Kosta magoroso.
Mashabiki na Wadau wengi wasoka hapa
nchini licha ya kupitia katika nyakati tofauti ngumu katika soka la Tanzania
Toka enzi za Jk Nyerere kamwe kuna baadhi ya wanandinga ambao walipata kutikisa
soka la hapa nchini awawezi kuwasahau ,miongoni mwao ni Kosta Magoroso ambaye
alicheza katika kiwango cha juu sana akiwa na Waziri Mkuu Dodoma,Tukuyu Stars
Pamoja na Lipuli Ya Iringa.
Magoroso ambaye ni mzaliwa wa Iringa
mjini Eneo la Mkwawa alianza kusakata kandanda katika shule tofauti za msingi
kutokana na baba yake kuhama hama kikazi ambapo ilisoma katika mikoa ya
Shinyanga ,mbeya ,morogoro,na Iringa katika shule ya Mlangari na baadae nyota
yake iling’ara zaidi akiwa katika masomo ya sekondari.
Magoroso anaeleza baada ya
kumaliza masomo ya sekondari alianza kucheza soka la nguvu akiwa na timu ya
vijana ya iringa mwaka 1986 timu ambayo iliundwa na wachezaji vijana ambao
walisheheni vipaji vya hali ya juu na walifanikiwa kupata majina makubwa na
kutingipsha soka la hapa nchini wakiwa na timu tofauti za ligi kuu.
Baadhi ya wachezaji hao ni Stivin
musa [marehemu],Goerge Kumbemba,Dankani Buti Nini akiwa na reli ya Marogoro
,charamanda saidi [kurugenzi ya Dodoma],pamoja na Daud Kufakunoga [prisons ya
mbeya.wengine ni Jems Mwagama Maji Maji ya Songea,Yusuph Kobe SDA Dodoma pamoja
na Rajabu Juma Ambaye aliweka na reli ya morogoro.
Baada ya kuchezea vijana ya Iringa
kwa mafanikio makubwa mwaka 1987 alisajiliwa na timu ya Waziri Mkuu ya
Dodoma ali ambayo ilipelea nyota yake kuzidi kupea zaidi na kuchaguliwa
katika timu ya Taifa ya vijana kwa kuwa kipaji chake kionekana kwa kila
aliyemwona uwanjani.
Mechi yake ya kwanza katika
michuano ya kimataifa walicheza na timu ya Taifa ya Sheli sheli mchezo ambao
ulimalizika kwa sale ya bao 1-1 yeye akiiswazishia Tanzania katika dakika ya
90, pia mchezo wa pili walicheza na timu ya vijana Ya sheli sheli mchezo ambao
kwa mara nyingine uliisha kwa sare ya bao 1-1 na bao la Tanzania
lilifungwa na Athumani China mara baada ya kupokea Pasi safi toka kwake na
kukwamisha mpira kimiani,ambapo timu hiyo ilienda nchini Usheri sheri Mara
baada ya kuarikwa katika sherehe ya kitaifa ambayo ilifanyika nchini
humo.
Baada ya kucheza timu ya vijana kwa
mafanikio mwaka 1989 alibahatika kuitwa katika timu ya taifa ya Tanzania hali
ambayo ilimfanya apagawe na kujisikia kama yupo peponi kwa kuwa habari za
kujiunga na timu ya taifa kwa mara ya kwa aliambiwa na kaka yake na baadae
akasikia kupitia Magazeti,yeye binafsi aliwanza sana kuhusu kuchaguliwa kwake
na alijifikikilia jinsi ambavyo angecheza na wachezaji wakubwa ambao ailikuwa
akiwasikia kwenye vyombo vya habari,na mara baada ya kujiunpga na timu
alifanikiwa kuwafunika wachezaji wakonge ikiwemo kumnyang’anya namba Selestine
Skinde.
Vile Vile mwaka 1989 alijiunga na
Tukuyu Stars timu ambayo aliitumikia hadi mwaka 1992 na akatimukia timu ya
nyumbani ya Lipuli Fc timu mbayo hakudumu sana na baadae akaitwa na timu yake
ya zamani ya Waziri mkuu Dodoma timu na aliichezea adi mwaka 1996 ambapo
kutokana na kuwa na mapenzi na timu yake ya nyumbani ya Iringa akaamua kurupdi
Lipuli na akacheza hadi mwaka 2000 hapo ndipo akatundi Darga.
Mechi za kimataifa.
“nakumbuka mechi yangu ya kwanza
nikiwa na timu ya Taifa ya wakuwa niliogopa sana kuingia ukwanjani kwa
kuwa mimi nilikuwa ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa na umri mdogo
katika kikosi chetu ambacho kilichuana na timu ya daraja la kwanza toka
Urusi mchezo ambao kocha alinipanga na nilifanikiwa kucheza vizuri hali ambayo
ilipelekea nimnyang’anye namba Selestine Mbunga Skinde.
“ambapo katika mchezo ule ambao timu
ya taifa ya Tanzania ilishinda bao 4-3 nilifanikiwa kufunga bao 2 kwa mikwaju
ya penalti ambazo nilizipiga kwa presha kubwa kwa kuwa wachezaji
wakongwe waliogopa kupiga ili wasiaribu rekodi zao endapo wangekosa zile
penalti,kikubwa mchezo ule ulinijengea uwezo wa kujiamini na
kujituma katika michezo ambayo ilikuja mbele yangu.
“mchezo mwingine ninaoukumbuka ni
Kati yetu Stars na Tmu ya Taifa ya Zambia mwaka 1990 katika michuano ya SADCC,
michuano ambayo Zambia walichukua ubingwa kwa kuzibebesha kapu la magori
timu zote ambazo zilikuwa zikishiriki katika michuano hiyo.
