Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.





Shaibu Kambanga.

  

“Mwaka 1994 nilimshushia mwamzi kipigo ambaye alikuwa akichezesha mechi yetu na Shinyanga Shooting kwa kosa la kuzidisha muda wakati Dakika 90 na zile za nyongeza zilikuwa zimekamilika yeye  kwa vile hakutaka Maji Maji tushinde mchezo ule na sisi tayari tulikuwa tunaongoza bao 1-0 aliongeza dakika nyingine takribani 7 hadi wapinzani wetu walipopata bao la kusawazisha na akamaliza mpira.

Wakati mpira unaendelea nikamfua mwamzi na kumwambia kama Shinyanga watasawazisha bao letu ningempiga,kwa kweli mara baada ya mwamzi kumaliza mpira na matokeo kusomeka 1-1 kama ambavyo nilihaidi sikufanya ajizi  nilimfuata mwamzi na kumshushia kichapo cha maana ambapo wachezaji wenzangu walishitukia mwamzi yupo chini baadae polisi walinichukua na kunipeleka kituoni  kwa kosa la kushika sheria mkononi.

 lakini niliachiwa saa sita usiku na nikawa huru pia usiku ule ule nilikutana na yule mwamzi mara baada ya kumwona nikamwomba msamaha na baadae tofauti zetu zikawa zimeisha na tukaagana kwa amani,lakini kikubwa kilichomfanya awapendelea wale jamaa ni kwamba msimu ule
Shaibu Kambanga makala.......Shinyanga walikuwa katika msitari wa kushuka daraja na walihaidi timu yeyote itakayokatiza ukanda wa ziwa  kwa hali yeyote lazima itafungwa, mwamzi aliongwa lakini mchezo ulikuwa ni mgumu sana upande wao kutokana na ubora wa Maji Maji.
Baadae Fat walinifungia miezi 6 adhabu ambayo nililidhia kuitumikia,ila kitu ambacho sikukipenda Fat  hawakutangaza mapema kama nimefungiwa walisubiri hadi Mchezo uliofuata kati yetu na Yanga Mjini Songea ndipo walipotangaza nimefungiwa tayari nikiwa nimevaa jenzi sikuwa na jinsi nikavua jenzi na kumpisha mwezangu”

  Anasimulia Shaibu Kambanga ambaye alikuwa Mlinda Mlango wa Kutumainiwa wa Maji Maji ya Songea Mwaka 1989 hadi 2000,na kufanikiwa kuandika rekodi kubwa katika medani ya soka hapa nchini.

Kambanga ambaye ni mtoto wa kwanza katika familia yenye watoto 8 ya mzee Kambanga,alizaliwa mkoani Mtwara eneo la Ligula na kupata elimu ya msingi katika Shule ya Ligula nyota yake ilianza kuangaza tangu akiwa shuleni hapo na kusifiwa na kila aliyemwona.


Katika maojiano maalumu na Jelamba viwanjani anafafanua zaidi kuhusu maisha yake ya mpira;-

  “Nilianza kucheza  Soka la ushindani nikiwa na Toto Afrika ya Mtwara mwaka 19884 timu ambayo niliichezea kwa miaka 3 ambapo mwaka 1997 nikajiunga na Opec Fc ya masasi timu ambayo nilipata ujunzi wa kutosha kwa kuwa nilikutana na makocha kama Namanje pamoja na Molisi ambao walinifua vilivyo na nikacheza vizuri hadi timu yetu ikapata nafsi ya kushiriki ligi ya Mkoa kanda,tukiwa kanda Maji Maji wakalizika na mchango wangu wakanichukua moja kwa moja.

  ''Niliichezea Maji Maji  toka mwaka 89 kwa mafanikio makubwa sana ambapo kufikia 2000 nikaamua kulipa kisogo soka na kuangaikia maisha yangu.

Simba yanga walishindwa masharti yangu.


  ''Wakati nacheza Maji Maji pia nilikuwa mwajiliwa kama dereva katika ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Ruvuma niliwaambia kama wanaitaji uduma yangu kwa dhati waniamishie kikazi katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salam kama dereva wa pale wote walishindwa na nikaendelea kuchezea Maji Maji.

