|
||||
Ali yusuph Suleiman ‘Tigana’
kwa wadau na mashabiki wa soka hapa
nchini hasa kwa wale wenye miaka kuanzia 25 na kuendelea ukipita katika kijiwe
chochote na gafla ukasikia jina la ALI Yusuph Suleiman maarufu kama ‘Tigana’
likitajwa na usimkumbuke! wakati ni shabiki wa ukweli wa soka,hakika itabidi
ufanyiwe uchunguzi wa akili kwa kuwa tutakuwa na wasi wasi juu ya uwezo wako wa
kufikiri,kutokana na uwezo mkubwa ambao Tigana alikuwa nao pindi alipokuwa
akisakata gozi la ng’ombe hapa nchini.
Tigana mzaliwa wa Ilala mpakani mwa
mtaa wa Sadani na Newala, jijini Dar es salam alianza kusakata kandanda mwaka
1880 mwaka ambao Tanzania ilipata nafsi ya kushiriki kwa mara ya kwanza na
mwisho michuano ya mataifa ya afrika nchini Nigeria katika shule ya msingi uhuru
changaiko na nyota yake ikang’aa Zaidi katika timu ya vijana ya shauri moyo
kids pamoja na Nambanga Fc, katika mzungumzo na gazeti hili anafafanua mengi
kuhusu maisha yake ya soka:-
“Nilianza kucheza soka la ushindani
katika timu ya Manyema Fc mwaka 1990 timu ambayo ilikuwa ikishiriki ligi daraja
la Tatu katika nafasi ya kiungo mshambuliaji ambapo baada ya kuonyesha uwezo
mkubwa nyota nyekundu na Pan Afrika waliingia kwenye kinyang’anyiro cha
kunisajili ambapo mwaka 1992 nikatua Pan Afrika timu ambayo nilichezea
kwa misimu miwili na hatimaye mwaka 1994 nikajiunga na Yanga Africans, kwa
kipindi hicho nilikuwa na uwezo mkubwa sana wa kucheza mpira.
“Umahili wangu na umakini hasa
wakati wa kufunga pindi nikutanapo na timu pinzani uliwafanya simba wanitafute
kama chakula pindi mtu awapo na njaa toka nilipokuwa Pan na walifanikiwa
kuinasa saini yangu mwaka 1996 baada ya kuniwinda kwa kitambo kirefu na
nilifanikiwa kuwatumikia wekundu wa msimbazi hadi mwaka 1998 hapo nilipata
nafsi ya kwenda nchini Malaysia.
“Dili la kucheza mpira katika timu
ya Malaysia mimi pamoja na mwanamtwa Kiwelo tulifanyiwa na moja ya
viongozi ndani ya simba na tulicheza kule hadi mwaka 2001 hapo nikarudi
tena Simba,wakati narudi simba maelewano kati yangu na viongozi yalikuwa yameyumba
kwa kuwa kipindi tupo Malaysia tulizurumiwa sana na baadhi ya viongizi ambao
walitupeleka kule,na dili la kwenda kule pesa zote walichukua huku tukilipwa
mishaara ambayo haikufanana na uwezo wetu wa kusakata kandanda,kuna kipindi
tuligoma kucheza adi walikuja viongozi wa simba kusuluhisha mgogoro ambapo mimi
sikutaka kubaki kule lakini ilitulazimu kubaki kwa vile hati za kusafiria
walikuwa nazo wao ikatulazimu kuendelea kucheza kinyonge.
“kiukweli Malaysia sisi tulitoa
msaada mkubwa sana kwa timu yao ambapo kabla ya kutusajili sisi timu hiyo
ilikaa bila kombe kwa takribani miaka 20 lakini baada ya kutua sisi tukachukua
ubingwa wa nchi hiyo,baada ya kurudi simba uhusiano wangu na viongozi uliyumba
kutakana na matatizo ya fedha ya dili la Malaysia hivyo nikacheza kwa msimu
mmoja na baadae nikatimukia yanga na nikaitumikia timu hiyo toka 2002 adi 2003
apo nikarudi katika timu ya mtaani kwangu Ilala Fc kipindi hicho ilikuwa
imepanda ligi kuu nayo nikaitumikia kwa msimu mmoja na 2004 nikaenda kucheza
soka la kulipwa uarabuni katika nchi ya Omani.
