mwanza
ambapo Mwaka 2002 nikaacha kabisa kujihusisha na Mambo ya soka hapo ndipo
nikatundika Daruga Rasmi.
Nakumbuka.
“mwaka 1990 wakati nipo Reli ya
Morogoro tulicheza na Timu ya soka ya Maji Maji ya Songea,katika pambano hilo ambalo
lilikuwa kali sana kutokana na Maji Maji kuwa na kikosi imara hadi kipindi cha
kwanza kilipomalizika nakumbuka tulifungana bao 1-1,
“Kipindi cha pili mchezo ulianza kwa
kasi sana ambapo dakika za mwisho nilipokea Pasi safi nje ya 18 na bila kufanya
ajizi nilifumua Shuti kali ambalo lilipeleke mlinda mlango wa Maji Maji
kuchanika mikono na kuachia mpira ukaingia Wavuni.
“Mimi mwenyewe nilishangaa sana
tukio lile mara baada ya kumkuta bwana Shaib Kambanga Disko usiku baada ya
mechi akiwa amefungwa bendeji,nikampa pole na akanieleza kuwa hakuwai pata
mkwaju kama ule,tukaendelea kuburudika.
“Nakikumbuka kikosi cha Reli ambacho
kilikuwa kiboko ya Vigogo na Timu zingine hapa nchini,ambacho akitakuja
sahaurika hapa nchini ambapo langoni alikuwepo Athumani Msumari,safu ya ulinzi
iliimalishwa na James Charles[marehemu],Abdallah
Mkali[marehemu],Gasper Lupindo[marehemu] pamoja na Fikiri Magoso. Viungo
alikuwepo Mtwah Kiwelu,Boniface Njohore pamoja na Dankani Butinini huku safu ya
ushambuliaji ikiongozwa na mimi mwenyewe Mbui Yondani,Msafiri Khamis Bila
kumsahau Living Stone.
Hawaezi kusahau
“Mwaka 1991 mechi ya ligi kuu kati
ya Reli na Bandari ya Mtwara mimi na beki wa Bandari tuliruka juu kuuania mpira
mara baada ya kuingizwa majaro zuri toka winga ya kulia bahati mbaya tukaukosa
mpira na tukagongana Vichwa na tukadondoka vibaya sana.
“Katika tukio lile mwenzangu alipata
fahamu baada ya siku ya Tatu,mimi japokuwa nilirudi uwanjani kuendelea na
mchezo usiku uliofuata sikupata usingizi nilipata maumivu ambayo sikuwai
kuyapta tangu nilipozaliwa kwa Baba na Mama, ambapo baada ya siku chache
niliendelea na mchezo.
Ushirikina
“Upo hasa kwa virabu vikubwa Simba
na Yanga mara nyingi hasa katika mechi za watani wa jadi lakini kwa timu zingine
kama Reli sikushuhudia suala lolote la ushirikina tulikuwa tunafanya mazoezi na
kumtegemea mungu.
“Siamini hata kido imani hizo sio
kweli ,wakati nipo Simba kuna mambo mengi yalikuwa yanafanyika wakati wa
mchezo lakini tulikuwa tukichezea kichapo kama kawaida.
Simba walinibebesha Gunia la
Misumari.
“Mwaka 1993 wakati nikiwa
Simba,nilikosa bao la wazi wakati zikiwa zimesalia dakika 3 mpira
kumalizika,katika kombe la Caf kwa sasa shirikisho,kati ya Simba na Timu Toka
Msumbiji,nakumbuka ilikuwa CCM Kirumba Mwanza mchezo ambao ulimalizika kwa sare
ya bila kufungana.
“Baada ya mechi ile sikuwa na
amani,wenye timu walinitazana kwa jicho baya huku wakinituhumu kuwa mimi
ni mpenzi wa Yanga na kwamakusudi nikaamua kuwakosesha Simba ushindi kiukweli
iliniuma sana.
“Basi kutokana na tuuma ile na licha
ya kwamba kiwango changu kilikuwa kikubwa masikini ya mungu sikupewa nafasi
hata ya kusafiri na timu kwenda nchini Msumbiji katika mechi ya marudiano
waliniacha Bongo.
