Na Sophia Mwaipyana ,Mbeya
Maisha ni safari ndefu
ambayo binadamu tunasafiri huku hatujui safari hiyo inaishia wapi ikiwa
imeambatana na mipango mingi ambayo kila binadamu anatamani ifanikiwe ilikuweza
kumwaongezea nguvu ya safari yake lakini kunawakati tunakutana na vikwazo vingi
ambavyo vinaweza kufanya ukakata tama lakini tunaambiwa kukata tamaa nisawa na
kujiroga mwenyewe.
Bahati Mwaipopo alikuwa na
mipango mingi aliyo tamani kutimiza kupitia soka lakini alikutana
na vikwazo vingi hali iliyo pelekea lengo lake la kupata kazi kupitia soka
kugonga mwamba.
JELAMBA ilifanikiwa kufanya naee mahojiano kuhusu maisha yake ya
soka ambapo aliatufahamisha kuwa alianza kucheza soka toka akiwa darasa
la tano katika shule ya msingi Mbalizi hadi mwaka 1987 akiwa shule ya
sekondari Kipoke aliiwakirisha nyanda za juu kusini katika mashindano ya
Umisenta taifa yaliyo fanyika mkoani Shinyanga .
Timu yake ya kwanza
kuichezea ni timu ya Young Stars ya Mbalizi mwaka 1989 -1991 na mwaka
1993 aliichezea timu ya Benki kuu na mwaka 1994 -1996 aliichezea
timu ya Ujenzi Rukwa na mwaka 1997 aliichezea Tukuyu Stars hadi mwaka
1998 alihamia katika timu ya 44kj iliyokuwa mbalizi ni timu ya jeshi.
Kwanini Tukuyu Stars hukudumu
“Kipindi kile mpira ulikuwa
haulipi kama sasa kwahiyo lengo langu kubwa nilikuwa nataka nipate timu ya
jeshi ili nipate kazi na ndiyo maana nikaenda katika timu ya jeshi lakini
bahati mbaya zaidi sikuweza kutimiza ndoto yangu ya kuingia jeshini kupitia kipaji
changu”
Mechi ngumu kwako
“Ni ile mechi ya mwaka 1995
Ujenzi na Yanga mwaka huo Yanga ilikuwa inaitwa Yanga Kampara kwasababu
walikuwa wametoka kuchukua ubingwa Uganda na mechi hiyo tulifungwa goli
nne na mechi ilikuwa ngumu sana kwetu kutokana na timu hiyo
kusheheni wachezaji wazuri”
Tukio gani ambalo huwa
halisahau
“nimatukio kama mawili hivi
huwa siyasahau katika maisha yangu lakwanza ni ile ajari ya basi mwaka
1992 nikiwa naichezea Benki kuu tulikuwa tunaenda Tabora kucheza na
Polisi Tabora”
“Tulipofika kijiji kimoja
kinaitwa Kasulu dereva alikuwa katika mwendo kasi gafla akaona mtu mbele sasa
ile anataka kumkwepa gari likahama njia ila namshukuru mungu wachezaji
tulipata majeraha tuu hakuna aliye poteza kiungo wala maisha”
“chakushangaza hata
tulipofika Tabora waligoma kutusogezea mechi kwahiyo tulicheza hivyo hivyo na
tukatoka sale ya goli moja’
‘Pia mwaka 1996 nikiwa
ujenzi nakumbuka tulienda kucheza mechi na timu ya Waziri mkuu Dodoma
tulikaa siku nne tukiwa tumeishiwa pesa yakula hadi pesa ya kuweka mafuta
katika gari ili kurudi Rukwa’
“Kwahiyo wachezaji tukawa
hatuna chakula wale wenye uwezo tulikuwa ukimchukua mchezaji mmoja
unaenda naye kula chakula cha mchana jioni tena unaenda kula na
chezaji mwingine”
“Alitokea msamaria mmoja
ambaye ni mkazi wa Sumbawanga akatupa pesa ya kujaza mafuta ambayo
yatatufikisha Mbeya kwahiyo tulipofika Mbeya mimi nikaisafirisha timu na
nikaenda kurudishiwa pesa tulipo fika Sumbawanga”
Kwanini ujenzi ilipoteza
mwelekeo
“Unajua mkuu wa mkoa kipindi
kile timu inafanya vizuri mkuu wa mkoa alikuwa Chrisanti Mzindakaya kwahiyo
alikuwa anaipa sapoti sana timu pamoja na Padri Msakira kwani ilikuwa hadi
kambi tunaweka misheni wakati mwingine chini ya usimamizi wa padri”
“kwahiyo shida ilikuja pale