“Omani sikukaa sana kwa kuwa
nilipewa mkataba wa mwaka mmoja ambapo ulipoisha mkataba nikarudi Bongo na
mwaka 2005 nilijiunga na Timu ya Moro United maarufu kama chelsea ya bongo
kipindi hicho moro walifanikiwa kushika nafsi ya pili katika ligi kuu ya
Tanzania na kuwakirisha Tanzania katika michuano ya kimataifa.
“nikiwa na moro United tulifanikiwa
kucheza vizuri katika mechi za hawali katika kombe la shirikisho lakini
kutokana na kuwepo kwa wachezaji wachache wazoefu katika kikosi chetu
tulitolewa na timu ngumu ya Etoile du Sahel ya Tunisia kwa Jumla ya bao 6-1
ambapo kwao walituchabanga bao 4-1 huku nyumbani wakitushindilia bao 2 mtungi
na tukaaga mashindano.
“mwaka 2008 niliamua kutimkia nchini
Afrika kusini mara baada ya timu hiyo kukumbwa na ukata mkubwa ambapo Tajiri
aliyekuwa akishikiria timu hiyo alijitoa kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi na
wachezaji wengi nyota tuliamua kuondoka, nikiwa Nchini Afrika ya kusini
nilisota sana kutafuta timu ya kuchezea kwa kuwa mfumo wa kujiunga na timu za
nchini humo ni sawa na Barani Ulaya ambapo ili timu ikuchukue lazima uende na
meneja.
“Mimi nilijaribu bahati yangu katika
timu ya Mamelodi sundowns pamoja na Santos lakini niligonga mwamba kwa kuwa
sikuenda na Meneja,katika Timu ya Santos wakati nilipoenda kufanya maojiano na
viongozi wa timu hiyo nilitanguzana na mdogo wangu wakaniuliza huyu ni Meneja?
Nikakataa kwa kweli sikuweza kupata msaada ingawa nilichezea timu hiyo kwa
kipindi Fulani.
“Baada ya dili la kucheza mpira
Afrika kusini kukwama mnamo 2008 mwishoni nilikwea pipa kuelekea bongo kutokana
na kusota nchini Afrika Kusini kwa muda mrefu bila kupata mkataba licha ya
kiwango changu kuwa juu, niliamua kuachana kabisa na soka,anasimulia Ali Yusuph
Tigana kisha Anaendelea:-
Mvi Bukoba iliambatana na majonzi
ndani ya Simba.
“siku ya Tukio la kuzama kwa meli ya
Mvi Bukoba kila nikikumbuka napatwa na simazi kubwa sana kwa kuwa tukio lile
liliambatana na matukio mengine mawili kwangu,kwanza siku hiyo simba tulitoka kupoteza
mchezo wa kimataifa dhidi ya Arab Contractor katika Mjini Alexandria nchini
Misri,ambapo mchezo wa kwanza walitufunga nyumbani jijini Dar es salam kwa
jumla ya bao 3-1, ambapo misri tulitoka sare ya bao 2-2 tukaaga mashindano.
“baada ya mchezo mishare ya jioni
tulipata taarifa kupitia kwa shirika la habari la kimataifa,CNN kwamba Meli ya
Mv Bukoba imezama na watanzania wengi wamepoteza maisha kiukweli majonzi
yaliongezeka mara dufu kwa kuwa tayari tulikuwa na machungu ya kuaga mashindano
hapo tukapeana taarifa huku tukijiandaa kurudi Tanzania.
“hiyo ni 9 kakini 10 wakati
tuliposhuka uwanja wa ndege jiji Dar es salam hapo tulinyong’onyea kabisa kwa
kuwa tulipokea Taarifa ya kwamba mchezaji wa Mahili wa Soka Ramadhani Lemi
alikuwa amefariki dunia’anavuta pumzi kwa majonzi kutokana na kukumbuka
jinsi ilivyokuwa’kisha anaendelea kusimulia; kiukweli majonzi ambayo
tulikuwa nayo ni makubwa sana basi moja kwa moja tukaenda kwenye mazishi ya
mchezaji mwenzetu,mungu awaweke mahali pema peponi na wale wote ambao
walipoteza maisha.