  ''Sikutaka kwenda kucheza mpira Simba na Yanga bila kazi kwa kuwa viongozi wa timu hizo ni wanafiki sana mara nyingi wanawatelekeza wachezaji katika mazingira ya kutatanisha na wanaondoka mikono mitupu Mfano Omri Husein na John Alex waliachwa na timu hizo na waliathirika sana kisaikorojia.


 Ulevi ulichangia kupoteza mechi na Mkana Red Devols ya Zambia.

  ''Nakumbuka mwaka 1989  Maji Maji tulitandikwa bao 3-0 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Mkana Red Devols toka zambia chanzo kikubwa cha kupoteza mchezo ule wachezaji wa Maji Maji usiku wa kuamkia mchezo walilewa sana kwa sababu walibweteka na sare ya bao 2-2 na  Simba hali ambayo ilipelekea kutoa mwanya kwa wapinzani wetu kucheza kwa nguvu na kutuzidi ujanja.

  ''Nakumbuka siku ile nilicheza vizuri sana kwa upande wetu mwisho wa mchezo wachezaji wa Mkana wakaniita na wakaniambia na cheza vizuri na ili nifike mbali natakiwa kujituma sana katika mazoezi na kumsikiza mwalimu.

 ''Na kingine ambacho kila nikifikiria kuhusu mchezo ule najawa na huzuni,ni kwamba moja ya wachezaji walionipa ushauri toka timu ile wachezaji 6 walipoteza maisha kwa ajali ya ndege  wakiwa na timu ya Taifa ya Zambia hali ambayo inanifanya kujisikia uchungu sana pindi ninapokumbuka tokio lile.
Nimenusurika kifo kwa Ajari mara 3.

  ''Ajali ya kwanza ilitokea Misungwi mwanza tulikuwa tunatoka kucheza na pamba ya mwanza dereva  wa basi letu alikuwa amelewa  kwa kuwa toka tulipotoka stendi makonda walisema kuwa hatutafika mbali sisi tukabaki midomo wazi lakini kwa kuwa ilikuwa asubuhi hatukuwa na uhakika kama dereva alikuwa amelewa.

 ''Tukaondoka mwanza huku dereva akiwa mwendo kasi sana na alikuwa kimya muda wote lakini baada ya kusafiri kwa takribani km 40 toka mwanza mjini kuna sehemu bara bara ilikuwa ikifanyiwa matengenezo kwa kuwa dereva alikuwa mwendo kasi gari likamshinda na hatimaye likapinduka.

  ''Mimi niliumia zaidi kuriko wezangu wote nakumbuka nilipasuka sehemu ya kichwa pia nilikatika sikio tukio ambalo liliniweka nje ya uwanja kwa kipindi kirefu na baada ya kupata matibabu ya uhakika nikarejea uwanjani.

  ''Tukio lingine mwaka 2001 muda mfupi mara baada ya kusitaafu soka nikiwa na gari la mkuu wa Wilaya Songea Mjini nilipata ajali Mbaya sana mimi  nikiwa Dereva,nashindwa  kuelezea zaidi kuhusu ajari ile kwa kuwa najisikia uchungu sana kwa mazingara ya ile ajari.

 ''Ninachoweza kusema kuhusu ile  Ajari nilifungwa jela na sikupata msaada toka kwa mtu yeyote wakiwemo Maji Maji ambao niliwatumikia kwa mafanikio makubwa kama sio msamaha wa Rais ningeozea jela.

 ''Ajari nyingine ambayo kama si kudra za mwenyezi mungu nilikuwa naongoka duniani ni kukanyagwa na tairi la Basi eneo la Mafinga Iringa,mimi nilikuwa dereva msaidizi kwenye gari letu wakati tupo Mafinga nishuka kwenye gari pembezoni mwa Bara bara kuchukua mzigo gafla nihisi kitu kinavunja Mguu nikapata nguvu na kuruka kwa kasi kuelekea upande wa pili wa bara bara ambapo ngozi na nyama toka juu ya ugoko ilikuwa imeshuka chini lakini mara baada ya kufanyiwa vipimo mfupa ulikuwa mzima nikatibiwa na nikaruhusiwa kurudi nyumba,kwa kweli ajari hizi ni rahisi kusimulia ukweli ni kwamba nimeponea chupu chupu.

   Asimulia tukio la Sikinde kumtemea mate Mwameja.  


