David
Aidani Mjanja ni miongoni mwa washambuliaji maili ambao waliwahi
tokea na waliwika sana hapa nchini mnamo miaka ya 1990 -2005,katika club
tofauti za ligi kuu hapa nchini,na Timu ya Taifa.
Mjanja
ambaye ni mtoto wa saba katika familia yenye watoto 8 alizaliwa mwaka 1973
katika Kijiji cha Mdemu mkoani Dodoma, katika maojiano maalum ameeleza mengi na
kufafanua historia ya maisha yake ya soka kwa kina;
David mjanja wapili toka kushoto [waliosimama]
“nilianza
kucheza mpira katika shule ya msingi mndemu huko Dodoma ,na baada ya kuhitimu
elimu ya shule ya msingi nikajiunga na chuo cha ufundi Makenika N V T C,kwa sasa
ni chuo cha Veta,baada ya kuitimu nilipata ajira katika kiwanda cha Mazuria
Morogoro,hapo ndipo nyota yangu ilipoanza kunga’aa na nikafanikiwa kupata
nafasi ya kuitumikia timu ya mkoa wa Morogoro.
“Ushirika
ya Moshi walivutiwa na uwezo wangu wa kusakata kabumbu nikiwa na timu ya mkoa
wa Morogoro ambapo 1991 nikajiunga na timu hiyo hapo nilidumu hadi 1994
ndipo nilipoamua kutimukia Yanga timu ambayo ilikuwa ikisaka saini yangu kwa
udi na uvumba kwa kipindi kirefu wakati nikiwa na timu ya Ushirika.
Sababu
za kuongoka Yanga
“Nilipenda
toka moyoni kuchezea Yanga kwa kipindi Kirefu lakini ilinilazimu kuondoka kwa
shingo upandi mara baada ya kukwaruzana na moja wa kiongozi ambaye alikuwepo
katika kamati ya usajiri kwa sababu ambazo mimi mwenyewe adi leo hii
sizifahamu.
“nakumbuka
niliambiwa kuwa tayari jina langu limeshawekwa kwa ajili ya kusainishwa mkataba
mwingine,lakini yule kiongozi akaamua kulikata jina langu na kumweka mchezaji
ambaye alikuwa amemtafuta yeye mwenyewe ili kuniondoa kwa maslai binafsi
iliniuma sana na mwaka 1997 nikaamua kutimukia Maji Maji ya Songea.
“Wakati
nikiwa Maji Maji maisha yalikuwa mazuri kwa kuwa Maji Maji ya kipindi kile
ilikuwa na uongozi imara nikacheza pale hadi 2000 Prisons wakaniona kutokana na
uwezo wangu wa kupachika mabao na wakaamu kunichukua, ambapo nilichezea Prisons
hadi 2005 hapo ndipo nikafikiria kustaafu soka.
“Lakini
kwa kipindi hicho Prisons walikuwa na Tawi la Timu yao Tanga ambalo
iklifahamika kwa kwa jina la Small Prisons wakaamua kunipereka Tanga ambako
niliendelea kutumikia Timu hiyo.
“Baada
ya kuitumikia timu Hiyo kwa misimu mitatu hapo ndipo nikaona uwezo wangu wa
kusakata kabumbu umefikia kikomo na mwaka 2008,nikatangaza kutundika Daruga,na
kuyapa kisogo mambo yote yahusuyo kandanda.
Hawezi
kusahau
“Mwaka
1995,katika meshi ya watani wa jani Simba na Yanga wakati mimi nipo Yanga kuna
tukio lilifanyika Usiku wa manane katika uwanja wa jangwani unaweza usihamini
lakini siku hiyo alichukuliwa mbuzi mzima na kufukiwa katikati ya uwanja ili
kuwaloga Simba.
“Tukio
hilo ambalo lilifanyika ndani ya Dakika kumi na Tano,alichukuliwa mbuzi Mzima
huku akiwa amezibwa kwa Pamba katika maeneo yote ambayo yanatoa Hewa huku kila
mchezaji akiwa na mganga wake binafsi pakachimbwa shimo huku zikinyunyizwa dawa
na kumfukia yule Mbuzi.
“wakati
tukiendelea kupewa dawa zingine wale waganga walitupa masharti na kutuambia
kuwa mtu yeyote atakayetoa siri na kupokea pesa kwa ajili ya kuhujumu timu
atakutwa na Adhabu kali Sana.
