Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.






Sophia Mwaipyana





ALLY Said Jobbe  maarufu kwa jina la Jobbe  ni kocha ambaye aliinoa timu ya Mecco  ambayo ilifanya vizuri sana   kuanzia  miaka ya 1989.
Jobe alizaliwa miaka 59 iliyo pita mjini Kahama ingawaje  asili yake ni Bagamoyo mkoani Pwani,alianza maisha ya  soka toka akiwa shule ya msingi Uhuru mchanaga nyiko na baadae kajiunga na shule ya sekondari Uyuwi  iliyopo mkoani Tabora.
Lakini alikatishwa na maisha ya kucheza soka baada ya mwaka 1971 kupata ajali Mbaya akiwa  katika timu ya Gmal Fc iliyo kuwa mkoani Shinyanga baada ya kuanguka na kuangukia mkono hali iliyo sababisha mkono kuvunjika na toka siku hiyo aliacha kucheza mpira  na badara yake akaanzisha timu yake.
“mwaka huo huo nikarudi dar es salaam nikaanzisha timu ilikuwa inaitwa O.A.U  tulikuwa tukifanyanyia mazoezi maeneo ya Tandika,mwaka 1978 nikawa mwalimu wa timu ya Tazara Combine napo sikudumu sana nikaenda zangu Zambia katika  katika chuo cha Tazara kinaitwa Mpika sikukaa sana kama miezi miwili tuu”
“nika hamishiwa Tazara Mbeya   nikiwa kama mwendesha mitambo hapo tazara nikaanzisha shule ya mpira iliyo itwa Iyunga Charld mwaka 1979 hadi 1986 huku nikifundisha timu ya Zovwe Fc.
“ na mwaka huo huo  nikafatwa na uongozi wa Mecco ambao waliniambia niache kazi Tazara na nikaajiliwe katika kampuni yao ambao walikuwa wakijenga ambacho kwa sasa ni Must”
“kweli niliacha kazi Tazara na nikaenda kuwa mwalimu wa timu ya mecco huku nikiwa  mfanyakazi wa Mecco katika kitengo cha ufundi magari na mwendesha mitambo”
“kweli mwaka ulio fuata 1987 tukaianzisha timu ila niliianzisha katika mazingira magumu sana kwani niliambiwa wachezaji wote wawe wafanyakazi wa mecco tu kwahiyo tulianza kama timu birudani tuu kwa wafanyakazi”
“lakini baada ya kuwa timu nzuri tukashiriki katika ligi ya wilaya ,mkoa ,kanda hadi ligi kuu hapo uwongozi ulikubari  tutafute wachezaji kutoka maeneo mbalimbali”
“tukiwa makocha wawili mimi na Mafta Isa lakini cha ajabu tulifumbwa hakuna aliye juwa kuwa yeye ndiye kocha mkubwa na nani kocha msaidizi lakini tulifanya kazi na timu ikafanya vizuri”
“mwaka 1991 nilihama Mecco na kwenda Tiger Fc iliyo kuwa Tunduma lakini sikukaa nazani hata mwaka sikumaliza wachezaji wakawa wanataka kufanya wao wanavyo taka siyo nitakavyo mimi”
“yani wachezaji walio anzisha klabu huwa wanamatatizo sana  huwa wanataka wafanye wao wanavyo taka na uwongozi ulikuwa unawasikiliza sana,unakuta wanataka umpange hata kama hajaja kufanya mazoezi kwahiyo nikaona kazi itakuwa ngumu nikaachana nao”
“mwaka 1992 nikaitwa na mkuu wa wilaya ya Tunduru nikaja kuifundisha timu ya  halmashauli ya Tunduru ambayo inaitwa Kurugenzi Fc ,nikaanzisha na timu yangu inaitwa Jobe Kids kwasasa imekuwa na inashiriki ligi daraja la pili ngazi ya Kanda ila kwasasa inaitwa Small Boys ni timu inayo fanya vizuri huku kwetu “
Wachezaji gani ni matunda yako.
“kwawachezaji wa sasa ni huyu mtoto aliyeenda Mbeya City Peter Mapunda  Yule nimemkuza mimi kisoka ,ila kwa wachezaji wa zamani kuna huyu Abdal Mwinyimkuu ,hawa wakina kiweru mmoja wao nimemfundisha ,Charles Makwaza ,Buchumi,Dennis Mrowe na wengine siwakumbuki”
Nini ilikuwa siri ya Mecco kufanya vizuri
“nilikuwa na wachezaji ambao walikuwa hawaogopi mazoezi,yani wachezaji wenye moyo wa uzarendo walikuwa tayari kuipigania timu yao,uongozi mzuri na bila kuwasahau wazee wa mkoa wa Mbeya wakina Mwaijumba walikuwa wakitupa sapoti sana kwahiyo ushirikiano ndani ya timu tayari ni ushindi tosha ndiyo maana tulifanya vizuri”