''Mwaka 1995 wakati wa mechi ya Maji Maji na Simba {Marehemu}  Selestine Sikinde alifanya majaribio mengi sana ya kumfunga Mwameja  ikashindikana kupata bao alichokifanya akamfuata Mohamed mwameja kwa hasira na kumtemea mate usoni tukio lile limchukiza sana mwameja akaanza kumkimbiza sikinde uwanja mzima mashabiki wote uwanjani wakawa wanashangaa.

  ''Sikinde alitimua mbio moja kwa moja adi kwangu mimi nikamchukua na kumweka mgongoni kwangu  arafu nimnyoshea mkono Mwameja ishara ya onyo kuwa akisogea angekiona cha mtemakuni kwa kuwa wachezaji wengi walikuwa wakikumbuka tukio nililomfanya mwamzi Shinyanga na katika timu yetu walikuwa wananijua kama kamanda wao Mwameja akasalimu   amri na mwamzi akawapa kadi ya njano kila mmoja,baada ya tukio lile mashabiki walicheka sana na kunishangili kwa kitendo cha kumwokoa Sikinde asichezee kichapo toka kwa mwameja,lakini hadi mwisho wa mchezo matokeo ni 0-0.


Kwanini alifanishwa na Peter Shilton wa Uingereza?.

  ''Mwanzoni hata mimi ni likuwa nashangaa kusikia watu wakiniita kwa jina la Shilton lakini baada ya kuwauliza waliniambia vitu vyangu ninavyovifanya vinafanana na yeye kwa wao mashabiki na wanahabari walikuwa wakiburudika sana pindi niwa golini.

 ''Kipindi nacheza nilikuwa na uwezo wa kudaka mpira katika mazingira yeyote kutokana na uwezo wangu mkubwa wa kuruka sarakasi hali ambayo ikiperekea kukubaria.

  ''Kwa kipindi kile kila timu ilikuwa na washambuliaji wakatili kiasi kwamba ilikuwa ni ngumu sana kwa makipa hasa ukizingatia sheria za  kumlinda golikipa zilikuwa nyepesa ikilinganishwa na saizi,pia mimi kwa upande wangu nilikuwa simwogopi mshambuliaji yeyote,mtu ambaye mimi nilikuwa namweshimu kwa kupiga mashuti alikuwa Madaraka Suleiman Mzee wa kiminyio huyo alikuwa balaa lakini kwangu aligonga mwamba adi mwenyewe alijishangaa lakini wakati nipo maji maji yeye nilikuwa namtumia kama mtu wa kunifanyisha mazoezi ya mashuti.

 ''Nakumbuka baada ya mzoezi na mwalimu nilikuwa namwita Madaraka na kunifanyia mazoezi ya mashuti tuliwa pekee yetu,alikuwa anapaga kwenye eneo la penalti na nje ya 18 mara nyingi tulikuwa tunaweka mashuti 40,lakini kutokana na uwezo wangu kati ya mashuti 40 nilikuwa naweza kudaka au kupangua mashuti  35 huku nikiruhusu kuingia kwenye kamba mashuti 4 au 5 pekee hali ambayo ilinifanya niimalike zaidi pindi niwapo uwanja hapo ndipo jina la Shilton lilipotea.


Acheza mechi 30 peke yake bila msaidizi.


  ''Nikiwa na Maji Maji niliwai kucheza mchezo 30 peke yangu bila msaidizi kipindi hicho mlinda mlango katika timu nilibakia pekee yangu mara baada ya wezangu kuondoka morali ya mchezo kwangu ilikuwa juu sana nilikuwa adi nilijiogopa.

  ''Kuna kipindi nilikuwa nimeumia goti mchezo zidi ya Ushirika ya Moshi ilinilazimu kucheza kwa kuwa timu ilikuwa haina mlinda mlango mwingine,nikapigwa sindano ya ganzi na kuingia uwanjani, katika mchezo huo tulipata ushindi wa bao 2-0,hadi mwisho wa msimu nikiwa mlangoni pekee yangu timu ilimaliza katika nafasi ya nne.

Ulevi,wanawake tatizo kwa wachezaji.

Wachezaji wetu lazima wajitambue  kwa kuwa athari za kuwa na wanawake na kunywa pombe zipo wazi kwa mchezaji zinapunguza nguvu kwa wachezaji hasa wa siku izi wamekuwa wakionekana katika viwanja vya starehe siku za mechi ngumu pasipo kujali afya zao kama wachezaji.


