Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.





Na Alex Mapunda 







 
Aliy Mchumila.
    “Mwaka 1985 Yanga tulicheza na pan-Afrika,nakumbuka wachezaji wa Yanga tulimzonga mwamuzi  kwa kutoridhika  na uchezeshaji wake mimi nilizunguka kwa nyuma na kumpiga kikwenzi  mwamzi pasipo yeye kujua,baada ya mchezo nilijsikia aibu  sana nikamfuata na kumwomba msamaha,akanisamehe kwa dhati”

    Anasimulia Aliy  Mchumilia ambaye nyota yake ilianza kunga’a na  kucheza kwa kiwango kikubwa  miaka ya 1980 hadi 1990 akiwa na RTC-Kagera ,Yanga Africans pamoja Maji Maji ya Songea akiwa kama kiungo mshambuliaji.
     Mchumila mzaliwa wa Wilaya ya Musoma alianza kucheza mpira akiwa shule ya Mwisenge  na kiwango chake kikaonekana kwa watu wengi  katika mashindano mbali mbali ya umitashumta,baadae alijiunga na masomo ya sekondari lakini aliamua kuacha na kujiunga na timu ya  RTC-Msoma  timu ambayo ilikuwa ikishiriki ligi ya mkua, mara baada ya kukosa karo ya shule.
      Mungu sio athumani mwaka 1982 ilisajiliwa na RTC – Kagera  timu ambayo ilikuwa ikishiriki ligi daraja la kwanza [kwa sasa ligi kuu],kiwango chake kilionekana zaidi akiwa na timu hiyo katika mchuano ya ligi kuu kituo cha mwanza ambacho kilikuwa kikiusisha timu Za Simba Sc,Rtc-kagera,cop United  pamoja  na CDA ya Dodoma  ambapo mwaka 1983 alipata nafasi ya kuchezea timu ya Taifa ya Tanzania kwa mara ya kwanza na kufanikiwa kuichezea kwa kiwango cha hali ya juu.
   Yanga walimwona akiwa na timu ya Taifa wakampa mkataba  na yeye akasaini moja kwa moja kwa kuwa toka akiwa mtoto alikuwa na ndoto ya kuchezea yanga kwa vile alikuwa akiipenda toka Moyoni,Mwaka 1987 yeye na wenzake akiwemo Idd Chama,Omari Husain pamoja na Aran Shomari waliamua kutimukia Maji Maji ya Songea mara baada ya kuibuka  kundi la Yanga Ukuta  ndani ya Yanga hali ambayo iliwachanganya wachezaji wengi  na kila upande ulitaka kusajili wachezaji wake.
     Alicheza kwa mafanikio akiwa na wanalizombe  kiasi kwamba alipata nafasi ya kuteuliwa kama timu meneja  akiwa bado kama mchezaji na kufikia mwaka 1991 hadi 1993 alibaki Maji Maji akiwa kama Meneja wa Timu .