Nilikimbia na laki moja ya Dewji.
“wakati nipo Pan Afrika kuna kipindi
tulicheza mechi ya kirafiki na wekundu wa msimbazi Simba,mchezo ambao nilicheza
kwa kiwango cha hali ya juu sana hali ambayo ilipelekea viongozi wengi wa simba
kunimezea mate ambapo baada ya mchezo ule, aliekuwa mdhanini wa simba Azim
Dewji aliwatuma watu wake kunitafuta ambapo walikuja hadi nyumbani na
wakanichukua na kunipeka ofisini kwake.
“siku ya kwanza kuingia ofisini kwa
Dewji niliogopa sana kwa kuwa sikuwai fikilia kama kuna siku nitafanikiwa
kuingia ofisini kwake kwa kuwa Dewji alikuwa Tajiri mkubwa,baada ya kuingia
ofisini kwake alinipokea vinzuri na akaniambia kuwa ameridhika na uwezo wangu
wa uwanjani na alinitaka kusaini Simba,nilijifikiria sana kabla ya kumjibu kwa
kuwa Pan Afrika walikuwa wamenifadhili mambo mengi sana hivyo nilifikiria juu
ya kusaini simba bila kuwalipa fadhira zao,kwa woga nilimkubalia dili la
kusaini Simba.
“basi Dewji akanipa kitita cha
shiringi laki moja pia akiniambia kuwa anasafari ya kwenda uingereza
hivyo akirudi tutakamilisha kila kitu,kiukweli moyoni nilikuwa njia panda
na uamzi ambao nilipanga kuuchukua baada ya kufikiria kwa kina ni kuchezea Pan
Africa kwa kuwa tayari nilikuwa na mkataba nao.
“Dewji baada ya kutoka Uingereza
alinitafuta sana ili kusaini mkataba Simba kwa kipindi hicho aliwatuma watu
wake lakini nilikuwa nikiwapiga chenga kwa kuwa kipindi kile mawasiliano
yalikuwa magumu nilifanikiwa adi msimu uliponza nikavaa uzi wa Pan Afrika.
Ushirikina.
“ulikuwepo,upo na utaendelea kuwepo
kama timu zetu hazitaamua kuchana na Imani hizo hasa hapa nchini,baadhi ya timu
zetu suala la kutumia madawa siku za mechi ni ishu ya kawaida sana,Mimi binafsi
siamini Imani hizo kwa kuwa mpira ni Mazoezi nchi zote ambazo nimeinda kusakata
kandanda la kuripwa Imani hizo hakuna wao ni mazoezi pamoja na mbinu za kocha.
Mechi kali.
“moja ya mechi ambayo naikumbuka
katika michezo yote ambayo nimewai cheza katika maisha yangu ya soka ni mchezo
kati ya Yanga na Timu ya Bulawayo Ilenders ya nchini Zimbabwe katika klabu
bingwa Afrika,mechi ya kwanza ilifanyika Jijini Dar esalam ambapo mchezo
ulimalizika kwa sare ya bao 2-2 matokeo ambayo yaliwakatisha tamaa viongozi
wengi wa Yanga kwa kuwa ilitakiwa kwenda nyumbani kwao.
“safari ya kwenda katika mchezo wa
Marudiano viongozi wengi wa yanga waligoma kwenda meneja pekee alikubari
kusafiri na timu hadi Bulawayo,ambapo siku ya mechi mashabiki wa Ilenders
walitupa presha sana ambapo kila mmoja wao alikuwa ameshika bango ambalo
lilisomeka 5-0 na uwanja wa Bulawyo ni mkubwa sana na siku hiyo ulitapika,basi
mimi sikuwakawiza kipindi cha kwanza nikawapiga bao,uwanja wote ulikuwa kimya
hapo ndipo tukapata nafasi ya kucheza kwa Amani.
