Mwandishi Alex Mapunda.
Isihaka Majaliwa Kabeya.
UKIITAJA Maji Maji ya miaka
ya 1983-1998 ambayo ilikuwa tishio kwa soka la Tanzania , bila shaka
lazima utamkumbuka Isihaka Majaliwa Kabena ambaye yumo katika orodha ya makipa
ambao walikuwa na uwezo mzuri wa kulinda lango hapa nchini.
Majaliwa ambaye ni mzaliwa wa
Mihomboni , Iringa Mjini ni mtoto wa 12 kati ya watoto 14 kwa Mama Mmoja
alibahatika kuzaliwa mwaka ambao Tanganyika ilipata uhuru toka kwa mwingereza
[1961] ambapo amezugumzia hisitoria yake ya
“Nilianza kucheza soka Darasa la
Tano katika shule ya msingi Mwembetogwa Iringa Mjini,ambapo watu wengi walianza
kukiona kipaji changu kutokana na umahili ambao nilionesha pindi nilipokuwa
langoni.
“Baada ya kumaliza shule ya
msingi, mwaka 1976 nilijiunga na Afrikani Wanderers ya Iringa timu ambayo
ilikuwa inashiriki mashindano ya mkoa huko ndiko nilianza kucheza soka la
ushindani katika timu ambayo niliduma kwa misimu miwili,ila 1979 timu
ya reli ya Iringa ikanisajili na kufanikiwa kucheza kwa mafanikio
makubwa.
“Kutokana na kujituma na uwezo niliounyesha
mwaka 1983 nikatua Maji Maji ya Songea nikiwa hapo nyota yangu iling’aa zaidi
na kiwango changu kuimalika zaidi kwa kuwa nikiwa na timu hiyo tulifanikiwa
kuchukua ubingwa hapa wa kombe la muungano mara mbili mfurulizo ,na baada
ya kucheza na wanalizombe kwa muda mrefu hatimaje mwaka 1989 nikarudi nyumbani
Iringa kutumikia Timu Ya Mazao ya shirika la usagishaji Tanzania hata
hinyo mwaka 1991 nikaachana na mambo ya soka na kujikita na kilimo ambacho
naendelea nacho adi leo.
Hakucheza Simba,Yanga.
“Toka nilipoanza kucheza soka sikuwa
na ndoto za kuchezea timu za Simba na yanga kwa kuwa kipindi hicho Timu
ya Maji Maji ilikuwa kubwa na ilikuwa inaudumia wachezaji kuliko Timu zingine
hapa nchini .
Llakini pia kuna ushauri niliupata
toka kwa Sadi Ali ambaye aliwai chezea Timu ya Simba pindi nilipokuwa
Afrikani Wanderers, kuwa nisijiunge na timu hizo hata kama nikipata nafasi ila
hakuniambia kwa nini,lakini hata hivyo sikupata nafasi za kuzichezea Timu hizo.
Stasahau
Mwaka 1983 kulikuwepo na mechi kali
sana kati yetu na Simba toka jijini Dar es salam mechi hile ilichezwa wakati
kamati ya ufundi ya Simba ilikuwa inaongozwa na kikosi ambacho kilikuwa kimesheni
vichwa toka Brazil na wakati tunakutana nao Simba ilikuwa imezindua mfumo mpya
wa kibrazili maarufu Kama ‘Kanivo Samba’ hakika simba ile ilikuwa inatisha.
“Lakini kilichotokea uwezi
kuhamini lakini itabidi uhamini kwa kuwa ndivyo ilivyotokea,na nikiwa kama
mlinda mlango Namba 1 wa timu yetu Viongozi wakanichukua na kunipeleka
kwa Mganga wa jadi ambaye sasa ni Marehemu ili kuchukua mbinu za
kuidhibiti Simba.
“Wakati wa asuhuhi nakumbuka
mganga aliniambia kuwa, mechi itakuwa ngumu sana kutokana na uimala wa wapinzani
wetu,usiku wa leo nimejitaidi kuokoa magoli mengi sana kadili ya uwezo wangu
lakini hata hivyo yamebakia magoli mawili ambayo nitayamalizia uwanjani wakati
mechi ikiendelea.
“Wakati wa mchezo ulipowadia timu
zote zikaingia uwanjani na mechi ikaanza,mechi ilikuwa ngumu sana na Simba
walipata bao 2 za wazi lakini waamzi wa mchezo ule wakayakataa na kusema
wafungaji waliotea[off side] na hadi mwisho wa mchezo tukatoshana nguvu
ya bila kufungana.
