Na Alex Mapunda[mwandishi]
Stivin Mapunda
Stivini mapunda [Garrincha] ni
miongoni mwa washambuliji hatari sana ambao wamewai tokea hapa nchini na
akafanikiwa kutikisa soka la Tanzania kuanzia mwaka 1997-2005.akichezea timu
ya Maji Maji ya Songea ,Wekundu wa Msimbazi ‘Simba’ na Timu ya Taifa
[99-2005]
Garrincha alianza kucheza soka toka
shule ya msingi Hanga, Darasa la tatu akiwa na miaka 9 na akiwa sekondari alifanikiwa
kushiriki michuano mbali mbali ya shule pamoja na Umiseta hadi ngazi ya Taifa
ambapo kipaji chake kikaonekana na kuanza kung’ara nchi zima.
katika kipindi hicho akiwa shule ya
msingi Garricha alipata nafasi ya kwenda kucheza soka Ulaya kupitia kwa mzungu
aliyekuwa kocha wa maji maji wakati huo ambaye alikiona kipaji chake wakati
timu hiyo ilikuwa ikiweka kambi mara kwa mara huko Hanga, lakini baba
yake alikataa kutokana na kuofia usalama wa mwanao kwa kuwa alitaka
mwanao asiende mbali nae.
“Kocha wa maji maji kipindi hicho
toka Toka barani Ulaya alitaka kunichukua ili nikasome ulaya Pamoja na
kuendeleza kipaji changu cha Soka baada ya kukiona kipaji changu shuleni Hanga
wakati wao walipokuwa wameweka kambi, bahati mbaya baba yangu alikataa kwa
kuofia usalama wangu pindi nitakapo kuwa mbali nae hivyo
ikashindikana.anasimulia mapunda.
mwaka 1993 Mapunda alianza kucheza
soka la ushindani akiwa na timu ya Taiger mbeya timu ambayo alicheza kwa
kujituma sana ambapo kiwango chake kiliongezeka siku hadi siku na mwaka 1997
alitua rasmi katika Timu ya Maji maji maarufu kama wanalizombe toka mkoani
Ruvuma.
mapunda alicheza kwa umaili mkubwa
akiwa na maji maji ambapo aliiwezesha timu hiyo kuchukua ubingwa wa Tanzania
kwa mara ya Tatu mwaka 1998 katka ligi ya muungano na yeye alifunga magori
ambayo yaliiwezesha timu yao kuchukua kombe la ligi ya muungano kwa mara ya
tatu.
Garrincha aliwataja baadhi ya
wachezaji wa kikosi cha wanalizombea ambao walichukua ubingwa mwaka 1998
ni pamoja na Ivo Mang’itu[marehemu],John Alex,Amri Said,Wile Martin,Stivin
Mapunda,Twaa omari[marehemu],Godfrey kikumbizi,Kelvin haule,Said
msham[marehemu] pamoja na Omari Husein ambao waliipeleka Maji Maji kwenye
michuano ya kimataifa.
Hata hivyo kutokana nyota yake
kuendelea kung’ara kwa kiwango cha hali ya juu sana na kusakwa na timu kubwa
hapa nchini ilimlazimu kuipa kisogo timu yake ya nyumbani na
akajiunga na Wekundu wa msimbazi Simba,mwaka 1999,timu ambayo aliichezea kwa
mafanikio makubwa sana na aliisaidia timu hiyo kunyakua mataji mbali mbali
iiwemo kombe la Tasker,ligi kuu bara, pamoja na kombe la mapinduzi lakini kubwa
zaidi alisaidia kuifikisha Simba kwenye robo fainali ya clabu bingwa afrika
mara baada ya kuwasambalatisha vigogo wa soka toka Misri[ Zamareck] kwa
mikwaju ya Penalti na kufanikiwa kuingia Robo Fainali.
Safari yao katika ligi ya mabingwa
iliishia Robo fainali mara baada ya kuchezea kipigo toka kwa Mabingwa wa Ivory
[Isec Mimosas] katika mechi ya marudiano ambayo Simba walichezea Ugenini na
hatimaye wakaaga Rasmi mashindano.
Kurudi Maji Maji.