“Kuanzi hapo nilichukiwa sana hadi
nikahasirika kisaikorojia lakini ukweli
ni kwamba mimi sikuwa na mapenzi na Yanga na kukosa Bao ni suala la kawaidi kwa
mchezaji sio makusudi.
Waamzi.
“Viwango vyao vipo chini sana
hawjiamini pindi wawapo uwanjani kutokana na kupokea Takrima toka pande
mbili hali hiyo inapelekea wachezaji kuchezeana rafu mbaya na mwamzi anajifanya
haoni.
“Mfano kuna tukio lilitokea Hivi
karibuni la Haruna Moshi Boban kumchezea Rafu mbaya Kelvin Yondani
[Yanga]mwamzi badala ya kutoa kadi nyekundu akatoa kadi ya njano huu ni uzembe
mkubwa kwa waamzi wetu lazima wabadilike.
Katiba.
“TFF lazima wafanyie mabadiliko ya
katiba ya soka hapa nchini hasa kipengere cha uchaguzi badala ya wanachama
wachache kumchagua kiongozi wa chama wa ngazi ya chini au ya juu badala yake
achaguliwe na umaa, ili kuepuka tatizo la watu wachache wenye pesa wasiojua
mpira kuchukua madaraka kwa kuwaonga wapiga kura.
“Kuna kipindi nilijisikia aibu sana
wakati nilipoenguliwa mwaka 2005 katika nafasi ya ujumbe Ilemela na wakampa mtu
kutokana na vijiela vyake ambaye hajue chochote kuhusu mpira kunishinda mimi.
Wachezaji anaowakubali
“Namkubali sana Haruna Niyonzima
kiungo wa Dar Es Salam Yang Afrika yupo Vizuri kwa ukanda huu wa afrika
mashariki na kati, lakini sio kwamba napendelea ni ukweli wenyewe Mtoto wa kaka
yangu Kelvini Yondan Anafanya vizuri katika nafasi ya Ulinzi kwa hivi sasa hapa
nchini.
Kipa Msumbufu.
“Mwameja huyu ni balaa mimi nadiriki
kusema kuwa hakuna mlinda mlango ambaye hadi hii leo amefikia uwezo wa Mwameja.
“Mimi alikuwa akinisumbua sana
hakiri,mara nyingi mazoezini alikuwa anawaita na kuwawekea mpira eneo la
penalti na kuwaambia atakayefunga penalti tano nampa fedha,lakini matokeo yake
unaishia tatu au mbili,mimi sikuwai shuhudia Mwameja akifungwa Penalti 5.
Ushauri kwa Timu ya Taifa.
“Hata ashuke Yesu, kwa mfumo
wanaoutumia Taifa Stars na haina ya wachezaji walionao kushiriki kombe la dunia
ni ndoto,lazima yafanyike mabadiliko makubwa sana ili kunusuru soka letu.
“Mimi kipindi nacheza nilikuwa na
nguvu sana hizo nguvu za Thomas Ulimwengu ambaye ni nchezaji mwenye nguvu kwa
kipindi hiki hata robo kwangu hatii ndani,wachezaji wa kipindi chetu
walikuwa na vitu vingi sana ni mchezaji gani? Wa sasa ivi ana uwezo wa
kumwamisha beki kwenye Reli na kupasia wavu,hakuna.
“wachezaji wenye vipaji vya
kweli tunawacha na badala yake tunawakumbatia wachezaji wasio na akiri ya
uwanjani,Tff wanakijua cha kufanya.
Baada ya kustaafu.
“Kwa sasa nina miaka 47 hadi 2013,nina
mke na watoto wawili ,najisughulisha na ufugaji wa ng’ombe wa Maziwa pamoja
udalali wa kutafuta Bidhaa Mbali mbali Zinazopatikana hapa Mwanza kwenda
Dar na mke wangu ajishughulisha na ufugaji wa Kuku wa kisasa maisha yetu
Sio mabaya.
“kwa kweli sikunufaika na mpira
kiuchumi ila kuwa maarufu na kufahamiana na watu imenisaidia sana kufanya
shughuli zangu kwa uraisi,Anahitimisha Yondani ambaye ametokea katika ukoo wa
wachezaji wa ukweli wa soka na watoto wake muda wote anawahamasisha kuhusu
mpira,na wanacheza vizuri.
Chapisha Maoni