  ''Mimi kwa uzoefu  wangu nafahamu mchezaji akifanya mapenzi inachukua siku 3 kurudisha nguvu zake za kawaida,mchezaji ili acheze vizuri kwa kiwango chake inatakiwa asifanye mapenzi siku tatu kabla ya mchezo na kama atafanya siku moja kabla hawezi akacheza kwa kiwango chake.

  ''Mimi muda wote ambao nilicheza katika kiwango cha juu kiwango changu kilikuwa kile kile kwa kuwa nilikuwa nafuata sheria za kurinda afya nikiwa kama mchezaji,kuna kipindi  nilikaa Miezi mitatu bila kukutana na mke wangu lakini kwa wachezaji wa siku izi ni ngumu.  


  Upenzi kwa Simba ni chanzo cha Maji Maji kujichinja yenyewe kwa ushirikina.
''Mwaka 1996 mzee wa timu ya Maji Maji sitamtaja jina kwa kuwa namweshimu sana alituita chumbani na kutufunika shuka nyeupe akaanza kupiga Manyanga mimi nilikuwa nimekaa na marehemu Kisochi lemba mzee alikuwa anaongea lugha ambayo hakuna aliyekuwa anailewa lakini ilikuwa kila akipita nilipo mimi nilisika neno la mwisho akisema Maji Maji tufungwe tatu na Simba nilijaribu kumweleza mwezamu yeye akasema sio kweli ila mzee kasema Maji Maji tushinde tatu,niliendelea kumsikiliza yule mzee kwa makini sana na baada ya tukio lile nilijalimu kuwaeleza wenzangu wote walishangaa.
 ''Tukaja kwenye mechi mchezo ulikuwa mgumu sana upande wetu na kama yule mzee nilivyomsikia mimi Simba walituzibua bao 3-0 na yule Mzee ni mwanachama hai wa Simba Mwenye kadi.
''Na mara nyingi ilikuwa Siku ya Mechi na Simba Wachezaji wa Maji Maji walikuwa wakituwekea dawa kwenye chakula ili kutupunguza nguvu.
“Mechi zote ambazo tulikuwa tunacheza na Simba chakula alikuwa anapika Yule Mzee ambaye ni Mganga wetu lakini mechi zingine alikuwa anapika mtu mwingine,nakumbuka siku ambayo alituombea kufungwa dhidi ya Simba alituwekea dawa kwenye chakula ili kutupunguza nguvu,kutokana na tukio lile Masaa machache kabla ya Mchezo mwezetu John Alex aliamua kuchukua vifaa vyake na kurudi nyumbani,hali ambayo hakuna mtu yeyote ambaye alishituka na baada ya mchezo tukakung’utwa na Simba huku wachezaji tukiwa hoi.
Atoboa siri ya Maji Maji kuwa kibonde kwa Simba.


  ''Asilimia 90 ya viongozi wa Maji Maji ni mashabiki na wadau wa Simba hadi hivi sasa hali ambayo inapelekea Maji Maji kufungwa Nyumbani na ugenini huku wakijikakamua  sana ni sare mara nyingi simba inapofika Songea toka miaka ya 1990,maandalizi yanakuwa afifu sana na tatizo kubwa ni ushabiki wa viongozi.

Yanga hata hikutane na Maji Maji ya sasa,hawachomoki kwenye uwanja wa Songea.

  ''Mara nyingi mechi na  yanga maandalizi yanakuwa makubwa sana ndani na nje ya uwanja na ukizingatia viongozi wengi ni wanachama wa Simba kila mwanamaji Maji anaingia uwanjani kwa lengo moja tu  kuiangamiza yanga,kiukweli kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni ushindi kwa Yanga katika uwanja wa Maji Maji ni sare.

  ''Lakini tatizo kubwa ambalo limepelekea Maji Maji kuwa na Hasira kubwa kwa Yanga kuna wakati Maji Maji iliposhuka daraja kwa Mara ya Kwanza mchezo wa Mwisho walikutana na Yanga kila timu ilikuwa ikiitaji pointi moja tu kwa maji maji asishuke  Daraja lakini kwa Yanga kutangazwa bingwa.

  ''kitu ambacho kilitokea katika mchezo ule ambao  nakumbuka ulipigwa Morogoro Yanga waliisaliti Maji Maji na kuishindilia kichapo bila huruma cha bao 4-0,hali ile ilipelekea uhasama na Yanga kuongezeka mara dufu na toka siku hiyo adi leo Yanga hawajawai pata ushindi Songea.