“mwaka 2005 niliamua kurudi maji maji
kutokana na migogoro ambayo ilikuwepo ndani ya clabu ya Simba hali ambayo
ilipelekea mimi na mwezangu kufungiwa pasipo kujua kosa letu na kututaka
kuandika barua kwa kuwa sikuwai gombana na mtu yeyote ndani ya Simba nikaamua
kuondoka kwa Moyo mweupe na kurudi katika timu yangu ya Zamani Maji Maji
sc.
“niliendeleza soka nikiwa na maji
maji toka milipo Toka Simba kwa misimu Kadhaa na baadae nikaamua
kutundika daruga na kujishughulisha na shuguli za kawaida.
Tukio ambalo sitasahau.
“mwaka 2004 tulifungiwa chumbani
siku 4 nchini Nigeria na ubarozi wa Tanzania ili kutunusulu tusikamatwe mara
baada ya kuchelewa toka nchini Benin ambako tulitoka kucheza kati yetu na timu
ya Taifa ya Benin mechi ambayo tulifungwa goli 4-0,na mara baada ya
kufika Nigeri tulikosa usafiri mara baada ya kukuta ndege ambayo tulitakiwa
kusafiri nayo imeongoka na kipindi hicho Tayari visa yetu ya kubaki
nchini humo ilikuwa imekwisha.
“Barozi wa Tanzania inchi Nigeria
SiSiko ilimlazimu kutufungia chumabani huku tukila nyama kipande kimoja na
mkate mara moja kwa siku kama Gerezani kwa uzembe ambao ilifanywa na viongiozi
wetu,na hatimaye siku ya 4 tulifanikiwa kuondoka na viongozi wetu hawakuwai
kuzungumzia chochote kuhusu tukio lile.
“Inanisikitisha sana kwa timu ya
taifa kukwama ugenini kwa kipindi cha siku 4, mimi binafsi kwa kipindi chote
cha maisha yangu hapa duniani siwezi kusahau”.alisema mapunda.
Ugomvi na ndolanga
“Sababu za mimi kugombana na
mwenyekiti wa Fat Mhidin Ndolanga zilisababishwa na kocha wa timu ya Taifa
kipindi hicho ambaye pia alikuwa kocha wa timu ya prisons ya mbeya Charles
Boniface mkwasa kuwapanga wachezaji wa timu yake ya Prisons katika mechi ngumu
nchini Rwanda kati yetu na Rwanga kwa kuwapa uzoefu wachezaji wake ili wafanye
vizuri ligi kuu bara,na kuwaacha wachezaji muhimu nikiwemo mimi, ambao tulikuwa
tunaaminika ni wachezaji wazuri.
“Wakati mechi ikiendelea Ndolanga
alimtuma mjumbe wake kuja kumhuliza kocha kwa nini mapunda hajaaza katika
kikosi cha kwanza?,kocha alikaa kimya baadae akajibu ataingia,wakati huo hata
wachezaji wezangu benjini walimwambia mapunda inatakiwa aingie akaokoe timu kwa
kuwa tayari tulikuwa tumeshafungwa goli 1 hata hivyo kocha hakuchukua maamzi
yeyote.
“Lakini zikiwa zimebaki dakika tano
mpira kumalizika Mkwasa akaniita kwa Hasira nikapashe ili niingie nikaamua
kukataa kwa kuwa muda ulikuwa umeisha hali hiyo ilimkasilisha na akaamua
kuandika ripoti ya jumla kuhusu mechi hile kuwa Mapunda alikataa kucheza tangu
mwanzoni mwa mchezo ali ambayo ilimfanya mwenyekiti wa Fat akasilike na kusema
kuwa Sitacheza timu ya Taifa hadi hatakapo ng’atuka madarakani.
“Ugomvi wetu ulikuwa mkubwa hadi
ukasababisha waziri Juma kapuya kumfungia Ndolanga kutokana na vurugu ambazo
zilifanyika mara kwa mara kwa wadau na mashabiki wakishinikiza nicheze
mpira,lakini mara baada ya Ndolanga kurudi Madarakani na kukaa kiti kimoja
kuzungumzia mgogoro wetu na yeye kujua Tatizo, mambo yote yakaisha na hadi hivi
sasa mimi na Ndolanga ni Marafiki wa kudumu.