Tofauti wa chezaji wa sasa na  zamani
“wachezaji wa sasa utandawazi umewaharibu kwani unakuta mchezaji unamfundisha anaona kama unamdanganya kwasababu kaona wachezaji wa Nchi za wenzetu wanavyo fundishwa kwahiyo nae anataka afundishwe kama wao “
“kitu ambacho hakiwezekani kabisa kwani wenzetu teknolojia yao ni kubwa huwezi kulinganisha na huku kwetu,lakini wachezaji wa zamani kwanza walikuwa tayari kupokea mafunzo toka kwa mwalimu na walikuwa wanakushauli kuwa mwalimu ukitufanyia hivi tutafanya vizuri na walikuwa na uchungu na timu zao”
“lakini wachezaji wa sasa unaona kabisa mchezaji yupo tayali kwa matokeo yoyote yale afungwe ashinde yeye yote sawa kwasababu wame weka pesa mbele kuliko mafanikio ya timu “
Nini ugumu wa kazi ya ukocha
“kwangu mimi huwa inaniwia vigumu sana pale unamfundisha mchezaji  jinsi ya kucheza  na sheria kabisa za mpira lakini kesho  unakuta mchezaji anacheza anavyo taka yeye na anavunja sheria unakuta anapewa kadi nyekundu anacheka  wala haoni kama anamuumiza mwalimu wake yani wachezaji wakati mwingine wanakuwa hawako siriasi na kazi yao”
  
