|
Mbopa Luoga
Mbopa Luoga ni miongoni mwa mabeki
imara kuwai kutokea hapa nchini alikuwa moja ya Beki Hatari ambaye aliumiza
vichwa vya washambuliaji hapa nchini miaka ya 1992 hadi 2000 akiwa na Maji Maji
ya Songea.
Luoga,Mzaliwa wa Litui Nyasa,
alianza kucheza mpira tangu akiwa shule ya msingi Kibasila Jijini Dar es Salam
ambako Baba yake aliajiriwa katika wizara ya habari na utamabuni na baadae
wakaamia songea Mjini ambapo alibahatika kujiunga na Maji Maji Kids.Amezungumza
na championi Ijumaa na kufafanua mengi.
“Nilianza kucheza Soka la ushindani
nikiwa na RTC Songea timu ambayo ilikuwa ikishiriki ligi daraja la pili ngazi
ya Taifa mwaka 1887,sikukaa sana ndani ya mwaka huo huo nikatimukia
Urafiki ya Dar [timu ya kiwanda changuo] hapo nilidumu kwa kipindi cha miezi 4.
“Lakini kabla mwaka huo kumalizika
tuliitwa na Timu ya Tanesco Songea wachoezaji wote ambao tulienda Urafiki wote
tukarudi na kukijenga kikosi cha Tanesco ambacho kilicheza kwa nidhamu ya hali
ya juu na kufanikiwa kupanda ligi kuu toka ligi daraja la nne nikiwa kama
kepteni wa timu.
“Timu hiyo ya Tanesco ambayo
ilikuwa ikiongozwa na kocha Ray Gama[marehemu] pamoja na Mdachi Kombo
ilivyunjwa na Tanesco kwa sababu ambazo hazikutajwa ingwa ilikuwa imepanda ligi
kuu.
“Mwaka 1991 kwa kuwa Tanesco
ilivunjwa na uongozi wa timu hiyo ikabadilishwa jina na ikaitwa Zimanimoto ili
kupata nafasi ya kushiriki ligi kuu badala ya Tanesco na tulifanikiwa kucheza
na Yanga,Reli Pamoja na Maji Maji lakini baadae timu ikasambalatika kwa kuwa
tulitakiwa kubaki kazini kama wafanyakazi wa Tanesco.
“Nilitua Maji Maji mwaka
1992,kipindi hicho nikuwa katika kiwango cha juu sana ambapo nikikuwa kiboko ya
washambuliaji hapa nchini pindi walipokuwa wakikutana na timu yetu ya Maji
Maji, hapo nilicheza kwa muda mrefu Sana na kipindi chote hicho nilikuwa
nikiitwa katika timu ya mkoa wa Ruvuma, ambapo mwaka 2001 nikaachana na soka la
ushindani na kubakia kama mchezaji wa Kambalage Veterani na mfanyakazi wa
Tanesco.
Aligoma kujiunga na Yanga naTukuyu
Stars.
“Ndugu mwandishi mtu yeyote hawezi
kuchezea ajira,ni ukweli usiopingika uwezo wangu wa kusakata kabumbu
ulikuwa wa hali ya juu Sana Yanga waliwatuma wawakilishi wao kuja kunichuka
Songea ili kuchezea timu yao kwa kweli sikuwapa nafasi ya kufanya mazungumzo
kwa kuwa nilikuwa naeshimu sana ajira yangu ndani ya Tanesco.
“Vile vile Tukuyu Stars waliniitaji
ili kukitumikia kikosi chao lakini mimi sikuwa tayari kujiunga na Timu yeyote
Hapa nchini nje ya mkoa wa Ruvuma kwa kuwa niliogopa kuweka Rehani ajira yangu
Toka Tanesco.
Awezi kusahau
“Nakumbuka mwaka 1998 mechi
kati ya CDA ya Dodoma na Maji Maji ya Songea ambayo ilichezwa mjini Dodoma
kutokana na uimara wa timu yetu tulishinda bao 1-0 ambao ulichezwa kipindi
waeshimiwa wabunge wakiwa Dodoma,bao ambalo lilifungwa na Maarimu Salehe
Romario dakika ya 72.
“Baada ya Mchezo kuna tukio ambalo
alilifanya mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kipindi kile Mweshimiwa Anna Makinda siwezi
kulisahau kwani baada ya kuizamisha CDA alitukaribishwa kwenye chakula cha
mchana.
“Wakati wa chakula makinda alivua
Viatu na akaweka pembeni na akajifunga kanga kiunoni akawa kama mhudumu,
akachukua maji na Kutunawisha mikono wachezaji wote kama Yesu alivyo waosha
miguu mitume wake na baadae akatuletea chakula na kumpa kila
mchezaji, kwa kweli Tukio lile lilitushitua sana kwa uduma adhimu kama
ile pia ilitupa morali ya hali ya juu sana.