Mechi anayoikumbuka
“Naikumbuka sana mechi ya Clab
bingwa kati yetu Simba na Timu ya jeshi toka Botswana,mwaka2003 ili kuwa mechi
muhimu kwetu na tulicheza katika kipindi kigumu ambapo wachezaji 5 muhimu wa simba
walikuwa wamefungiwa na mimi nilipewa jukumu la ukepteni na mechi hiyo
ilichezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es
salam,mechi ambayo tulipata ushindi dakika ya 89 ya mchezo goli ambalo
liliwekwa kimiani na mimi mwenyewe bara baada ya kubanwa sana na ngome ya ulizi
ya Timu hiyo.
“Watu wengi wakizani kwamba mechi ya
marudiano Tutatolewa kutokana na ushindi mwembamba ambao tuliupata nyumbani
lakini mambo yakawa tofauti, tukiwa ugenini tulicheza kwa morali kubwa na
tukafanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-0,na tukafanikiwa kusonga mbele ambapo
mechi iliyofuata tulipambana na Zamareck ya Misri.
Mchezaji ninayempenda
“Wachezaji wengi wanacheza vizuri
lakini mtanzania anayekipiga Tp Mazembe nchini kongo Mwana Samatta, nampenda
sana ni mchezaji ambaye anatambua cha kufanya pindi awapo uwanjani.
Beki msumbufu kwangu
“kiukweli mabeki walikuwa
wananiogopa,mara nyingi nilikuwa nakabwa na mabeki wane,watatu, kwa kuwa
nilikuwa mtu hatari sana ,mabeki wote nilikuwa nawaweza.
Ushauri wake kwa Timu ya Maji Maji.
“Viongozi wazieshimu pesa za club,na
wahakikishe wanapigana hili kupata pesa za kuendeleza timu, wa ajili ya
mafanikio ya wanamaji maji.
Kuyumba kwa Simba.
“Tatizo ni migogoro ilkiyopo ndani
ya uongozi,simba sio timu mbovu,kinachotakiwa ni viongozi kuondoa tofauti zao
ili kurudisha heshima ya Simba ambayo ni Timu kuwa hapa nchini.
“Lakini pia kupanga kikosi mara kwa
mara,kikosi ambacho sisi tulifika nacho robo fainali kilikuwa na uzoefu wa
miaka mingi na tulikuwa tunacheza kwa kuelewana sana tofauti na kikocha cha
Simba ya Sasa.
Ushauri kwa wachezaji wa sasa.
“Kutokana na kwenda kwa wakati wachezaji wa Tanzania wafanye mpango wa kuwa
na mwanasheria ambaye atakuwa anawakilisha matatizo ya wachezaji kwa uongozi wa
timu ili kuepuka matatizo yanayojitokeza kwa wachezaji na uongozi pindi wanapodai
haki zao kwa kuambiwa kuwa hawana nidhamu hii itasaidia kuwalinda wachezaji.
“asilimia kuwa wachezaji wanakosa
uhuru kwa viongozi wa club na inafikia kipindi mchezaji akidai haki zake
anafungiwa na kuambiwa amekosa nidhamu kutokana na viongozi wetu kujifanya
wanajua kuliko wachezaji.
Maisha Baada ya Soka
“Hivi sasa nimeoa na nina mke na
watoto 3 na umri wangu ni miaka 36 [adi kufikia 2013],namshukuru mwenyezi mungu
kutonana na soka nafahamiana na watu wengi ambao wengi wao tunasaidiana katika
maisha kiukweli mpira umenifungulia dira ya mafanikio yangu.
“Nina ofisi na najishugulisha na
ukandarasi wa majengo pamoja na bara bara,lakini nafikiria kuwa na ofisi kubwa
ili kuhakikisha najijenga vizuri zaidi kimaisha.
Zawadi kwa Watanzania.
“Nina mpango wa kujenga shule ya
soka ‘sports academy centre’ambayo itafundisha mpira kuanzia ngazi ya chini ili
kuwapata wachezaji wenye uwezo wa hali ya juu ya kucheza soka hapa nchini.
“Natarajia baada ya muda mfupi
ujenzi utaaza kwa kuwa tayari taratibu za awali zimeshakamili na shule hiyo
natarajia kujenga mkoani Ruvuma.alisema Garrincha.
Chapisha Maoni