Vipi swara la ushirikina katika soka
“ hahaha umenikumbusha mbali mwanangu  ingawaje uchawi wa soka ni mazoezi tuu hakuna kitu cha ziada ila sasa soka letu sisi waswahili tumetawaliwa na imani sana za kishirikina tukiamini bila uchawi hatuwezi kushinda”
“Yani mganga  anauwa soka sana kwani unakuta mchezaji anaenda kwa mganga anampa rushwa anamwambia mganga mimi mwalimu hawezi kunipanga katika mechi ya kesho kwahiyo mganga  anakuja kwa mwalimu anaangalia majina ya wachezaji waliopangwa “
“akikuta jina la yule mchezaji halipo utasikia mwalimu hapa  usipo mpanga mtu Fulani lazima mnafungwa mimi nilivyo lala nimeota hivyo kwahiyo lazima  umpange ,na huwezi kusoma majina ya wachezaji wanao takiwa kuingia uwanjani bila mganga kuyabariki  au a kanuiza maneno yake”
“lakini kwangu ilikuwa tofauti  ilikuwa mganga akininga’nganiza kumpanga mchezaji nilikuwa na mwingiza ila hachezi kwa mda mrefu namtoa kwani unakuta mwingine hana uwezo lakini mganga kasema apangwe”
“yani waganga wanakula sana pesa za timu unakuta pesa anayo pewa mganga timu ikishinda ni zaidi  ya mshahara wa mwalimu aliye ifanya timu hiyo ishinde ambaye anafanya kazi kubwa kuwafundisha wachezaji”
“nilisha shuhudia mganga akipewa milioni tatu kama asante kwa kutufanya tushinde hapo bado malipo mengine roho iliniuma sana kwani ukiangalia  mimi niliye wafundisha vijana napewa mshahara kidogo sana  roho iliniuma sana kiukweli”
Tukio usilo lisahau
“nipale nilipo achishwa kazi Tiger kisa sikumchezesha  mchezaji wao wanao mtaka wao,tulikuwa hapo Vwawa mchezaji huyo alikuja wakati  wenzake wamesha pangwa bado dakika kidogo tuu mpira uwanze “
“wakaja kuniambia ni mpange basi mimi nilikataa basi wakamjaza maneno kuwa  mwalimu ndiye alikuzibia ila sisi uwongozi hatuna matatizo na wewe na ukiangalia Yule mchezaji ndiyo walikuwa wameianzisha timu hiyo na alikuwa akisikilizwa sana”
“kwahiyo kesho yake kiliitishwa kikao na nikapewa  kilicho changu na kuambiwa niondoke muda huo huo ilikuwa kama saa saba mchana sikuwa na jinsi ikabidi niondoke”
Mafanikio uliyo yapata kupitia soka
“kwanza ni kujulikana na watu wengi ,pia nimepata kazi sehemu mbali mbali kwa ajili ya mpira kwani hapa Tunduru  nafanyia katika halmashauli na nilikuja huku kwa sababu ya  kuifundisha timu na nikapewa na ajira”
Timu gani ilikuwa inakupa hofu ikiwa inakutana na timu yako
“nitimu mbili ambazo zilikuwa zinanitoa jasho na hofu kubwa kila nikikutananazo ni timu ya African Sport ya Tanga na Pamba ya Mwanza  kwani wachezaji wangu walikuwa wakishindwa kabisa kuwakabiri mabeki wa timu hizi”
“yani iwe nyumbani au ugenini hatujawai wafunga siku zote tulitoka droo kila tunapo kutana kiukweli timu hizo nilikuwa naziogopa sana kwani chochote kiliweza kutokea  kutokana  na ubora wa timu hizo”
Kwanini mecco haikudumu
“timu ile ilianza kupoteza mwelekeo walipo ifanya timu ya shirika la Mecco na siyo tena kuongozwa na uongozi wa Must kwahiyo walengwa wote wakawa hawasikirizwi na wachezaji wakahama”
Mchezaji gani unaye mpenda Tanzania
“nampenda sana Bobani  nimchezaji mzuri ingawaje anavituko vyake lakini akiamua kucheza mpira anacheza vizuri sana”
“kwa wachezaji wa zamani  ni timu yangu yotr ya Mecco  kama Buchumi,Charles Makwaza na Nasibu Abasi kwa sasa ni marehe, na wengine wote ambao sijawataja ila nilikuwa nao Mecco”
Ushauri wako kwa makocha wenzio
“kwanza nikwa viongozi wetu wa chama cha makocha  wawe wanatutembelea hadi huku  siyo wanaishia  dar ,morogoro wajitahidi kutembea Nchi nzima kutupa elimu ili tuweze kuwanoa vijana wetu kwani huku kunavipaji vingi ila makocha ndiyo tatizo kubwa”
Familia
“nina watoto 15 ila kwa sasa wamebaki  kumi na ninawake watatu kwahiyo familia yangu moja ipo hapa Tunduru,Mbeya na Bagamoyo,kati ya hawa alikuwepo mtoto mmoja aliye rithi kipaji changu lakini hakukiendeleza kwani alienda jeshini  na sasa ni kapteni huko Nairobi anaitwa Jobbe,ila huyu msicha wa mwisho anaitwa Rahima anacheza sana mpira wa pete anasoma  makata sekondari”
Unategemea kustafu
“hapana sijui tastafu lini kwasababu bado nina kiu ya kuona vijana wenye vipaji nawafundisha nandiyo maana nikistafu mwakani kazi nitaanzisha Academy niendeleze kuinua vipaji vya wachezaji huku Tunduru lakini kwa sasa  nina timu yangu inaitwa Jobbe Fc”
Mwisho


Chapisha Maoni