“Asubuhi
tukaamka na tukajiandaa na mchezo,wakati wa mechi ulipofika tukaingia uwanjani
kwa kweli mchezo ulikuwa mgumu sana kutokana na umahili wa Simba ya kipindi
kile Hadi mwamzi wa katikati alipopuliza kipenga kuhahiria dakika 90 za mchezo
zimemalizika Simba 1,Yanga 0 bao ambalo lilipachikwa kimiani na Dua
Saidi,siwezi kusahau.
“Nakumbuka
wachezaji wa Yanga walikuwa Steven Nemes,Kenny Mkapa,Salumu Kabunda,Wille
Martin,Method Mogela,Said Mwamba,Mohamed Husein,Edbili Lunyamila,David Mjanja
Pamoja na Sanifu Lazaro,ambayo licha ya maandalizi ambayo timu yetu iliyafanya
ndani na nje ya uwanja tulitoka uwanjani tukiwa vichwa chini.
“Kiukweli
ushirikina hauna mchango wowote katika mpira zaidi ya mazoezi na na kujituma
uwanjani, lazima nchi zetu za kiafrika zibadilike kama tunataka kufika mbali
kisoka na pawepo na viongozi na sio watawala.
Haijawai
Tokea
“nalikumbuka
bao ambalo nililifunga mwaka 1998 nikiwa na Timu ya Maji Maji ya Songea
dhidi ya wekundu wa msimbazi Simba Toka Jijini Dar Es Salam, mara baada ya
Kelvin Haule kuingiza crosi safi Toka winga ya kulia nami Sikufanya hajizi
nikapiga shuti kali golini ambapo kilichotokea hata mimi sielewi niliupigaje
ule mpira Golikipa Joseph Katuba akiwa amezubaa Pale Golini ule mpira Uligonga
mara tatu mwamba wa juu na chini kwenye chaki mfurulizo na kutumbukia
Kimiani,ni tukio la pekee ambayo mimi sikumbuki kama limewai tokea katika mechi
zingine.
Mechi
anayokumbuka
“Kipindi
nipo yanga ilikuja timu toka afrika kusini [ Vall professional] ,ilikuwa mechi
ngumu sana nakumbuka ilikuwa club bingwa Afrika raundi ya kwanza na mimi
niliingia kipindi cha pili na katika mechi hiyo tulifanikiwa kupata ushindi wa
bao 2-1,hali ambayo ilipelekea mchezo wa marudiano kuwa mgumu zaidi kwani
ilitulazimu kusafiri hadi ugenini.
“Hatukukata
tamaa tukafanya mazoezi ya nguvu na tukajiweka fiti kwa ajiri ya mchezo
wa marudiano,katka mchezo huo wa marudiano ambao ulichezwa nchini afrika kusini
tulicheza kwa kujituma sana na hadi mwisho wa mchezo tuliambulia sare ya bao
1-1,ambapo bao la ugenini likatusogeza katika raundi ya pili ambayo tulipambana
na timu kutoka visiwa vya usheli sheli.
Hakuwai
humia
“Mungu
mweza wa yote kwani kwa kipindi chote ambacho nilikuwa nikicheza kwa takribani
miaka 15,sikuwai humia nilikuwa nacheza mpira bila matatizo yeyote zaidi tuu ya
maumivu ya kawaida pindi mchezaji atokapo uwanjani kama ilivyokuwa kwa
wachezaji wezangu.
Maoni
yake kuhusu Timu ya taifa
“Timu
ya taifa ya sasa imepiga hatua angalau wachezaji wanacheza mpira wa kuvutia ila
kinachotakiwa kufanyika ni wachezaji kuwa wazalendo pamoja na Tff kuwa karibu
Na timu kwa hali na mali.
Baada
ya kustaafu
“kwa
sasa mimi ni Askari Magereza kazi ambayo niliipata tangu nilipokuwa nikichezea
Tanzania Prisons mara baada ya kuwapa masharti ya kutokuchezea timu yao hadi
watakapo nipa kazi kweli walilidhia ombi langu na wakanifanyia mpango wa ajira
ya kudumu.
“Sasa
ivi nipo Singida ambapo Nimeoa na nina watoto wawili,pia nafanya kazi ya ufundi
ambao niliusomea kabla ya kuanza kung’ara katka medani ya Soka.
Anasimulia
David Mjanja ambaye kwa sasa yupo bize na kazi ya uaskari magereza ambapo kwa
kipindi chote ambacho amecheza mpira alipata nafasi ya kuchezea timu ya taifa
mara moja tu katika mechi ya kirafiki zidi ya Kenya wakati yupo Ushirika ya
Moshi,pia amekili wazi kuwa alikuwa akisumbuliwa sana na Mohamed Mwameja wa Simba
ambaye katika maisha yake ya soka alifanikiwa kumfunga bao moja pekee.
Chapisha Maoni