 Ardhi Wameninyang'anya uwanja wangu.


   ''wakati nacheza  Maji Maji timu ilinipa viwanja Viwili kimoja Ruvuma kingine Msamala,lakini kitu ambacho kimetokea ardhi wamenipora na nimejaribu kufuatili hakuna ufumbuzi uliopatikana hali ambayo inanipa uchungu mkubwa Sana nikikumbuka huwa najawa na hasira kali sana.

  ''Lakini nashukuru uwanja wa Ruvuma nimejenga na upo vizuri na maisha yanazidi kusonga.

Malanzi ya tambazi yamezorotesha Maisha yangu.

  ''Mwaka huu toka mwenzi wa saba sijafanya kazi,kutokana na mguu wangu kuvimba sana kwa homa ya  Tambazi.  
Kwa asiyefahamu tambazi ni uvimbe ambao unatokea sehemu yeyote ya mwili unafafanana na jipu lakini kwa tambazi uvimbe unakuwa mkubwa sasa kwa sisi waafrika unaweza kusema umerogwa,kumbe ni mkusajiko wa sumu pamoja na uchafu ambao unakuwa umejikusanya sehemu moja ya mwili na unatafuta sehemu ya kutokea.

  ''kwa kweli mguu wangu ulikuwa umejaa sana hali ambayo ilipelekea kuacha shughuli zote na kushinda nyumbani huku mke wangu,pamoja na boss wangu wa kampuni ya Ottawa wamekuwa wakiniudumia vizuri sana mungu awape baraka tele,na naendelea vizuri nitarejea kazini kama dereva muda sio mrefu.

Mchezaji anayempenda.

  ''Wachezaji wengi wanapewa Majina makubwa ambayo yanapingana na uwezo wao lakini Mrisho alfan Ngassa namkubari sana kwa kufanikiwa kuzichanganya Simba,Azam na Yanga na kwasasa ametajirika kupitia timu hizo.

Ushauri kwa Maji Maji.


Viongozi wa Maji Maji wameweka wigo mkubwa kwa wachezaji wa zamani Sisi ndio tunajua mbinu mbali mbali za kimpira na tunajua  timu inatakiwa kufanya nini ikiwa katika wakati wowote bila kujali pesa,watupe nafsi ya kuwa karibu na  timu naamini tutatoa mchango Mzuri.

 ''Kuna kipindi Mlale Jkt walinichukua wakati wanakaribia kupanda daraja niliwashauri mambo mengi sana adi leo wanaeshimu mchango wangu.

Anachokumbuka akiwa mchezaji Wa  Maji Maji.

  ''kuna kipindi mbinu za mwalimu zinakuwa zimefeli uwanjani inalazimika kutumia nguvu za ziada ili kupata ushindi sisi Maji Maji tulikuwa na mtu alikuwa anaitwa Evans Ponella huyo alikuwa balaa kwa kumiliki mpira na kupiga chenga mimi namfananisha na J J Okocha wa Nigeria,basi ikifikia dakika ya 80 timu imefungwa au tunaitaji ushindi,wachezaji wote tulikuwa tukipeana ishara kuwa pasi zote ziende kwa ponella.

  ''Yeye Alikuwa na stamina ya hali ya juu na alikuwa akikata chenga kuelekea eneo la 18 kutokana na uwezo wake alikuwa anawauzi sana mabeka na wakawa wanamfanyia sana faulo hali ambayo ilipelekea sisi kupata penalti nyingi sana na mara nyingi tulikuwa tunaibuka na ushindi dakika za mwisho kupitia yeye.
Baada ya kustaafu mpira.

  ''Mimi ni dereva,nimeendesha magari ya serikali,taxi na sasa ni dereva wa Basi katika kampuni ya Ottawa high Class safari za kwenda dar,maisha yangu yanaenda vinzuri.

  ''Ninamke na watoto 3 nilizaliwa mwaka 1966 naipenda sana familia yangu,Anaitimisha Shaibu Kamba kwa kushusha pumzi ndefu mara baada ya kusimuli matukio mazito ambayo hakupenda kuyakumbuka kwa kipindi hiki.  
…………………………………………………mwisho………………………………………………………..


Chapisha Maoni