“kipindi cha pili Said maurid SMG
aliwakimbiza na akawatundika bao la pili bao ambalo liliwachanganya sana
mashabiki wao na ikaperekea wachezaji wao wacheze kwa presha kubwa,dakika za
mwisho tulipata penalty ambayo ilizua vurugu kwa mashabiki adi ilipelekea mpira
kumalizika bila sisi kupiga penalty ile,mashabiki walikuwa wakirusha chupa
ngumu uwanjani kiasi kwamba ilikuwa kila tukisogea kupiga penalty walizidi
kurusha chupa nyingi Zaidi ambapo mwamzi bada ya kuona hali tete Zaidi akamua
kumaliza mpira.
“kingine ambacho kilitokea baada ya
kumalizika ule mchezo mashabiki walituzuia kutoka dimbani ilikuwa kila tukitoka
wanarusha chupa na kitu ambacho tulikifanya tulichukua makoti yetu na kuweka
kichwani huku tukitimua mbio kuelekea katika chumba cha kubadilishia
nguo,nakumbuka siku ile tulipigwa sana chupa za mgongoni na mashabiki.
“baada ya mchezo huo nakumbuka
tulipangiwa na Mamelodi sundowns toka nchini Afrika ya kusini ambapo katika
mchezo huo mimi na Said mwamba tulifungiwa kwa madai ya utomvu wa nidhamu basi
yanga ikapoteza mbele ya waafrika kusini na ikaaga mashingano.
Kituko
“ilikuwa kali ya mwaka wakati wa
mchezo wetu na timu toka Bulawayo kipindi cha pili kipa wetu Doe mokey
kuna kitu alikisema adi leo bao sijaelewa kama alikuwa akitutania au
kweli,Mokey alituita na kutuambia kuwa mimi naacha kusimama langoni kwa kuwa
goli naliona kubwa sana kuliko la kule wachezaji wote tuliduwaa kwa kuwa
aliongea huku akitukazia macho,wezangu wakamjibu wewe usitutanie mbona mwenzako
amesimama hapo hapo hakulalamika?akaendelea kusisitinza kuwa hawezi kusismama
langoni,baada ya kumsii kwa muda allikubari kuendelea na mchezo,lakini kusema
kweli siku ile alisurubiwa sana langoni kwa kuwa aliokoa michomo ya hatari sana
adi kuna kipindi alilalamika vidole vilikuwa vikimuuma.
Daraja la tatu la zamani sawa na ligi
kuu ya sasa.
“kwa wachezaji ambao wamecheza mpira
miaka ya 1980 adi 1990 watakubaliana na mimi kuwa ligi kuu ya sasa ni
sawa na ligi daraja la tatu kipindi kile kwa kuwa kipindi kile mpira
ulikuwa na ushindani wa hali ya juu sana,timu ya ligi daraja la tatu kipindi
kile ikikutana na timu ya ligi kuu kwa sasa hakuna utofauti, vijana wasasa
wanashiriki mambo mengi yasiyokuwa ya lazima badala ya ucheza mpira.
Yanga walipotezea dili langu la
Ulaya.
“wakati wa nchezo wetu kule Bulawayo
kuna waarabu walikuja pale kwa ajili ya kusaka wachezaji,na baada ya kutuona
sisi walilidhika na kiwango chetu na waliwaita vingozi wa yanga na wakafikiana
juu ya sisi kwenda Ulaya katika kisiwa cha Spuras ili kufanya majalibio,baadae
nilitofautiana kidogo na uongozi wa timu hiyo hadi wakanifungia wakidai
kuwa nilikuwa na utomvu wa nidhamu wakapotezea dili langu la kwenda Ulaya mimi
hata sikuuliza.
“Mimi nadhani kucheza kwangu simba
ilikuwa tatizo kwa Yanga kwa kuwa kipindi hicho pambano kati yetu na simba
lilikuwa limekaribia, mimi na mwenzangu walitutuhumu kuwa tumepokea pesa
Simba ili kufungisha Timu kitu ambacho mimi nilikishangaa sasa na wala sikuwai
fanya ,na kwa bahati mbaya Simba walitufunga Bao 1-0.