“Mimi sijawai shuudia tukio kama
lile naamini ilikuwa mwanzo na mwisho kutokea na mimi staacha kumwombia makinda
kwa mungu kwa wema wake wote ambao aliufanya akiwa kama mkuu wa mkoa wa Ruvuma
kwa Timu Ya Maji Maji.
Ubingwa wa Maji Maji mwaka 1998.
“Mechi yetu ya mwisho kombe la
Muungano na Prisons ya Mbeya ilikuwa ngumu sana na tulifanikiwa kupata ushindi
kwa mbinde wa bao 2-1 na tukafankiwa kutawazwa mabingwa.
“Nakumbuka Yanga tuliwanyang’anya
tonge mdomoni kwani walitakiwa wapate ushindi dhidi ya Kem kem ya Zanzibar ili
wachukue ubingwa ambapo walipoteza mchezo kwa kufungwa bao 2-1 na kutuacha
wanalizombe tukichekelea.
“Baada ya ushindi huo tulipangwa na
timu ngumu Toka Misri ya National Alhaly katika roundi ya kwanza ya club Bingwa
Afrika wakatukausha Nyumbani na ugenini ambapo dar tulifungwa bao 3-0 na Kairo
tulichezea kipigo cha bao 2-0 Dakika 5 za mwisho.
“Kikosi cha Wanalizombe ambacho
kilitwaa ubingwa mbele ya Tanzania prisons katika uwanja wa sokoine Mbeya
wachezaji ambao walicheza alikuwepo Doi Moke,Ali Mopelo,Omari Husein,Amri
Said,Willy Martin,Mbopa Luoga,Dello Ntumba,Twaha Omari[marehemu],Godfrey Kikumbizi,Said
Mshamu Pamoja na David Mjanja. Garrincha pamoja na Omari Kapilima walikuwepo
kwenye Timu ya Taifa.
Walikuwa wanasali.
“Kipindi sisi Tunacheza Maji Maji
Ushirikina haukuwepo tulikuwa zaidi Tukimtegemea Mungu na mazoezi ya
uhakika ambayo tulikuwa tunayafanya.
“Nakumbuka Mimi,David Mjanja,Dello
Ntumba [mkongomani] pamoja na Daktari wetu wa timu Mzee Chanangula tulikuwa
tukisali pamoja siku moja kabla ya mechi, mara baada ya chakula cha jioni,mara
nyingi ilikuwa kuanzia saa mbili usiku hadi saa Tano.
“Sijui kama viongozi walikuwa
wakifanya mambo mengine kwa Siri lakini mimi walikuwa wakinifahamu kuwa ni mtu
wa sala hivyo hawakuthubutu kuniambia kitu chochote kinyume na mwenyezi Mungu.
Wachezaji anaowapenda
“Nawakubali sana Frenk Domayo wa
yanga Pamoja na Messi wa Barcelona wananikosha sana.
Timu ya Taifa
“Itengenezwe kuanzia chini ili
kuweza kuwa na timu bora, wachezaji waliowengi hapa nchini hawana uwezo wa
kukabiliana na wachezaji wa kutoka nje kwa kuwa uwezo wao ni mdogo,kuwaendeleza
wachezaji wakiwa wamekomaa ni sawa na kumwagilia mmea kwenye majani.
“Bila kuwa na Timu za vijana
tutachelewa sana kushiriki kombe la dunia,mimi nakumbuka nilianza kucheza
kwenye timu ya Vijana ya maji Maji ali ambayo ilipelekea kuwa mchezaji mzuri.
Ushauri kwa Timu Ya Maji Maji.
“Wanaruvuma wote wawe kitu kimoja na
viongozi ili kuiudumia timu kwa moyo mweupe na kama pesa itukepo katika timu
tutakuwa na wachezaji wazuri.
Baada ya kustaafu
“Hadi leo bado ni Mfanyakazi wa
Tanesco kazi ambayo ni msingi wa maisha yangu pia niliwai kuwa mwakirishi wa
mkutano mkuu TFF toka nikiwa kama mjumbe kisha nikachaguliwa kama kocha
msaidizi katika kikosi cha underseventeen cha mkoa wa Ruvuma ambacho kilichukua
ubingwa wa Tanzania mwaka 2008 na kwa sasa nimetuliwa kuwa katibu wa kamati ya
ufundi na Tiba katika Timu ya Maji Maji Fc.
“Kwa sasa nina umri wa miaka 49,nina
mke na watoto 5,ambapo ni mchezaji wa kambalage Veterani pia nina timu yangu
binafsi ya vijana ambayo inaitwa Matogoro Mabatini Fc,anaitimisha Mbopa Luoga
ambaye wakati akicheza awezi kuwasahau mshambuliaji wa Jkt Mafinga Bwana
Mwalami Pamoja na Sande Manala [Computer] ambao walikuwa na uwezo mkubwa
uwanjani.
mwisho
Chapisha Maoni