|
||||
Aliy Mchumila.
“Mwaka 1985 Yanga
tulicheza na pan-Afrika,nakumbuka wachezaji wa Yanga tulimzonga mwamuzi
kwa kutoridhika na uchezeshaji wake mimi nilizunguka kwa nyuma na kumpiga
kikwenzi mwamzi pasipo yeye kujua,baada ya mchezo nilijsikia aibu
sana nikamfuata na kumwomba msamaha,akanisamehe kwa dhati”
Anasimulia
Aliy Mchumilia ambaye nyota yake ilianza kunga’a na kucheza kwa
kiwango kikubwa miaka ya 1980 hadi 1990 akiwa na RTC-Kagera ,Yanga
Africans pamoja Maji Maji ya Songea akiwa kama kiungo mshambuliaji.
Mchumila
mzaliwa wa Wilaya ya Musoma alianza kucheza mpira akiwa shule ya Mwisenge
na kiwango chake kikaonekana kwa watu wengi katika mashindano mbali mbali
ya umitashumta,baadae alijiunga na masomo ya sekondari lakini aliamua kuacha na
kujiunga na timu ya RTC-Msoma timu ambayo ilikuwa ikishiriki ligi
ya mkua, mara baada ya kukosa karo ya shule.
Mungu
sio athumani mwaka 1982 ilisajiliwa na RTC – Kagera timu ambayo ilikuwa
ikishiriki ligi daraja la kwanza [kwa sasa ligi kuu],kiwango chake kilionekana
zaidi akiwa na timu hiyo katika mchuano ya ligi kuu kituo cha mwanza ambacho
kilikuwa kikiusisha timu Za Simba Sc,Rtc-kagera,cop United pamoja
na CDA ya Dodoma ambapo mwaka 1983 alipata nafasi ya kuchezea timu ya
Taifa ya Tanzania kwa mara ya kwanza na kufanikiwa kuichezea kwa kiwango cha
hali ya juu.
Yanga walimwona akiwa
na timu ya Taifa wakampa mkataba na yeye akasaini moja kwa moja kwa kuwa
toka akiwa mtoto alikuwa na ndoto ya kuchezea yanga kwa vile alikuwa akiipenda
toka Moyoni,Mwaka 1987 yeye na wenzake akiwemo Idd Chama,Omari Husain pamoja na
Aran Shomari waliamua kutimukia Maji Maji ya Songea mara baada ya kuibuka
kundi la Yanga Ukuta ndani ya Yanga hali ambayo iliwachanganya
wachezaji wengi na kila upande ulitaka kusajili wachezaji wake.
Alicheza
kwa mafanikio akiwa na wanalizombe kiasi kwamba alipata nafasi ya
kuteuliwa kama timu meneja akiwa bado kama mchezaji na kufikia mwaka 1991
hadi 1993 alibaki Maji Maji akiwa kama Meneja wa Timu .
Kama waswahili
wasemavyo uchungu wa mwana aujua mzazi basi baba yake alijisikia mpweke
kuishi mbali na mtoto wake na akamua kumrudisha Musoma hali ambayo yeye
aliridhia na akaachana na Maji Maji na kurudi nyumbani kwa mkono wa baraka toka
uongozi wa Maji Maji .
Akiwa Musoma aliamua
kujiunga na timu ya Maji Mara, timu ambayo aliichezea adi mwaka 1997 hapo ndipo
aliamu kulipa kisogo soka.Anasimulia Mchumila Kisha anaendelea;-
Gormahia walinipa namba Yanga.
Mwaka 1985 yanga tulikiputa
na Gormahia ya Kenya michuano ya club bingwa afrika kipindi hicho
mimi sikuwa na namba ya kudumu, nakumbua Yanga ilikuwa ikiongozwa na kocha Bad
Sarehe [Marehemu] wakati huo pia walikuwa na kocha mzungu ambaye bado halikuwa
hajakabidhiwa timu rasmi kutokana na vibali vya kufundisha soka hapa mchini
vilikuwa bado ila alikuwa akija mazoezini kwa kuibia na hata siku ya mchezo
hakukaa jukwaani.
Katika mchezo huo
wapinzani wetu walikuwa mbele kwa bao 1-0,Yule kocha mzungu kuona vile
aliamua kufanya mawasiliano ya siri na kocha Bad Sarehe ili waniingize kwenda
kuokoa Jahazi,kitu ambacho walikisikia na wakamtoa kepteni marehemu Juma
mkambi mimi nikachukua mikoba yake, kweli sikufanya hajinzi nilicheza kwa
kujituma sana adi nikafanikiwa kusawazisha bao mbele ya Wakenya na kuazia siku
ile nikawa tegemeo katika timu ya Yanga.
Kikosi tishio Jangwani mwaka 1983
-85.
Kikosi cha yanga
kiliundwa na wachezaji ambao tulikaa kambini kwa muda mrefu sana na kilisheheni
mastaa ambao tulikuwa tishio hapa nchini,Nakumbuka alikuwepo Joseph
Fungo,yusufu Ismail [marehemu],Ahamed Amasha marufu kama Mathematics,Aran
Shomari Pamoja na Athumani Juma Chama a.k.a Jogoo.