Mzindakaya alipo hamishwa na kuja mkuu wa mkoa mwingine ambaye alikuwa hapendi
michezo kwahiyo shida ilianzia hapo timu ikayumba mishahara ikawa hakuna tena
wachezaji tukaweka mgomo na wakatuambia asiye taka aondoke mimi na wenzangu kama
watatu tuliondoka”
Ushirikina katika soka
“Ushirikina upo sana
sema kuna utofauti kila timu ina utaratibu wake timu nyingine wanafanya
viongozi na nyingine hadi wachezaji mnashirikishwa ,mfano kuna wakati wachezaji
tulikuwa tunaamshwa usiku tunaenda kuchezeshwa mpira makaburini”
‘Nakumbuka
kunasiku tulikua tunacheza Iringa katika uwanja wa
Samora sikuhiyo mimi nilikuwa ndiyo kapteni kwahiyo kabla ya mechi wakati
wenzetu wanavaa mimi na golikipa tulitolewa na kupelekwa mto Lwaha ‘
“Tulipo fika kule nilipewa
njiwa nimnyonge njiwa huyo alikuwa amefungwa sanda nyeusi nikamnyonga alafu
nikaambiwa nimtupie katika mto huku nikinuwiza baada ya hapo tukaondoka kwenda
uwanjani”
“Lakini chaajabu tulipo fika
uwanjani mechi ilikuwa ngumu sana na tulifungwa goli 3-1
kwahiyo ushirikina katika soka upo sana ila hauna faida yoyote zaidi ya
kupoteza mwelekeo wa timu kwasababu mkiamini sana hiyo imani ndiyo
pale mtapoteza mechi nyingi sana”
Kwanini ushindani kipindi
hiki ni mdogo
“Timu zote iliifanye vizuri lazima iwe na
wadhamini kwahiyo tunaona kwasasa wadhamini wamebaki tu katika timu za
dar-es-saalm na ndiyo timu hizo zinakuwa na ushindani mkubwa kwasababu
wachezaji wanapata mahitaji yote kwa wakati’
“Kwahiyo hali hii inaziathili
sana timu zetu za mikoani ukiangalia zamani timu nyingi zilikuwa zinawadhamini
wake ukiangalia Mecco ilikuwa chini ya shirika la ujenzi yani timu nyingi
zilikuwa na wadhamini wao hasa mashirika binafsi”
“lakini sahizi tunaona
mabadiriko kwa huyu mdhamini ambaye ameanza kuja hadi mikoani kuwadhamini
Mbeya City na Ndanda Fc kwahiyo wadhamini wajitokeze ilituweze kuongeza
ushindani katika ligi yetu ‘
“Zamani timu nyingi zilikuwa
zinachukuwa ubigwa kutokana na hilo lakini kwasasa tunabaki tu simba
Yanga unaona mfano safari hii mabigwa ni Azam kwanini sababu wanamdhamini
wao ambaye ameifanya timu ilete mabadiriko katika ligi kuu”
Mafanikio
“Kama nilivyo kwambia zamani
mpira ukipata mafanikio makubwa nikupata ajira siyo vinginevyo zaidi zaidi ni
kutembea Nchi nzima na kufahamika”
Mchezaji gani
unaempenda hapa Tanzania
“Ni Canavaro Yule
nimchezaji sababu kiwango chake hakishuki na hana utani akiingia uwanjani
hata kama nimechi ya kirafiki, pia ni mchezaji ambaye anacheza nafasi
niliyokuwa nacheza mimi”
Wachezaji unao wakumbuka ulio
cheza nao
“nikiwa ujenzi ni Atupele
Mapungiro na nikiwa 44kj ni sajigwa jamaa alikuwa mvumilivu sana katika mazoezi
na alikuwa na bidii”
Ushauri wako
“Mimi ushauri wangu ni kwa mashabiki
wa Mbeya tuzipe sapoti timu zote ilizote ziweze fanya vizuri sasa
tukiegamia upande mmoja je siku hiyo timu tunayo itegemea isipo fanya
vizuri itakuwaje, tukumbuke Prisons ndiyo timu toka zamani ilikuwa
inatuwakirisha katika soka”
Familia
“nina familia ya watoto sita
ila kati yao namuona mwanangu Girbet ndiye atarithi kipaji changu kwani
nyota njema huonekana asubuhi “
Maisha ya sasa
“Sahizi ni mjasiriamari napia
naichezea timu ya maveterani ya Mbalizi na ninaishi huko katika mji mdogo
wa Mbalizi,na sitegemei kuacha kabisa kucheza soka kwasababu napenda
niupe mwili wangu mazoezi”
Chapisha Maoni