Na Alex Mapunda.
KELVIN Haule ni miongoni viungo
washambuliaji wachache ambao walikuwa na uwezo mkubwa wa kufunga ambapo jina
lake lilikuwa kubwa alipochezea Maji Maji Pamoja na Timu ya Taifa “Taifa
Stars”.
Katika mazungumzo
maalum na Gazeti hili ameeleza mengi kuhusu maisha yake ya soka wakati
akicheza:
“nilianza kucheza soka Tangu
nilipokuwa mdogo kwa kuwa niliupenda mchezo huo,lakini nilianza kucheza soka la
ushindani katika kiwanda cha nyuzi Iringa mwaka 1983,hapo nilicheza kwa kipindi
cha mwaka 1 na mwaka 1984 nilijiunga na timu ya Reli ya Iringa hapo nilicheza
kwa mafanikio makubwa baadae nikasajiliwa na timu ya Tukuyu stars [Mbeya]ambayo
ilikuwa ikishiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara, kwa sasa Ligi kuu ya
vodacom.
“nilisakata kabumbu kwa
kipindi cha miaka mitatu nikiwa na Tukuyu stars,ambapo timu yetu ilifanikiwa
kushiriki michuano ya Afrika mashariki, mara baada ya timu yetu kufanya vizuri
na katka michuano hiyo tulifanikiwa kufika hatua ya robo fainali na
bahati mbaya tulitolewa na Sports Club Villa toka Uganda katika mechi hiyo
tulifungwa goli 4-1 na tukaaga mashindano.
“kwa kipindi chote ambapo
nilikuwa na Tukuyu Stars nyota yangu ili ng’ara sana ambapo timu mbali mbali
zilikuwa zikinigombania lakini mwaka 1987 nikaamu kujiunga na Maji Maji
ya songea maarufu kama wanalizombe na hapo nikacheza kwa mafanikio
makubwa zaidi na nikaiwezesha maji maji kuwa mabingwa wa ligi ya muungano mara
moja mwaka 98 na kupata nafasi ya
kushiriki clabu bingwa afrika chini ya Meneja wa mahili wa maji maji wa kipindi
hicho Shaffy Bora.
“ Maji maji nilicheza kwa
kipindi kirefu kutokana na uongozi mzuri na mshikamano ambao ulikuwepo ndani ya
timu hiyo na kufikia mwaka 2000 nikaondoka,na kwa kipindi chote hicho kuanzia
mwaka 1987 – 2000 nilipata nafasi ya kucheza timu ya taifa ambapo wakati huo
kiwango changu kilikua zaidi na nikafahamika nje ya mipaka ya Tanzania na
umaarufu wangu ukaongezeka mara dufu.
“Niliamua kutundika
daruga rasmi mwaka 2002 nikiwa na miaka 39 nikiwa na Twiga Stars ya kinondoni
timu ambayo sikuchoeza kwa mafaniko makubwa kutokana na kwenda kwa umri na
kutofurahishwa na maslahi ya kipindi hicho hapo nikatundika daruga na kubakia
katika timu za veterans.
Sababu za kuto kucheza Timu kubwa
“Sikucheza timu kubwa kwa
sasabu timu hizo toka kipindi hicho hazikuwa na malengo endelevu kwa wachezaji
kikubwa walikuwa wanaitaji uduma ya mchezaji na sio kumjengea mchezaji maisha
ya baadae,lakini nikacheza kwa mafanikio makubwa ingwa sikujiunga na timu hizo
ambazo zina mizengwe na zinawajali wachezaji wa upande.
“Kuna kipindi nitekekezwa na
Yanga hotelini mwaka 1987 wakati nipo na Tukuyu Stars kwa kipindi cha mwenzi
mmoja bila kujua hatima yangu ni ipi huku wakinipa matumaini ya kunipa mkataba
lakini tulishinda baadae kwa kuwa Yanga waligoma kuniamishia kikazi jijini Dar
es salam na wakanitaka nicheze bila kazi kwa kuwa kipindi kile kila Timu
ililazimika kumtafutia mchezaji kazi nje ya soka, nikaamu kuachana nao na na
kujiunga na Wanalizombe mjini Sopngea.
Anachokumbuka
“Stasahau wakati nipovunjika
mguu mwaka mwaka 1987 katika uwanja wa CCM kirumba mwanza katika michuano
ya Shimmuta,wakati ya mechi kati ya NMC-shirika la usagaji pamoja na BIT timu
ambayo iliusisha makampuni ya biashara, katika mechi ambayo ilikuwa na
ushindani mkubwa kutokana na wachezaji wengi wa ligi kuu kusajiliwa na timu
hizo.