Nakumbuka Tanzania tulichezea
kichapo cha bao 2-0, na Zambia ambayo ilikuwa ikiongozwa na mchezaji
mahili aliyekuwa akisakata kandanda nchini Uholanzi kwa sasa ni Rais wa
shirikisho la soka nchini humo ,michuano ambayo timu yetu haikufanya vizuri.
Imani za kishirikina.
“Zilikuwepo,zipo na zitaendelea
kuwepo imani ambazo kwa muda mwingine zinawafanya wachopezaji wabweteke
badala ya kufanya mazoezi kwa juhudi na maharifa,kunatukio moja lilitokea
uongozi wa timu ambayo nilikuwa nikichezea [jina linaifadhiwa] waliandika
majina ya timu pinzani na kuyapeleka kwa a mganga ambapo mganga
aliyachukua yale majina na akayaweka mdomoni mwa kondoo na Yule kondoo
akafukiwa katikati ya uwanja ili kuwaroga wapinzani wetu.
“Kweli katika mchezo ule tukiwa
katika uwanja wetu wa nyumbani tuliibuka na ushindi wa bao 3-0,vile vile mwaka
1994 kulikuwepo na mechi kati ya Lipuli na wekundu wa msimbazi Simba kitu
ambacho kilitokea katikati ya mchezo nyuki walitanda uwanjani hali ambayo
ilipelekea wachezaji wote na waamuzi kulala chini ya uwanja hadi nyuki
walipoondoka tukio lile mashabiki wa soka waliliusisha na imani za kishirikina
kwa kuwa wale nyuki waliondoka bila kumng’ata mtu yeyote.
Tofauti Kati ya soka la zamani na
sasa.
“sisi wachezaji wa zamani tulikuwa
tunajielewa sisi tulikuwa na kila kitu ambacho mchezaji anatakiwa kuwa
nacho akiwa uwanjani,tofauti na hivi sasa wachezaji wanapewa vitu ambavyo
wanatakiwa kuwa navyo nje ya uwanja wakati uwanjani hawajui ,Tatizo la soka
letu lanzima watu wote wanaohusika na mchezo huo wajtambue na kila mtu
atekeleze majukumu yake ipasavyo kwa manufaa ya soka letu.
Hawezi Kusahau.
“Niliigharimu Tanzania katika
michuano ya Challenge michuano ambayo ilikuwa ikifanyika nchini kenya kwa
kukosa Penalti ambayo ilisasabisha sisi tupoteze mchezo ule kwa bao 2-1 bao la
Tanzania liliwekwa kimiani na Juma mgunda , baada ya kumalizika mchezo ule
niliumia sana lakini makocha pamoja na wachzaji wezangu walinipa moyo na
kunieleza kuwa hata wachezaji wakongwa wanakosa penalti hivyo sio jambo la
ajabu.
Goti lilimtoa Tukuyu Stars.
“Mwaka 1992 nikiwa na tukuyu Stars
niliumia goti katka mchezo dhidi ya Simba mara baada ya kukumbana na Goerge
Masatu eneo la 18 wakati naelekea kufunga baada ya mchezo ule Baba
aliniita kuja kutibiwa Iringa nikaamua kuachana na Tukuyu Stars na
na kurudi iringa na nuikapata matibabu kwa kipindi cha miezi 5,ambapo sikurudi
tena Tukuyu nikamua kujiunga na Lipuli ya ilinga timu ya nyumbani.
“Kikubwa ambacho kilikuja
kunikuta Mara baada ya kuumia goti nilipoteza nafsi ya kuchezea timu ya taifa
ya Tanzania taifa strs kwa sisi kuitwa kwenye timu ya taifa ilikuwa ni fahari
kubwa na heshima ya pekee sana.
Nyota wa sasa Hapa nchini.
“Mrisho Ngasa ni mchezaji wa
pekee sana kwa kuwa bado anacheza katika kiwango cha juu tukilinganisha
na wachkezaji wengi wa sasa wanachuja baada ya muda mfupi.
Mashabiki wanawapa pombe wachezaji.
“kwa kiasi kikubwa soka la Tanzania
linauwawa na mashabiki ingawa hawajitambui,kinachotokea ukiwa unafanya
vizuri mara kwa mara mashabiki wanakuchukua kwenda kukunyesha pombe baa kama
starehe kwao kitu ambacho kinasbabisha wachezaji kushuka viwango vyao kwa kuwa
kuna kipindi mcheaji unajikuta unapata ofa za kunywa pombe na kustarehe
mfurulizo ali ambayo ni hatari sana hasa kwa wachezaj wetu wa sasa ambao
wanapenda sana Starehe.
Ushauri kwa Tanzania /timu za
Iringa.
“yanalalamikiwa mambo mengi sana
lakini pia tunaitaji kuwa na makocha wenye taaluma ya mpira,Tff watoe
mafunzo ya ukocha kwa mikoa yote ili kuwapata makocha wengi wenye
sifa pia TFF waachane na tabia ya kutoa mafunzo kwa kuweka vituo katika
mikoa michache ali ambayo inapelekea washiriki kutumia gharama
kubwa na wengine kukata tama.
“Mkoani Iringa hatuna timu ya ligi
kuu tangu Lipuli iliposhuka daraja miaka 12 iliyopita hali ambayo ni
haibu sana kwa mkoa wenye sifa kama Iringa kukosa timu ya ligi kuu ,tuwaunge
mkono Kurugenzi pamoja na lipuli ili tuweze kuwa na timu ya ligi kuu misimu
ijayo.
Baada ya kustafu soka.
Chapisha Maoni