Wengine ni
Marehemu Juma Mkambi [Jenerali],mimi mwenyewe,Charles Boniface Mkwasa ,makumbi
Juma maarufu kama homa ya jiji,Omari husein bila kumsahau Juma Rashid Rampara,
kikosi ambacho kilikuwa tishio Afrika mashariki na kati.
Ushirikina
Wakati
nikiwa Maji Maji kama Meneja nakumbuka Tulimsajili Mzee wa kamati ya
ufundi nje ya uwanja toka Afrikan Sports Mzee ambaye wao aliwapa
ubingwa,kiukweli toka nimezaliwa sikuwai kutana na mzee kama Yule alikuwa
na uwezo mkubwa sana na mara zote kabla ya mchezo alikuwa na uwezo wa kusimulia
kila tukio ambalo litatokea katika mchezo hali ambayo ilitupa kiburi cha
sisi kucheza kwa kujiamini sana.
Nakumbuka kuna mechi
tulienda kucheza na Yanga Jijini Dar es salam mchezo ambao ilikuwa mgumu sana
kwetu lakini Yule mzee wiki moja kabla alituambia kuwa Yanga
Tutawafunga Bao 1-0 na kusisitiza kuwa hakuna mshambuliaji hata mmoja ambaye
angefunga bao kwa upande wetu ila bao litafungwa na beki na aliniagiza nitoe
taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa Yanga tutawakaanga bao moja
hali ambayo sikuifanya kwa kuwa ilikuwa mapema sana.
Tuliondoka
Siku ya Jumatatu kuelekea jijini Dar es salam na tulilala Iringa tukiwa
njiani Yule mzee aliangalia kwenye rada zake na akasema kuwa bao bado ni
moja halijabadilika hadi tulipoingia Jijini dar alizidi kusisitiza na siku ya
mchezo kwenye kikao cha asubuhi [FREE MATCH MEETING] aliniagiza nikawatambie
yanga kuwa tutawafunga bao moja nilifaya hivyo lakini yanga walitudharau sana .
Mchezo ulikuwa
mgumu sana kwa pande zote lakini mimi na viongozi wenzangu tulijiamimi sana kwa
kuwa mtaalaum Alisha tuambia matokeo ya mchezo ambapo kama alivyosema Yule Mzee
beki wa Maji Maji Piter Mhina aliwafunga midomo mashabiki wa wa yanga kwa kufunga
bao safi ambalo lilidumu hadi dakika 90 za mchezo zipokamarizika.
Kikubwa ambacho
kilitokea katika mchezo ule mwamuzi aliwapa kwa makusudi Offside tatu za wazi
za kufunga mabao lakini zote ziliokolewa na Kisochi lamba kwa Mbwembwe
kwa vile nae alikuwa anajua kuwa kwenye mchezo ule haliwezi kupatkana bao
linguine zaidi ya lile ambapo hata viongozi hatukutoa malalamiko yeyote
kwa vile matokeo ya mchezo tulikuwa tukiyafahamu wiki moja Kabla.
Tofauti ya soka la sasa na zamani.
Wachezaji wanadhani
kucheza mpira ni kujifaya mastaa mtaani pasipo kuonyesha uwezo uwanjani,na
kikubwa hawajitambui kama Sisi tulivyokuwa tukicheza zamani
wasipobadilika soka letu bado litabaki kuwa chini.
Bao kali
Mwaka 1984 yanga
tulicheza na Kill tex ya Arusha mchezo ambao nilifunga bao la ushindi kwa
kisigino mara baada ya kupokea pasi safi toka winga ya kulia na mimi nilikuwa
katikati ya msitu wa mabeki skuitaji kugeuka moja kwa moja nikapasia wavu
kwa kisigino.
Anayemkubali
Mmbwana Samatta Popa amefanikiwa kuandika rekodi ya pekee kwa sasa
na kung’arisha soka letu ,kutoka moyoni naeshimu sana mchango wake.
Ushauri kwa Soka letua/ Mara
Soka la
mara linaitaji mshikamano wa hali ya juu sana ili tuweze kufanya vizuri Mimi
najisikia Uchungu sana,Rais mpya wa TTF atekereze kwa dhati yale yote
ambayo alituhaidi katika kampeni zake,kwa mkoa kama wetu kukosa ligi kuu
ni tatizo kubwa viongozi wa Mara hawathamini mchango wa wachezaji wa
zamani,kweli nimeamini Nabii hakubariki kwako.
Kuna
kipindi nilikuwa kocha wa timu ya polisi mara timu ilikuwa na memwekeo mzuri
lakini uongozi wa timu wakamleta kocha ambaye alikuja kuyumbisha timu,mimi
naamini ufahamu wangu katika mpira ni mkubwa kama nitahaminiwa pamoja na
wakongwe wenzangu tatainua mkoa wetu kisoka.
Baada ya kustaafu Soka.
Kwa sasa
mimi ni kocha,pia nafanya shughuri zangu za kawaida na zaidi ni mchezaji wa
Veterani Mara nina mke na watoto 6,anahitimisha Aliy Mchumila ambaye
awezi kumsahau marehemu Karoje Machera [Simba] beki ambaye alimtoa sana jasho
uwanjani.
mwisho.
Chapisha Maoni