   Kama waswahili wasemavyo uchungu wa mwana aujua  mzazi basi baba yake alijisikia mpweke kuishi mbali na mtoto wake na akamua kumrudisha Musoma hali ambayo yeye aliridhia na akaachana na Maji Maji na kurudi nyumbani kwa mkono wa baraka toka uongozi wa Maji Maji .
   Akiwa Musoma aliamua kujiunga na timu ya Maji Mara, timu ambayo aliichezea adi mwaka 1997 hapo ndipo aliamu kulipa kisogo soka.Anasimulia Mchumila Kisha anaendelea;-
Gormahia  walinipa namba Yanga.
  Mwaka 1985 yanga tulikiputa na Gormahia ya Kenya michuano ya club bingwa afrika   kipindi hicho mimi sikuwa na namba ya kudumu, nakumbua Yanga ilikuwa ikiongozwa na kocha Bad Sarehe [Marehemu] wakati huo pia walikuwa na kocha mzungu ambaye bado halikuwa hajakabidhiwa timu rasmi kutokana na vibali vya kufundisha soka hapa mchini vilikuwa bado ila alikuwa akija mazoezini kwa kuibia na hata siku ya mchezo hakukaa jukwaani.
   Katika mchezo huo  wapinzani wetu walikuwa mbele kwa bao 1-0,Yule kocha mzungu kuona vile aliamua kufanya mawasiliano ya siri na kocha Bad Sarehe ili waniingize kwenda kuokoa Jahazi,kitu ambacho walikisikia na wakamtoa kepteni  marehemu Juma mkambi mimi nikachukua mikoba yake, kweli sikufanya hajinzi nilicheza kwa kujituma sana adi nikafanikiwa kusawazisha bao mbele ya Wakenya na kuazia siku ile nikawa tegemeo katika timu ya Yanga.
Kikosi tishio Jangwani mwaka 1983 -85.
   Kikosi cha yanga kiliundwa na wachezaji ambao tulikaa kambini kwa muda mrefu sana na kilisheheni mastaa ambao tulikuwa tishio hapa nchini,Nakumbuka alikuwepo Joseph Fungo,yusufu Ismail [marehemu],Ahamed Amasha marufu kama Mathematics,Aran Shomari Pamoja na Athumani Juma Chama a.k.a Jogoo.
    Wengine ni Marehemu Juma Mkambi [Jenerali],mimi mwenyewe,Charles Boniface Mkwasa ,makumbi Juma maarufu kama homa ya jiji,Omari husein bila kumsahau Juma Rashid Rampara, kikosi ambacho kilikuwa tishio Afrika mashariki na kati.
Ushirikina
     Wakati nikiwa Maji Maji kama Meneja  nakumbuka Tulimsajili Mzee wa kamati ya ufundi  nje ya uwanja toka Afrikan Sports Mzee ambaye wao aliwapa ubingwa,kiukweli  toka nimezaliwa sikuwai kutana na mzee kama Yule alikuwa na uwezo mkubwa sana na mara zote kabla ya mchezo alikuwa na uwezo wa kusimulia kila tukio ambalo litatokea katika mchezo  hali ambayo ilitupa kiburi cha sisi kucheza kwa kujiamini sana.
   Nakumbuka kuna mechi tulienda kucheza na Yanga Jijini Dar es salam mchezo ambao ilikuwa mgumu sana kwetu  lakini Yule mzee wiki moja kabla alituambia  kuwa  Yanga Tutawafunga Bao 1-0 na kusisitiza kuwa hakuna mshambuliaji hata mmoja ambaye angefunga bao kwa upande wetu ila bao litafungwa na beki na aliniagiza nitoe taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa  Yanga tutawakaanga bao moja  hali  ambayo sikuifanya kwa kuwa ilikuwa mapema sana.
     Tuliondoka Siku ya Jumatatu kuelekea jijini Dar es salam  na tulilala Iringa tukiwa njiani  Yule mzee aliangalia kwenye rada zake na akasema kuwa bao bado ni moja halijabadilika hadi tulipoingia Jijini dar alizidi kusisitiza na siku ya mchezo kwenye kikao cha asubuhi [FREE MATCH MEETING] aliniagiza nikawatambie yanga kuwa tutawafunga bao moja nilifaya hivyo lakini yanga walitudharau sana .
    Mchezo ulikuwa mgumu sana kwa pande zote lakini mimi na viongozi wenzangu tulijiamimi sana kwa kuwa mtaalaum Alisha tuambia matokeo ya mchezo ambapo kama alivyosema Yule Mzee beki wa Maji Maji Piter Mhina aliwafunga midomo mashabiki wa wa yanga kwa kufunga bao safi ambalo lilidumu hadi dakika  90 za mchezo zipokamarizika.
    Kikubwa ambacho kilitokea katika mchezo ule mwamuzi aliwapa kwa makusudi Offside tatu za wazi za kufunga mabao lakini zote ziliokolewa na Kisochi lamba kwa  Mbwembwe kwa vile nae alikuwa anajua kuwa kwenye mchezo ule haliwezi kupatkana bao linguine zaidi ya lile ambapo hata viongozi hatukutoa malalamiko yeyote  kwa vile matokeo ya mchezo tulikuwa tukiyafahamu wiki moja Kabla.
Tofauti ya soka la sasa na zamani.
    Wachezaji wanadhani kucheza mpira ni kujifaya mastaa mtaani pasipo kuonyesha uwezo uwanjani,na kikubwa  hawajitambui kama Sisi tulivyokuwa tukicheza zamani wasipobadilika soka letu bado litabaki kuwa chini.
Bao kali
    Mwaka 1984 yanga tulicheza na Kill tex ya Arusha mchezo ambao  nilifunga bao la ushindi kwa kisigino mara baada ya kupokea pasi safi toka winga ya kulia na mimi nilikuwa katikati ya msitu wa mabeki  skuitaji kugeuka moja kwa moja nikapasia wavu kwa kisigino.
Anayemkubali
      Mmbwana Samatta Popa  amefanikiwa  kuandika rekodi ya pekee kwa sasa na kung’arisha soka letu ,kutoka moyoni naeshimu sana mchango wake.
Ushauri kwa Soka letua/ Mara
     Soka la mara linaitaji mshikamano wa hali ya juu sana ili tuweze kufanya vizuri Mimi najisikia Uchungu  sana,Rais mpya wa TTF atekereze kwa dhati yale yote ambayo alituhaidi katika  kampeni zake,kwa mkoa kama wetu kukosa ligi kuu ni tatizo kubwa viongozi wa Mara hawathamini mchango wa wachezaji wa zamani,kweli nimeamini Nabii hakubariki kwako.
      Kuna kipindi nilikuwa kocha wa timu ya polisi mara timu ilikuwa na memwekeo mzuri lakini uongozi wa timu wakamleta kocha ambaye alikuja kuyumbisha timu,mimi naamini ufahamu wangu katika mpira ni mkubwa  kama nitahaminiwa pamoja na wakongwe wenzangu tatainua mkoa wetu kisoka.
Baada ya kustaafu Soka.
     Kwa sasa mimi ni kocha,pia nafanya shughuri zangu za kawaida na zaidi ni mchezaji wa Veterani Mara nina mke na watoto 6,anahitimisha Aliy Mchumila  ambaye awezi kumsahau marehemu Karoje Machera [Simba] beki ambaye alimtoa sana jasho uwanjani.
mwisho.


Chapisha Maoni