“katika mechi hiyo kwa upande wetu
NMC tulishinda goli 2-1 magoli ambayo nilifunga mimi mwenyewe,lakini Vegasitus
Limbu alinichezea rafu mbaya sana na akanivunja mguu,niliumia sana lakini mungu
akajalia nikaudumiwa vizuri na kurejea uwanjani.
Mechi ninayoikumbuka
“Naikumbuka sana mechi
ya clab Bingwa afrika raundi ya Tatu, kati ya Maji Maji na Fc Leopard ya Kenya
ilikuwa ni mechi kali na ngumu sana kwa upande wetu ambapo mchezo wa kwanza
ulifanyika jijini Arusha katika uwanja wa Amri Abeid,walituchalaza goli moja
mtungi hali nambayo ilikatisha tamaa ya kusonga mbele.
“katika mechi ya marudiano nchini
Kenya katika uwanja wa Moi Kasalani mechi ikianza kwa mashambulizi ya kila
upande wakati wote wa mchezo na hadi mwamzi anapuliza kipenga cha mwisho FC
Leopard 0,Maji Maji mtungi na tukatupwa nje kabasa ya mashindano.
Timu za Tanzania kufanya
vibaya
“wachezeji wengi wanaochezea
timu zetu za hapa nyumbani hawana uzoefu mkubwa wa kushindana tofauti na
wachezaji wa timu za wezetu ambao wanacheza mechi nyingi kushinda hapa nyumbani
hilo ni tatizo kubwa Tff lazima walifikile.
“vile vile hapa Tanzania
wachezaji wanaibuka tu kutokana na kucheza mitaani na kucheza timu kubwa ambazo
zinatuwakilisha katika mashindano ya kimataifa,kwa wenzetu wanakuzwa katika
shule za michezo toka wakiwa wadogo,hali ambayo inapelekea timu zetu kufanya
vibaya kimataifa.
Tofauti,FAT-TFF.
kipindi cha Fat wachezaji wa Timu ya
taifa Tulikuwa tunacheza katika mazingira magumu sana hasa kwa upande wa
vifaa,mara nyingi tulikuwa tunabeba vifaa toka nyumbani ikiwemo viatu na muda
mwingine ilitulazimu kufanya mazoezi bila vifaa vyote.
“lakini saizi ingwa kuna
matatizo kipindi kile yalizidi ila tulikuwa tunafanya vizuri kutokana na kwamba
wachezaji wa zamani walikuwa wazalendo na walichulia soka kama sehemu ya maisha
yao.
Wachezaji anaowakubari
“nawakubari sana Shomari
kapombe,saimon msuva pamoja Salum Habubakari[shua Boy] ambao ni chipukizi na
wapo katika viwango vya juu kwa hivi sasa.
“pia navutiwa na kiwango cha
mcheji wa kigeni wa Azam FC toka Ivory Cost kipre Tchetche, ambaye ni moto wa
kuotea mbali.
Mafanikio katika Soka
“kiuchumi mpira haujanisaidia
sana kwa kuwa kipindi kile hapakuwa na maslai kwa wachezaji zaidi ya kupata
pesa ya kula,ila nimefanikiwa kufahamiana na watu mbali mali na kufahamu maeneo
mengi katika nchi nyingi.
Ushauri kwa timu Maji Maji
“viongozi wa timu ya maji
maji wasiongoze timu na kutegemea watapata pesa katika Serikali ya mkoa ilo wafute
na wawe wabunifu kwa kutafuta njia mbadala ili kuongoza timu hiyo kwa manufaa
ya wanamaji maji.
“wadau wa soka wapo mbali na
timu yao ikilinganisha na zamani,lazima warudishe mawazo yao kwa timu ya Maji
maji ili kurudisha maji maji ya ezi zangu ambayo ilitikisa soka la Tanzania.
Maisha baada ya Soka.
“nafanya biashara ndogo ndogo
za ujasiliamali ambazo zinaniingizia kipato pia ni Makamu mwenyekiti wa chama
cha soka songea mjini [SUFA] pia ni katibu wa chama cha makocha mkoa wa Ruvuma,
ingwa sina mafanikio makubwa naishi vizuri na fanilia yangu.
“ sasa nimeoa na nina
watoto watatu wote wa kiume kwangu mimi ni faraja kubwa sana
na naishi nao kwa amani.
Chapisha Maoni