Kutokea kwa ‘Tigana’
“wakati nilipokuwa Mdogo watu
walikuwa wakiniita Ali Kanada kwa kuwa nilikuwa nikivaa Tsherti ambayo
iliandikwa ‘Kanada’ mara kwa mara hasa pindi nilipokuwa nikicheza mpira
katika timu yangu ya Utotoni ya Shauri Moja Kids,lakini baada yakiwango changu
kukua na kufanya vizuri watu wengi wakaanza kuniita jina la Tigana jina ambalo
nililichukia sana kwa kuwa sikuelewa maana yake.
“na kadili nilivyokuwa nikilichukia
na watu walizidi kuniita baada ya kuona kero nilimfuata mwalimu wetu wa timu na
kumwambia kuhusu jina lile yeye alicheka sana alafu akaniambia kuwa jina la
Tigana lina maana na akaniahidi kuwa tutaangalia mkanda ili kujua kuhusu jina
hilo.
“Basi mwalimu aliniita pamoja na
wezake akatuwashia mkanda kati ya Blazil na Ufaransa ilikuwa ni mechi ambayo
ilichezwa miaka ya 70,ilikuwa ni mechi zuli sana na kocha akanionyesha kiungo
wa ufaransa ambaye alikuwa akifahamika kwa jina la Jean Tigana kiukweli
alikuwa mchezaji mzuri sana mimi awali sikuwai sikia kuhusu mchezaji huyo
ambaye alikuwa mwembamba na sifa kama za mimi.
“Basi kuanzia siku ile nikawa
nafanya mazoezi mara kwa mara na kusikiliza mafunzo ya kocha huku nikifuata
nyayo zake na nilikuwa nikisikia jina hilo nilikuwa nafurahi sana kwa kuwa
walikuwa wakinifananisha na yeye.
Red Stars walinizuia kucheza msimu
mzima.
“mwaka 1992 nyota nyekundu pamoja na
Pan Africa wote waliniwinda ili kunisajili,nyota nyekundu pamoja na Pan wote
walituma watu wao kunitafuka, lakini mimi mwenyewe nilikuwa na mapenzi na pan
na nilikuwa siipendi nyota nyekundu.
“kuna jamaa mmoja wa nyota nyekundu
alikuwa akikaa mtaani kwetu alikuwa akinifuatilia sana akanichukua mimi na kaka
yangu adi ofisini kwa timu yao, mimi nikamwambia kaka yangu kuwa tuwadanganye
mimi nimesaini Timu nyingine hivyo nitashindwa kusaini kwao,kweli nikawaambi
kuwa tayari nilikuwa na mkataba sehemu nyingine hivyo itaniwia vigumu kusaini
kwao.
“uongozi wa Nyota nyekundu walinipa
mkataba na wakaniambia kuwa wapo tayari kurudisha fedha za timu ambayo mimi
nilikuwa nimechukua,kaka yangu baada ya kuona Nyota nyekundu wanatoa pesa
alilainika akanishawishi kusaini mimi sikuwa na mtetezi nikasaini Mkataba.
“Baada ya kufanya mazoezi siku nne
nikakutana na kiongozi wa Pan nikamweleza kuwa nimesaini Nyota akanichukua adi
ofisini kwao na wakanipa mkataba na wao wakahaidi kurudisha fedha ambazo nilichukua
toka Red Stars,kwa kuwa nilikuwa na mapenzi na Pan afrika nikasaini mkataba pia
nikahama mtaa ambao nilikuwa na nikaa mara ya kwanza niaamia mtaa wa Namanga
msasani kwa mama mkubwa ili viongozi wa Nyota Nyekungu wasinione.
“kitu ambacho kilinifanya nisicheze
kwa msimu mzima ni kwamba viongozi wa Pan waliwafuata Nyota na kuwatukana huku
wakiwakebei kuwa hawana pesa hivyo nyota nyekundu wakagoma kupokea pesa toka
Pan na wakasema kuwa wanamtaka mchezaji wao,kwa hali hiyo ilinilazimu kusugua
bechi adi timu ilipopanda ligi kuu hapo nikapata nafsi ya kuanza kuchezea Pan
Afrika katika mechi za mashindano,pia kwa kipindi hicho pia nilikuwa nikichezea
timu ya mtaani hapo ya Namanga Fc.