“Hapo ndipo nilipokumbuka maneno ya
mganga,kwa kweli siwezi kusahau ni tukio ambalo lilinitokea moja kwa moja
nikiwa na timu ya Maji Maji.
Mechi ninayokumbuka
“Mechi kati ya Mji Maji ya
Songea na CDA Dodoma mechi ambayo tuliibuka na ushindi wa bao 1-0 bao
ambalo ligubikwa na utata mkubwa hadi ikasababisha mechi kusimama kwa takribani
dakika 14,na mwamzi wa pambano lile Mzee Dastan Daffa na mwamzi wa Pembeni Amed
yasni kutoka Mpwapwa wakuamru mpira uende kati kati wakimaanisha ni goli.
“Lakini ukweli wenyewe mpira ambao
ulipigwa na Madaraka Suleiman toka winga ya kulia ulitoboa wavu wa pembeni kwa
nje na kutumbukia ndani ambapo waamuzi walipoona wavu unatikisika na mpira upo
ndani wakajua moja kwa moja ni goli na hadi mwisho wa mchezo maji maji moja CDA
sifuri.
Mechi ya kimataifa
“Ulikuwa ni mchezo wa kimataifa kati
yetu na Mofulila Wanderers toka mchini Zambia hatua ya makundi michuano ya Afrika
mashariki,katika mechi hiyo jopo la waamzi wakiwemo mmjo toka Malawi na
mmoja toka Zazibar waliufuata uongozi wa maji maji wakiitaji Takrima kwa ajili
ya kuipa msaada timu yetu wakati wa mchezo lakini,kutokana na aliyekuwa
kiongozi wa yanga Isa Makongoro kufungiwa Maisha kwa kosa la Rushwa
uongozi wa Maji Maji ukakataa kutoa chochote kwa msaada wa timu yetu.
“Tukio lile lilifanya jopo la waamzi
lilikasirika sana na wakahaidi kuifanyia ukatili maji maji wakati wa mchezo na
ndivyo ilivyotokea ambapo mchezo ulikuwa mgumu sana kwa maji maji na kila
timu yetu ilichokifanya kilionekana kibaya huku faulo zikiwa nyingi na muda
wote washabuliaji wa maji maji walikuwa wakiunasa mpira basi ni [off side na
hadi mwisho wa mchezo Tulifungwa Bao 2-1 na kutupwa nje.
Makocha wa kigeni na Wazawa
“Tatizo la hapa nchini makocha
wazawa wanapuuzwa tofauti na makocha wa kigeni ambao wanapewa kila kitu
wanachoitaji ,kama makocha wenyeji wangewezeshwa kama wa kigeni soka letu
lingekuwa na ushindani toka kwenye ngazi za chini.
“Tff na vilabu vyetu lazima
zizingatie hilo mimi sioni kitu cha ajabu ambacho wanakifundisha makocha wa
kigeni ambacho wazawa wamekikosa.
Ushauri kwa Watanzania
“Lazima lazima tuwe wavumilivu
tusipende kupanda na kuvuna wakati huo huo, lazima tuwe wavumilivu kwa kujenga
soka letu huku Tukijikita Zaidi kwa Soka la Vijana,na kuepuka Siasa katika
soka.
Wachezaji wanaomkosha.
“mimi binafsi namkubari sana kiungo
wa yanga Frenk Domayo ambaye amefanikiwa kumwamisha namba Haruna Niyozima
mchezaji wa kimataifa toka nchini Rwanda pia Mtanzania anayekiputa soka la
kulipwa nchini Kongo mbwna Samatta ni wanacheza Vizuri.
Baada ya Soka.
“ Toka mwaka 1991 nilianza kazi ya
kilimo ambayo hadi hii leo inanifanya mimi na familia yangu kuendesha
maisha yetu ya kila siku lakini Soka zaidi ya kufahamika na kujuana na watu
sikufaidika na lolote zaidi kupata posho ambayo haikututosheza kwa wachezaji wa
kipindi kile ikilinganishwa na wachezaji wa sasa”,Huyo ndiye majariwa ambaye
amekili wazi kuwa wakati akicheza alikuwa akinyanyaswa na Zamoyoni Mogera.
mwisho
Chapisha Maoni