Timu ya taifa.
“sijisifii ila kutokana na uwezo
wangu mkubwa wa kusakata kandanda nimefanikiwa kutumukia kikosi cha timu ya
taifa kwa misimu mingi sana,ambapo ifuatayo ni baadhi ya miaka ambayo
naikumbuka nimechezea timu ya Taifa,mwaka,1993,1994,1996,1998,2001 pamoja na
mwaka 2005 ambao ulikuwa mwaka wangu wa mwisho kuitwa timu ta Taifa.
Tukio kali
Anacheka kisha anaendelea; ”katika
mchezo wa soka kama timu yenu ikipata ushindi wachezaji ufarijika sana,sasa
kilicochotokea baada ya kumalizika kwa mchezo wetu mjini Bulawayo kati ya
yanga na wapinzani wetu Said Maurid alinitonya kuwa kuna zawadi ya
mchezaji bora twende tukachukue ambapo yeye alikuwa nyota wa mchezo ule
na aliniambia kuwa zawadi hiyo ni boksi moja la castle leager.
“mimi nilifurahi sana na nikamwambia
SMG asitoe taarifa kwa mtu mwingine adi baada ta kuchukua kile kinywaji,kweli
tukaenda kwa uongozi wa siku ile na tukakabidhiwa mzigo wetu tukaondoka nao
baada ya kuondoka Said Maurid yeye alikuwa hatumii pombe mimi nikachukua lile
furushi nikaenda nalo chooni nikafungua haraka na kuitoa castle nne na nikafungua
moja nikaaza kubugia huku nikipita kuimba huku nikiwatonya wenzangu kwa ishara
kuwa waende chooni kuna mzigo.
“wachezaji wezangu wakaenda chooni
kuvamia ule mzigo ambapo kuna wengine walichua mbili mbili wengine moja pi wapo
ambao walikosaka, sherehe ikaendelea mpaka tulipokwea pipa kuelejea
nyumbani Tanzania.
Tulisafiri kwa basi na timu ya Taifa
adi Zambia.
“mwaka 2003 timu yetu ya Taifa la
Tanzania sisi tukiwa wachezaji tulienda kwa usafiri wa Basi toka Dar es Salam
adi Zambia isipokuwa wachezaji watatu ndio walienda kwa usafiri wa ndege
akiwemo Juma Kaseja pamoja na Pawasa kiukweli tulichoka sana kwa kuwa tulikaa
kwenye basi kwa muda mrefu Sana.
“siku ya mechi wachezaji wa timu ya
taifa ya Zambia walicheza mpira mzuri sana kushinda sisi kwa kuwa tulikuwa bado
na uchovu wa safari ingawa juma kaseja alicheza vizuri sana siku ile hata hivyo
zambi walitutungua bao 2-0 na wao wakasonga mbele sisi Tukarudi nyumbi mikono
kichwani.
Wachezaji nyota.
“Tegete wa yanga alikuja vizuri sana
lakini kwa sasa amejilemaza kiwango kimepungua pia mchezaji wa kimataifa wa
Rwanga beki mbuyu Twete anafanya vizuri.
Ushauri.
“rais Malinzi ajitaidi kutekeleza
majukumu yake kama inavyotakiwa kwanza nampongeza kwa mpango wake wa kuzunguka
nchi zima kusaka vipaji kwa ajili ya timu imara ya Taifa,pia wasimamie
uwepo wa shule za michezo za ukweli ili kuhakikisha soka letu linafika mbali
kimataifa.
Maisha baada ya soka.
“Umri wangu ni miaka 43hadi 2013,
nina cheti cha ukocha nafundisha timu ya Daraja la kwanza ya Frend Rangers ,pia
nafanya biashara ndogo ndogo,na nina watoto watatu”,Anaitimisha Ali Yusuph
Maarufu kwa jina la Tigana ambaye alifanikiwa kutikisa soka la hapa nchini kwa
kucheza simba na Yanga pia timu ya Taifa ya Tanzania.
mwisho
Chapisha Maoni